Makyomwango
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 322
- 79
Ukweli huu usiopingika ni alama dhahiri umesoma sana mwenendo wa huyu mpigania haki mashuhuri katika nchi hii tangu mfumo wa vyama vingi uingie nchini.
Umashuhuri wake zaidi umejionyesha pale watanzania wengi kutomuunga mkono katika hoja zake kivitendo ingawa zinasomeka wazi ni za msingi na muhimu. Pamoja na kuwa peke yake hakukata tamaa amekuwa mpiganaji kuwashinda wale wa vita vya msituni hadi kuitikisa serikali mahakamani na kuishinda mara kadhaa licha ya vitisho kama katika kesi yake iliyomalizika leo kusingiziwa.
Wanasiasa wengi Tanzania hasa vyama vya siasa hawajaonyesha ushirikiano na mpigania haki huyo kwa kile tulichokizoea kukosa umoja kwa vyama vya upinzania hali ambayo imechelewesha hata mageuzi Tanzania tofauti na nchi kadhaa zinazotuzunguka katika kuendesha wimbi la mageuzi ya kweli kwa kukata mzizi wa fitina unaolindwa na watawala kujizatiti kwa kupokezana vijiti kana hatuna wenye uwezo na nafasi ya kufanya hivyo.
Mtikila udhaifu wake pia wa kutowakubali au kuwapa nguvu wanasiasa wenzake katika vyama vya upinzani huenda ni chanzo cha kutopata ushirikiano wa kutosha, hata hivyo sioni kama hoja ya kutompongeza kwa vile ayafanyayo ni mahsusi kwa demokrasia ya kweli katika nchi yetu, kama wastaarabu na waungwana tuna haki ya kumpongeza kwa nguvu moja kwa ushujaa alio nao, kwani amepigania haki za watanzania wote bila kujibakisha hadi kufikia pengine kuhatarisha usalama wake, ila tegemeo lake kama mchungaji ni Mungu pekee.
Naam, histori haitamwacha mtu huyu mashuhuri katika kutetea demokrasia ya kweli nchini mwetu bila woga, bila kukata tamaa, hadi kuishinda serikali mahakamani mara kadhaa kwa nia moja tu kutetea wanyonge wa taifa letu.
Ipo siku utajengwa mnara wa kumbukumbu yake katika kijiji alichozaliwa kiitwacho Milo kando ya mapangano ya milima ya Livingstone huko Upangwani iliyojipindapinda na magenge mengi kuteremkia bonde kuu la ufa huko Ziwa Nyasa ambako wenyewe wa huko ni sawa na nabii hakosi heshima ila katika nchi yake mwenyewe, aka wilayani Ludewa kwa mwanamapinduzi mwenzake Deo Filikunjombe.
Hakika huyo ni shujaa wetu. Sifa nyingi alizonazo mzalendo huyu na ambazo zimeandikwa katika thred hii mara nyingi hutolewa mtu akifa lakini kwa mchungaji zimetolewa kabla hajafa. Mambo haya hutokea mara chahe sana