Mtoto afukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu 'dagaa anaitwaje kwa kiingereza'

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
Mwanafunzi wa shule ya msingi Kakuyu amefukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu wake wa Kiingereza ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa dagaa kwa Kiingereza anaitwaje?

Mwalimu huyo aliposhindwa kujibu swali hilo alihamaki, akamcharaza mtoto huyo bakora sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake na akahitimisha kwa kumwandikia barua ya kumfukuza shule kwa madai ya utovu wa nidhamu na kutumiwa kama kibaraka wa maadui wa mwalimu huyo.

My Take:
jamani elimu yetu Tanzania ni wapi inakoelekea?
Je tuna walimu ama tuna maamuma?
 
Kama nawatch movie hali ilivyokuwa hapo class. Maticha wengine ni waduanzi kinoma.
 
Najaribu kufikiri namna huyo Mwalimu alivyokuwa akiongea kwa ki-english.
Wee pupils you know me? I will beat you and go speak to your father. You play play with me, I am another. Mmmhh"
 
Huenda alimwambia hiviiii... "Yuuu Pyupuli donti Follo follo mii... Aiii wiliii tichiii yuu ze lessoni...Umetumwa na nani? Kamoooonii...
 
Hebu niambieni wakuu,
Hata mimi sijui dagaa kwa kungereza anaitwaje!!
 
Duuh! Mkuu wa shule kakosea kabisa,kawaida walimu tuna approach nyingi za kumjibu mwanafunzi kama ameuliza na nikajiona cwezi kulijibu mfano
1.Njoo baadae au kesho
2.Nakupa assignment kesho unijibu e.t.c
Hebu nawewe niambie ungekua ndio mkuu na haujui maana ake ungefanyaje?
 
Tunamhukumu mwalimu wa watu bureee...haya wataalam wa lugha, dagaa kwa kidhungu? twasubiri, tusije ulizwa na wanetu halafu majibu yakawa kama hayo ya mwalimu!
 
Huyu mwalim hana mbinu za kujibu maswali, na inaonyesha kama hana jibu la swali aliloulizwa ana panic haraka badala ya kutafuta solution, kama Laurence alivyosema hapo juu, angetakiwa amrudishie yeye mwenyewe swali hilo au angemuambia nakupa home work kesho saa 4 nipatie jibu, au kumbe wewe unapenda dagaa ee!! kwani kuna dagaa wa aina ngapi? akishindwa unampa home work unamuambia unapaswa ujue aina za dagaa kwanza kwa hiyo nenda kesho uniletee aina za dagaa halafu nitakuambia dagaa wanaitwaje kwa kiingereza. Hapo hawezi kugundua kwamba hujui na kesho utampa jibu sahihi
 
Back
Top Bottom