Mtoto aliyekojolea msaafu kortini...

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Gazeti la majira limeripoti ya kuwa mtoto aliyekojolea msaafu atafikishwa mahakamani ili sheria za nchi zifutwe.

Maoni yangu ni kweli kitendo cha mtoto huyo kilikuwa cha kitoto na cha kijinga. Ila lilofanywa na kundi la waislamu kuandamana dhidi ya kitendo hicho cha mtoto, na kuharibu malia za watu pamoja na makanisa ni zaidi ya utoto, ujinga na na pia uwendawazimu.

Hivyo wakati yule mtoto akipandishwa kortini polisi wanapaswa kuwapandisha mahakamani watu waliohusika na wendawazimu huo pia.

Polisi pia inapaswa kuonesha wale waliochoma makanisa Zanzibari wapo wapi?

Vinginevyo ujinga na wendawazimu huu utatupeleka pabaya.
 
Tz raha jamani...wakubwa hawaguswi...aliemshawishi kimya....
 
I am tired of this shit! Ignorance is more than the devil. Mtu akikosa elimu ya kujitambua ni hatari mno, haya ni matokeo ya kukosa elimu kwa kundi kubwa la watanzania.

Pengine yanaonekana kuwa ni masuala ya kawaida lakini sababu kubwa ni serikali kukosa mipango madhubuti ya kuwasaidia wananchi wake. Matokeo yake wanapopewa elimu isiyo na faida kwao basi wanachukulia ni sahihi. We need to wake up, haifai kuanza kugombana sisi kama ndugu, watu tuishio pamoja.

Kama kuna watu wanatumiwa kutugawa, basi UWT ndo kazi yao. UWT acheni uroho, tamaa ya fedha fuateni maadili yenu ya kulitumikia taifa. Saidieni watanzania maskini, wajinga pamoja na weny kuhitaji msaada.
 
Issue kama hizi zinahitaji busara sana kudeal nazo. Sasa hawa watawala wetu hamna kitu kabisa aisee!

Yaani aliyekojolea msaafu anapandishwa kizimbani; wanaochoma magari, makanisa na mali wanadunda mitaani?
 
Pamoja na kwamba kitendo alichokifanya huyo mtoto ni kosa lakini kumfikisha mahakamani sahihi kabisa. Kwanza watu wazima wameandamana wakitaka kumuua, halafu siku 2 baadaye anapelekwa mahakamani!

Jamani, huyo mtoto ana miaka 14 tu. Hivi hakuna mtu mzima wa kumuelewesha badala kumpa mlolongo wa manyanyaso?
 
Msichanganye issue, kuna mtoto mmoja wa Pemba alikojolea Msaafu siku mbili kabla ya Mbagala... Kesi yake ipo Mahakamani huko Pemba!
 
Mtoto huyu anapelekwa mahakamani harakaharaka mbona waliochoma makanisa kule Zanzibar, Dsm na sehemu zingine hatujasikia wakipelekwa au wako juu ya sheria?
 
mimi ni muislamu....kufikishwa mahakamani mtoto huyu si sahihi!
Mkuu tunajijengea chuki sisi wenyewe. Sijui kwa nini watu wanaacha upendo wa kuthaminiana wa kawaida kabisa ambapo mtu anakuwa nao hata bila kuupata kanisani au misikitini!! Jibu ni moja tumeacha mila na desturi zetu nakuanza kufuata za watu wengine bila kujua misingi yake.
Mimi kama mkristo, sidhani kama ni dhambi nikikukaribisha kanisani nikakufundisha yale ninayoamini bila kukushurutisha baadae tukaenda msikitini nikakusikiliza ukiniambia yale unayoyaamini bila kunishurutisha. In a long run utajikuta kila mmoja anaishi kwa amani na upendo.
Kuna baadhi ya wachungaji ukiwasikiliza mahubiri yao, unaweza kurusha bomu liwapoteze usoni mwa dunia; hivyo hivyo kuna baadhi ya maimamu ukisikiliza mahubiri yao ni hatari. Na kuna baadhi ya wachungaji ukiwasikiliza unapenda kuendelea kuwasikiliza na unaweza kutamani ujiunge nao, hivyo hivyo kuna baadhi ya masheikh ukiwasikiliza mafundisho yao unasema why am I a christian?.
Lakini yote hayo yapo katika jamii zetu na pengine watu wanayafahamu ila kutokana na kuacha mila na desturi zetu tunayaapuuza.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom