Mtizamo wangu kuhusu taarifa za CAG hasa katika (LGAs)

diwan

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
308
114
Heshima mbele wanajamiii! Nimeamua kuja na mtizamo na angalizo juu ya report ya CAG ambayo ndio “The hot story kwa sasa”. Mtizamo wangu, mawazo yangu na ushauri wangu unatokana na uzoefu wangu katika kufanya kazi katika Serikali za mitaa ingawa kwa sasa nilishaachaUTANGULIZISheria zilizoanzisha Serikali za mitaa zinaitambua Halmashauri kama taasisi ambazo zina mamlaka yote kama zilivyo Wizara mbalimbali ila hili si kweli kwani Halmashauri, ,Manisipaa, Miji na Majiji bado zipo chini ya Wizara Mbalimbali katika kutekeleza majukumu yake. Yaani bado tegemezi kuanzia upangaji wa matumizi na Utekelezaji wa shughuli mbalimbali. Wizara ya TAMISEMI inajumuisha wizara na idara nyingine zote katika utekelezaji wa majukumu yake katikaa Halmashauri Manispaa, Miji na Majiji kama, ARDHI, FEDHA,MALIASILI, WVBM n.k.HALI HALISI YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KATIKA SERIKALI ZA MITAA.
Halmashauri zetu zimekuwa zikipanga bajeti kutokana na vipaumbele ambazo hupitishwa katika ngazi mbalimbali za maamuzi(Vikao vya kamati za madiwani ,Baraza la Madiwani, RCC na hatimaye kupitishwa bungeni.
Ila si kwamba kila kilichoombwa katika halmashuri iwe OC(Other Charges) au DEV(Miradi ya maendeleo) huwa kinakuja kama kilivyopangwa. Mara nyingi pesa hizi huja ama nusu, robo tatu ya kile kilichokuwa kimepengwa. Hivyo Halmashauri hutumia fedha hizo kutokana na vipaumbele kulingana na pesa iliyopokelewa. UKWELI KUHUSU UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA KATIKA HALMZASHAURI ZETUNi kweli katika halmashauri zetu baadhi ya watumishi hasa wakuu wa Idara/Vitengo wamekuwa wakitumia vibaya fedha zinazopokelewa katika idara zao. Hii ni kutokana mianya iliyopo katika uadaaji na utekelezaji bajeti za serikali iwe Serikali kuu/za mitaa. Mfano 1. Ulianzishwa mfumo wa EPICOR system katika Serikali za mitaa na uliigharam serikali Billions of money kwa ajili ya ununuzi wa vifaa, na mafunzo kwa Wahasibu leo huu mfumo uko wapi? Unatumika?na kama unatumika je unatumika ipasavyo? Haya ndio maswali ya kuanza kujiuliza? Kuna mfumo mzuri sana wa uandaaji wa bajeti na Matumizi katika serikali (PLANREP) je unatumika ipasavyo? 2. Ziara za Mawaziri makatibu wakuu na viongozi wengine wakitaifa akiwemo Rais na misafara yake katika Halmashauri na mikoa. Kama nilivyoanisha hapo juu ya kuwa fedha zinazoanishwa katika Bajeti zinakuwa allocated tayari kwa matumizi kutokana na Bajeti, Na mara nyingi tunaona viongozi wetu wakiwataifa wakikagua shughuli za maendeleo katika serikli za mitaa kama Ufunguaji wa Miradi, Ukaguzi wa miradi n.k. Kiuhalisia hawa watu wakifika katika Mikoa au wilaya gharama kama Malazi,Chakula, Mafuta hugharamiwa na Mikoa/Wilaya husika hizi unafikiri huwa zinatoka wapi kama sio hizo hzo za maendeleo na uendeshaji wa Ofisi za Halmashauri. Na kwa kuwa huu utaratibu katika maombi ya Fedha huwezi ainisha kuwa ni Posho ya Mh fulani. Hutafutiwa kazi ambayo ilitakiwa kutekelezwa pale. Sasa Je Wilaya zetu zinatembelewa na Viongozi na watendaji wakuu wa kitaifa mara ngapi kwa mwaka?3. Naomba tukubaliane kuwa sio kila Halmashauri iliyopata hati safi ni kweli safi, ila kila Halmashauri iliyopata hati chafu ni kweli chafu. Hii namaanisha kuwa 95% ya Halmashauri zote Tanzania ni chafu . Hii ni kutokana na maelezo 1 na 2 hapo juu. Ila inabidi mjuwe kuwa hizi hati zinapaitikana kutokana na how the Director katika halmashauri husika anawapokea na kuwatreat watu wa NAO pale wanapokuja kumkagua.. Tukumbuke kuwa hii nchi kwa sasa kabisa kiukweli ili mambo yako yaende ni lazima uwe na chochote mkononi. Hivyo tusijidanganye hata siku