Mtoto afukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu 'dagaa anaitwaje kwa kiingereza'

Dagaa unaweza pia kuwaita 'sprat' au kwa kitaalamu 'stolothrissa' (vz. stolothrissa tanganicae - dagaa wa kigoma(ziwa tanganyika!))

Kumbe walimu namna hii bado wapo? Nilifikiri enzi zetu sisi tuliosoma vijijini ndio ilikuwa ngumu kumuuliza mwalimu, enzi izo kwakweli utachezea fimbo hadi ukome mwenyewe! Huyu mwalimu nae hana maadili ya kazi yake! au ndio wale wa voda fasta?

i just remember nikiwa class 3 miaka hiyooo ndo tunaanza kujifunza na kuruhusiwa kutumia kalam za wino.... na kuanza kujifunza chirengeza. walim akauliza nani anaweza kuniambia maana ya razor blade.... uuuuuwi sitaisahau ile siku mweee. watu haraka haraka vitoto tukafikiria na kuambizana.. ni rozari ( aka tasbihi) kiongozi wa kujibu akanyoosha mkono, ticha ticha mii mii hia. Eh mwalim akamwona. akajibu kwa sauti kuu ... iz tasbihi. tukajiandaa kumpigia mwenzetu makofi ya pongezi. wee mwl akatahamaki. akaendelea kuuliza mmoja mmoja. woooote tulishaambizana tukajibu ze sem weee. tukapewa muda tukaulize madarasa ya juu wakati wa breki... loooh hakuna aliejua. basi tukalambwa mojamoja then akatuonesha kiwembe.

Mkuu thanx. but Hawa ni wa baharini (Hasa bahari ya hindi) halafu umbile lao ni kubwa kidogo.
Je wale wa ziwa Tanganyika na Victoria wanaitwaje kwa kidhungu?

Kwani Simba wa Serengeti anaitwa Lion kwa kiingereza yule Manyara anayepanda miti anaitwaje kwa kiingereza?

Hahahah! lol! hii kali! Mbavu zangu zinauma!
i just remember nikiwa class 3 miaka hiyooo ndo tunaanza kujifunza na kuruhusiwa kutumia kalam za wino.... na kuanza kujifunza chirengeza. walim akauliza nani anaweza kuniambia maana ya razor blade.... uuuuuwi sitaisahau ile siku mweee. watu haraka haraka vitoto tukafikiria na kuambizana.. ni rozari ( aka tasbihi) kiongozi wa kujibu akanyoosha mkono, ticha ticha mii mii hia. Eh mwalim akamwona. akajibu kwa sauti kuu ... iz tasbihi. tukajiandaa kumpigia mwenzetu makofi ya pongezi. wee mwl akatahamaki. akaendelea kuuliza mmoja mmoja. woooote tulishaambizana tukajibu ze sem weee. tukapewa muda tukaulize madarasa ya juu wakati wa breki... loooh hakuna aliejua. basi tukalambwa mojamoja then akatuonesha kiwembe.

Wanafunzi wa siku hizi wadadisi kweli kweli sasa usijeshangaa kakutana na mwl. Anayeishi nyumba ya kupanga tena ya chumba k1, amekatwa mshahara kisa mkopo aliochukua kumlipia ada mwanaye na hajawahi pata masurufi tangu aajiliwe na fungu la memkwa na mmem ndo siku hizi inafuatiliwa mpaka senti ya mwisho kwa mwl ambaye kwake dagaa ni chakula cha wageni tena mwisho wa mwezi ww ulitegemea nini? Usishangae asbh mama watoto alimwambia dagaa wameisha na yuko hali mbaya. Dk. Slaa aliwahi kusema jamii au nchi ya watu waliokata tamaa ni hatari sana.

small fish! .. hehehe

http://www.kamusi.org/en/lookup/sw?Word=dagaa

dagaa mchele je..?

shukrani kwa kufahamu mi nlikuwa sijui!

small fish! .. hehehe

http://www.kamusi.org/en/lookup/sw?Word=dagaa

dagaa mchele je..?

Hao watakuwa 'smalk fish rice'

hata mie ndio nimejua leo jina la dagaa. Nilijua ni 'small fish'.. Kweli hii lugha ya Kiingereza ni janga la Taifa, linafuatia baada ya Ukimwi..

hahahaaa, Mayasa!! umenichekesha sana hapo kwenye bold!

ubarikiwe sana mpendwa!

Hapana mkuu, ila nimewahi kufundisha sana sunday school kanisani, watoto wana maswali hadi unaweza kuchanganyikiwa, kuna siku waliniuliza "mwalim, hapo zamani kulikuwa na utupu wakati Mungu anaumba dunia, ina maana kulikuwa hakuna kitu chochote duniani, sasa huyu Mungu wakati anaumba hiyo dunia alikaa wapi?

Nimeipenda hiyo red!

Nakumbuka nikiwa darasa la tatu kuna mwenzetu alimuuliza mwalimu "what is your clan" akachemsha akasema ntakujibu kesho

Sometimes walimu wakishindwa wanaweza kuzua lolote...mimi nilipata kipigo kutoka kwa mwalimu na mpaka leo sijapata jibu kwa nini nilipigwa,ilikuwa hivi....tulikuwa na kipindi cha dini,karibu na kipindi kwisha mwl aliruhusu maswali,nakumbuka utotoni tunaambiana mengi kwa dhana tu,mojawapo tulikuwa tukiambiana eti kaburi kwa bahati mbaya siku ile lilipochimbwa ikatokea dharura na mazishi kutofanyika eti inabidi lilale na mgomba.."utoto" lakini mimi lilinikaa akilini na nilipopata nafasi nilimuuliza mwalimu wa dini,ikitokea hali kama hii kidini inabidi nini kifanyike? weee! nilipigwa nilipigwa ,ni zaidi ya miaka 20 sasa lakini sijasahau na wala sitosahau mpaka leo sijapata jibu kwa nini alinipiga.

Back
Top Bottom