Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa wangu...

Mfano wake huwezi kufananisha na UNABII unless wewe unachukulia UNABII ni kitu kidogo sana..Sasa unataka kunambia yeye anapewa wahi na Mwenyezi Mungu au anapokea kutoka wapi kama sii maslahi yake mwenyewe. Na wala haitaji kuandikiwa barua, mchungaji angesimama kuonyesha mfano bora zaidi kabla hata ya wewe kufikiria.

Mfano wako ungekuwa sawa na uzito wa hoja zake maana hawakilishi watu bali yeye mwenyewe, mtu isha kula hela za Rostam unabii ataupata vipi. Kila kesi anayoshinda inamweka yeye mahala na sio wananchi. Demokrasia inapiganiwa pale hakuna Demokrasia lakini kachumbari ya demokrasia kwa manufaa yake yeye huwezi kuita ni demokrasia. Nimesema Mgombea Binafsi anayekubaliana na itikadi za CCM lakini hapatani na watu wengi CCM huyu hana deal ni Mbinafsi tu kama Shibuda..
Mkuu tuachane na hayo ya unabii kwasababu tafsiri zake ni tofauti kutegemea na dini.So mtapishana tu na mjadala utaharabikia.Ushauri tu.
 
Vizuri umesema HERO WAKO lakini sii wangu miye kwa sababu siku zote anapigania haki yake yeye na sii ya WANANCHI. Kama nguvu hii ageiweka ktk kupigania haki za wananchi bila shaka kama sio mwaka 1995 basi 2000 angechukua nchi..MTIKILA ni Mbinafsi, mtu anayependa sana kutetea na kulinda maslahi yake kama mgombea..
Mkuu Mkandara, asante kwa kuongelea ubinafsi!. Ni kweli Mtikila ni Mbinafsi, So does Chadema, CUF and NCCR-Magauzi!. CUF had to join CCM in GNU not because it wished, but because it had to under the principle of "If you can't beat them..."!. Kwenye ule uzi wangu wa "Chadema Haijajipanga", nimelizungumzia hili, kuwa kama ni kweli Tanzania ni nchi moja yenye Bara na Visiwani, na ili Chama kishinde urais wa Tanzania, ni lazima kipate asilimia fulani ya kura za Zanzibar, niliwaambia Chadema, "Peke Yenu, Hamuwezi!", mtake msitake "Ni Lazima Mshirikiane!" na "Umoja ni Nguvu!".

Mtikila ni Mbinafsi na ataendelea kuwa hivyo kwa sababu hapo alipofikia ni "All the he wants!" and doesn't expect anything more!, Nilipokutana nae two years ago, nilizungumza nea kuhusu hili la Ubinafsi wake na nilipandisha hii thread humu, News Alert: Uso kwa Uso na Mtikila- Akataa Hongo ya Millioni 100!.

Na kama kawaida yake, 2015 atagombea tena urais!, just to be there na ataibomoa Chadema kisawa sawa, japo ubomoaji wake hauna impact kubwa kwa Chadema zaidi ya ku "inflict pain on the neck!". Kwa Chadema ambacho it wants more, ni lazima kishirikiane ili to get that more!. Ubinafsi hautawafikisha mbali!.

Mtikila nimeshampa pongezi zake kwenye Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...

Pasco.
 
Nimebahatika kufika nyumbani anakoishi Mtikila apartment za Nationa Housing jijini Dar, nisingependa kutaja mahali.
Nilichojifunza kutoka kwake ni kweli mtu aliye wa kawaida lakini tajiri rohoni, na alicho nacho anakitumai kujenga na kutetea uhuru wa watanzania, demokrasia ya watanzania tofauti na wanasiasa wengi na wachungaji wengi ambao wanatanguliza kwanza kujenga mahekalu yao.

Amini, usiamini nilipata kuelewa vema sana ukweli na undani wa Mtikila kwani safari yangu ilianzia kutembelea ofisi za Chama chake si mbali kutoka barabara ya Uhuru karibu na sehemu iliyojaza machinga wengi tu. Lengo lilikuwa kumfahamu huyu Mtikila, na wakwanza kuwaona ni wanaofanya kazi katika ofisi yake ni watu wa kawaida tu, ametanguliza kuwaajiri walala hoi.

Kama ungeweza kupata picha ya maisha ya Mtikila, mazingira ya umaskini lakini akiwa tajiri rohoni, ni nadra mno wengi wetu hapa kufanya anayofanya, na hapa ndipo tunapoweza kuamini nguvu ya Mungu ainavyotumika indirect kupitia sisi binadamu.
Kwani sii wote waliiishi hivyo kabla hawajaingia IKULU?..Mkuu usipumbazwe na hawa watu wanaotafuta Ukubwa wanaajua wanacheza siasa gani na kwa ajili gani. Unapomweka Ofisini mlalahoi kwa kodi ya wananchi hapo unataka kunambia ni akili hiyo? ama ametaka wewe na wengine mtazame hivyo wakati kazi zake hazifanyiki sawasawa isipokuwa kwa amri yake. Unapoweka Mlalahoi ofisini ina maana unataka kuamrisha watu wafanye utakavyo maana ukiweka mwenye elimu itakuwa ushindani kwako.

Asikudanganye huyu mtu kwa kuwa anaishi nyumba ya National Housing, tena inaonyesha wazi jinsi alivyokuwa mchovu mtu anapokea mabillioni (mshahara) ya kodi zetu kashindwa hata kujenga nyumba yake mwenyewe ataweza vipi kuijenga nchi. Na sidhani kama anaweza kuonyesha mshahara wake huenda wapi. Kiongozi huanza na wewe mwenyewe maana hatutafuti mchungaji bali tunatafuta kiongozi wa nchi ambaye atatuletea maendeleo sio wokovu wa kiroho.
 