moja kwamba waliopata hati safi ni wasafi HALMASHAURI KUKOSA MTETEZI BUNGENIWabunge ndio wawakilishi wa wananchi katika vyombo vya kutunga sheria, usimamizi wa serikali na uwajibishaji wa serikali iwe za mitaa kupitia vikao vya Madiwani na Bunge. Ni ukweli usiofichika kuwa wabunge wetu ukipita uchaguzi wakishatangazwa mara nyingi tunawaona bungeni tu. Hivyo hawafiki majimboni kusikiliza kero za wananchi,kusimamia miradi ya Maendeleo au kushiriki vikao vya madiwani ambavyo ni wajumbe. Kama kuna Mh Mbunge anabisha juu ya hilo ajitokee. Ukipitia mihtasari ya Vikao vya Madiwani eneo la Mbunge ,wengi wapo kwenye wajumbe wasiohudhuria na reason kama sio kwa taarifa basi ni Bungeni. Mfano Hivi Ubadirifu wa Kishapu 6 biln ulifanyika ndani ya mwezi mmoja? Uwajibikaji ungeanzia hata kwa Wah Madiwan na Wabunge wao maana kwa mujibu wa sheria ya Uendeshaji wa vikao vya madiwani kuna kikao kimoja kila mwezi cha finance, Je walikuwa wapi?au tatizo la shuleInasikitisha sana kuona Mh Mbunge au anauliza swali kwa Waziri ambalo jibu lake lipo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika. Mi naona kuna haja ya hoja nyingine zijibiwe na Wabunge kwa sababu zinatoka majimboni kwao.Hizi ripot za CAG zinapelekwa na kusomwa kwenye Baraza la madiwani, Na katika baraza la madiwani wataalamu huwa wapo ambao ndio mwenye kujibu hoja husika au kuwajibika. Ni kitu cha ajabu kuona mjumbe wa baraza anatoa mapendezo Bungeni ambayo alitakiwa kuyatoa katika barazahilo. Ni vizuri bungeni zikajadiliwa hoja ambazo ziko nje ya Uwezo wa Halmshauri kuliko kupoteza kodi za watanzania mkijadili Mfano.ubadhirifu wa Mtendaji wa kijiji Bungeni.Sio kwamba katika Wizara nyingine Hakuna ubadhirifu sababu ni ile ile 1,2&3. Bali kutokana na wizara kuwa na idadi za watumishi na kazi chache pia kwa kuwa zinakuwa na uwakilishi bungeni(Waziri) ndio maana imekuwa ni rahisi hata kupangua hoja zinazozikabili kwa wakati hivyo kukosa nguvu tofauti na Halmashauri ambazo Wakurukenzi wao hawaendi Dodoma kumsaidia katibu mkuu kujibu hoja zinazomkabili Waziri wao.NINI KIFANYIKE1. Uwajibikaji wa kila mtanzania mahali pale alipo kuanzia raia asiye na kazi, mwanasiasa, wataalamu na viongozi mbalimbali ili kuleta maendeleo endelevu kwa mustakabali na ustawi wanchi.2. Kila mtanzania anaishi kwenye mtaa/Kijiji. Je unashiki vipi katika kupanga, kuchangia, kutekeleza na kusimamia maendeleo ya mtaa/kijiji chako? Je unapata au ushafuatilia taarifa ya Mapato na matumizi kutoka mtendaji wa kijiji/mtaa?. Hivyo kila mtanzania anatakiwa ajue wajibu wake katika kuleta ustawi wanchi.3. Kutokana na repoti ya CAG hiyo iliyopita naamini wakurugenzi katika Serikali za mitaa wameshituka hvyo mkae mkijua kuwa kwa mfumo huu tulionao watu wa NAO watanunuliwa sana ili kuandika taarifa nzuri(Wako wapi TAKUKURU) 4. Kuna haja ya kusisitiza a Full utilization of EPICOR system na PLANREP naamini this is the best way ya kupunguza ubadhirifu serikalini kwa ujumla.5. Tuanze kukaguana sisi kwa sis kuanzia ngazi za chini maana pesa za miradi kwa sasa nyingi zinapelekwa ktk serikali za vijiji/mitaa hivyo tusipokuwa makini tusubiri makubwa zaidi. Kwa kupata au kuwataka watendaji wa mitaa/vijiji kutoa taarifa za mapato na matumizi.6. Watanzania tusiwe wepesi wa kulaumu na kulalamika pasipo kujuwa wajibu wetu, tuache itikadi za kisiasa tushauriane kwa kutumia elimu na taaluma zetu. Naamini kwa paoja tutafika.7. Kuna haja ya kuangalia weledi na uzalendo wa watawala wetu. Haina mashiko kuwa na muwakilishi mwenye Elimu ya STD 7 katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na technologia.Hili ni tatizo sana kenye Halmashauri. Mwisho nawakaribisheni kwa majadiliano, maoni,nyongeza,angalizo kwa maendeleo ya nchi yetu.

