Mtoto akilea Mtoto Mwenzake

Kijijini hii ni kawaida but, aliyebebwa mbona mkbwa sana? Na aliyebeba kama vile hawezi kunyanyuka nae?
Au dogo kalala then hawezi kumlaza, so imebidi akae ili apumzike wakati dogo anachapa bonji.
Inahuzunisha!
 
To be honest, hii picha inasikitisha na inatoa ujumbe mkubwa sana kuhusu jamii tunamoishi!! Ukimwangalia mtoto aliyebebwa ana afya njema, ni msafi na amevaa viatu, kwa hiyo hawa sio masikini wa kupindukia.

Ila mtoto aliyembeba anaonekana mchafu na asiye na matumaini katika maisha. Sura yake inaelezea masaibu mengi aliyonayo katika maisha.

Nikifikiria kwa haraka haraka ni kwamba mtoto huyu aliyembeba mwenzake atakuwa analelewa na mama wa kambo, ama ni yatima aliyekosa mwelekeo wa maisha na kuambulia kupewa ajira ya watoto. Usishangae kwa Tanzania kwamba mtoto huyo aliyembeba mwenzake akawa ni ''housegirl'' wa mtu anayefanya kazi ofisini na amesoma shule kabisa !

Mkuu Masaki ukiwaangalia hawa watoto kwa karibu wanafanana, labda huyu mkubwa alikuwa akicheza hivyo alikulupushwa na kumchukua dogo bila ya kuvaa viatu, tazama nguo yake pia sio mbaya, hapo labda dogo anapatwa na donge kwa nini ameachishwa mchezo kwa sababu ya mdogo wake, mi pia nakumbuka tulikuwa tukigombania kubeba watoto hata wa jirani yako kama wewe hauna mdogo wako hila yote yanawezekana: House girl, mama wa kambo, mdogo wake tumbo moja, mama mmoja baba mmoja au hata ni utashi wake inawezekana amebeba mtoto wa jirani
 
Back
Top Bottom