Mtoto Aangua Kilio Wakati wa Kuingizwa Kaburini

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mtoto mchanga wa kike wa nchini Brazili aliyetangazwa amefariki punde baada ya kuzaliwa aliangua kilio wakati anatumbukizwa ndani ya kaburi lakini alifariki baada ya kuokolewa na kufikishwa hospitali.
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi saba alijifungua mapema hospitalini kabla ya muda wake.

Lakini madaktari wa hospitali ya Santa Casa de Misericord katika mji wa Araxa walitoa taarifa muda mfupi baadae wakimwambia kuwa mtoto wa kike aliyejifungua alikuwa amefariki.

Taarifa ya madaktari ilionyesha kuwa mtoto huyo alifariki wakati wa kuzaliwa.

Wakati maandalizi ya mazishi yalipokamilika na maiti ya mtoto ilipokuwa ikiingizwa kaburini, mtoto huyo aliangua kilio hali iliyowashtua watu na kugundua kuwa mtoto huyo kumbe alikuwa hajafariki.

Kichanga hicho kiliwahishwa kwenye hospitali nyingine tofauti na kulazwa kwenye chumba cha watu mahututi.

Haukupita muda mrefu taarifa ilitolewa kwamba mtoto huyo amefariki dunia.

"Amefariki dunia baada ya ogani zake muhimu kushindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa oxygen kwenye damu", alisema msemaji wa hospitali aliyokuwa amelazwa mtoto huyo.
 
huyo malaika alikosa hewa, kumbe na madaktari wa huko juu wapo vilaza pia.
 
Back
Top Bottom