Mtoto abakwa na baba mlezi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Polisi mkoani Mbeya inamshikilia Joseph Mtawa, kwa tuhuma za kumbaka binti yake anayemlea mwenye umri wa miaka saba.

Mtuhumiwa huyo mkazi wa kijiji cha Shigamba Wilaya ya Mbeya Vijijini, alimbaka binti yake wa kambo baada ya kumvizia mtoto huyo akiwa amelala sebuleni saa tano usiku .

Alidaiwa kuwa alimtoa binti yake sebuleni na kumpeleka kwenye pagare na kumfanyia kitendo hicho.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani alisema mtuhumiwa huyo yupo rumande na atafikishwa mahakamani baada ya taratibu kukamilika.

Ilielezwa kuwa tukio hilo liligunduliwa na mama wa mtoto huyo mwenye miaka 27 (jina linahifadhiwa) ambaye alipiga kelele za kuomba msaada kwa majirani waliomkamata na kumfikisha polisi.

Kamanda Athumani alitoa wito kwa wananchi kuepuka vitendo vya udhalilishaji ambayo ni kinyume cha haki za binadamu na ustawi wa watoto.

Mara nyingi matukio kama haya yamekuwa yakitokea majumbani na yamefanywa na watu walio karibu na watoto ama ndugu zao na yamekuwa yakihusishwa na ushirikina .
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Back
Top Bottom