Angalizo; Itikadi za vyama pembeni masilah ya Taifa mbele
Kariiiiiiiiiiib.
 
Mode...Naomba uiweke katika paragraph coz naona imekaa katika mkao ambao c mzuri sana.
 
Unenena vyema mie mwananchi nitaingiaje huko wanakopanga mapato na matumizi

Ndugu uandaaji wa bajeti unaanzia kwenye kijiji/Mtaa unaoongozwa na Mtendaji wa mtaa au kijiji. Mipango hiyo ambayo inazingatia vipaumbele vya eneo husika hupelekwa Halmashauri kuwa compiled. Bajeti hizi hupitishwa na kamati za kudumu za madiwani na mwisho Baraza la madiwani. Pia taarifa za mapoto na matumizi huwasilishwak kila mwezi kwenye kikao cha Finace. Halkadhalika inatakiwa hivo kwenye mtaa/kijiji.
 
Kutoingia raia wengi katika michakato ya bajeti ndio tatizo kubwa katika kupanga na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma.

Wananchi wanaweza kuingia kwa ama kusikiliza ama kujiunga watu 5 kama sheria ya serikali za mitaa inavyoelekeza...mnapeleka maombi yenu halmashauri husika ya kutaka kuhudhuria baraza na kama mana jambo mnalotaka kuwasilisha mnaliweka....mtapewa muda wa kuwasilisha na kama hoja zinatimia litajadiliwa ama mtapewa maelekezo...

Kwa kuwa wengi wetu hatuna muda ama hatutoi muda kwa mambo kama haya, hatujui kinachojiri hadi bajeti za serikali zinatengenezwa, kutolewa, kusimamiwa na kutekelezwa...Anza sasa utajua, utaona utaelewa, utajifunza, utashiriki, utajipa haki yako ya kujua na kushiriki maendeleo ya eneo lako. utajua wanaposema matumizi mambaya wana maanisha nini...nk
 
Punguzeni matumizi hewa nyinyi

Ndugu yangu nahisi hujasoma nilichoandika hapo juu. Ila kwa kuwa mmeshezoea kusoma hoja zenye mistari miwli naomba ulewe kuwa.
1. Ni kweli kuna matumizi hewa. Lakini haya matumizi hewa yanatokana na nini(Source)
Hii ni kutokana na kutokuwa na bajeti ambazo zinaeleza uhalisia wa mambo. Mfano Hivi safari za Rais Wilayani huwa zipo kwenye Bajeti za Halmashauri?(kumbuka safari za raisi zina gharama kubwa saaana maana haji yeye peke yake) sasa ujue kuwa halmashauri huchangia kugharamia chakula, zawadi, malazi,Mafuta na kwa ajili ya msafara.
2. Mawaziri na Viongozi waandamizi wa Wizarani wanapotembelea Halmashauri hawatumii posho zao walizochukua kule, Bali huandaliwa mazingira ya kuwezeshwa na Halmashauri husika. Na kwa kuwa wanakuwa walishasaini kule(Wizarani) huwezi ukaandika request(DOKEZO) ya posho ,chakula au malazi kwa viongozi hawa inabidi uandike activity uliyokuwa umeipanga ambayo ndio itabidi uifute (Kumbuka budget iz fixed)
3. Hivyo kwa kuwa tayari kuna hii system ambayo ni week. Imesababisha watumishi kutumia hizi hizi nafasi kurequst pesa na kuzitumia visivyo.

Bado naamini tunayo nafasi. Kama Raisi anatembelea Wilaya fulani basi Ofisi yake(Ikulu) Igaramie the sema as Mawaziri kulikokuwa na Double expenditure kwa kazi moja.
 
Kutoingia raia wengi katika michakato ya bajeti ndio tatizo kubwa katika kupanga na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma.

Wananchi wanaweza kuingia kwa ama kusikiliza ama kujiunga watu 5 kama sheria ya serikali za mitaa inavyoelekeza...mnapeleka maombi yenu halmashauri husika ya kutaka kuhudhuria baraza na kama mana jambo mnalotaka kuwasilisha mnaliweka....mtapewa muda wa kuwasilisha na kama hoja zinatimia litajadiliwa ama mtapewa maelekezo...

Kwa kuwa wengi wetu hatuna muda ama hatutoi muda kwa mambo kama haya, hatujui kinachojiri hadi bajeti za serikali zinatengenezwa, kutolewa, kusimamiwa na kutekelezwa...Anza sasa utajua, utaona utaelewa, utajifunza, utashiriki, utajipa haki yako ya kujua na kushiriki maendeleo ya eneo lako. utajua wanaposema matumizi mambaya wana maanisha nini...nk

Yap dadangu; Watu wamekuwa mabingwa wa kulaumu na kulalamika pasipokujua kuwa wao ndio tatizo.
 
Back
Top Bottom