Manake ni hivi: leo hii Mnyika anaweza kusimama na kusema aliyoyasema Mtikila na asifungwe. Alichofanya Mtikila kwangu (ni kweli kesi zinamsaidia binafsi) ni kutengeneza "precedence". Kuna kesi nyingi sana za kikatiba zinazohusiana na haya masuala ya kisiasa ambazo mahakama zinatumia hukumu ya kesi za mtikila kama reference. Kesi ile ya uhaini ya Zanzibar ni mfano mmojawapo tu.
 
Kwa kweli inaleta faraja kupita kiasi kufahamu kwamba kumbe tupo watanzania wengi wenye mtazamo wa namna hii; Shukrani Candid scope, ipo siku kitaeleweka tu;

Ungeanza kujiita Mtangayika, kabla ya kujiita Mtanzania. Maana Mtanzania ni mtu ambae anatambua muungano wa ZNZ na Tanzania bara. Na huu haupo kwa sababu ya tofauti ya ideologies ambazo zinasambazwa na watu kama akina Mtikila,Jussa, wala Sharif Hamad, hila muungano huu hupo kwa sababu ni watu wa aina moja na ndio kitu Nyerere alichokiona.

Mtikila hawezi kuwa shujaa wa demokrasia miaka mia moja, hata Hitler alikuwa akisimamia maslahi ya wajerumani na demokrasia ya ujerumani lakini aliiona only in the eyes of those with european background, that is not democracy.

Tip angalia cinema inaitwa 'heroes' jamaa walikuwa wamejipanga kumuua mfalme kwa madai ya kwamba anaingilia maslahi ya ardhi yao na kutaka kuwatawala, mwisho wa siku Jet-Li anajikuta yupo sehemu ambayo anaweza kumuua 'Mfalme' wasiompenda lakini akagwaya. Kwa sababu akaja elewa kwamba ingawa haoni moja kwa moja na mfalme. Hila mfalme anachopigania ni unification of people of the same background na ndio sababu za Nyerere kuutaka muungano.

Kwenye Cinema Jet-Li alijua kwamba akimuua mfalme ama asipo muua lazima afe kutokana na sehemu aliyokuwepo, hila chaguo lake lilitokana na the long term of China vision ambayo Mfalme aliyoiona. Halafu unajiita mfuasi wa Mfalme (nyerere) wakati umuelewi.
 
Nashindwa kuelewa watu ambao wanapinga ukweli, mateso na jitihada zote aliyezifanya Rev Mtikila juu ya nchi hii. Na si kweli kuwa mengi aliyafanya kwa merits zake binafsi. Alipoanza siasa 1988 alianza na haki za binadamu.kuanzia wafungwa wa kisiasa (waliofungwa kwa uhaini kwa nia kumpindua mwl Nyerere), freedom of speech, haki ya mikusanyiko, vibali vya mikutano toka kwa mkuu wa wilaya, passport kwenda Zenj, mgombea binafsi etc. leo hii ni nani anayenufaika kama sio watanzania? Waulizeni mnaowaona kuwa ni wana siasa leo hii ni nani aliwakusanya, kuwaunganisha na kuanziasha original NCCR. Mtikila is very far ahead from our normal, average politicians from thinking, analysis, presentation and performance.
 
Ungeanza kujiita Mtangayika, kabla ya kujiita Mtanzania. Maana Mtanzania ni mtu ambae anatambua muungano wa ZNZ na Tanzania bara. Na huu haupo kwa sababu ya tofauti ya ideologies ambazo zinasambazwa na watu kama akina Mtikila,Jussa, wala Sharif Hamad, hila muungano huu hupo kwa sababu ni watu wa aina moja na ndio kitu Nyerere alichokiona.

Mtikila hawezi kuwa shujaa wa demokrasia miaka mia moja, hata Hitler alikuwa akisimamia maslahi ya wajerumani na demokrasia ya ujerumani lakini aliiona only in the eyes of those with european background, that is not democracy.

Tip angalia cinema inaitwa 'heroes' jamaa walikuwa wamejipanga kumuua mfalme kwa madai ya kwamba anaingilia maslahi ya ardhi yao na kutaka kuwatawala, mwisho wa siku Jet-Li anajikuta yupo sehemu ambayo anaweza kumuua 'Mfalme' wasiompenda lakini akagwaya kwa sababu akaja elewa kwamba ingawa haoni moja kwa moja na mfalme. Hila mfalme anachopigania ni unification of people the same na ndio sababu za Nyerere. Halafu unajiita mfuasi wa Mfalme (nyerere) wakati umuelewi.

Ndio maana neno mtanzania nimeliweka tofauti na mengine kimtazamo, au ulidhania nilikuwa nachezea tu key board? Kuhusu mimi kutomuelewa Nyerere, pengine upo sahihi, vinginevyo moja ya majukumu niliyojipa kwa muda wa zaidi ya miaka saba sasa ni kutafiti na kusoma juu ya philosophy ya Nyerere ili kuzidi kumuelewa;

Vinginevyo nayosema hapa ni mtazamo wangu tu, ndio maana wadau kama nguruvi3 huja na threads zenye title zilizojaa fikra na busara sana kama vile 'Duru Za Siasa: Mgongano wa Mawazo";

Ni matarajio yangu kwamba tutaendelea kugongana kimawazo!!
 
Tupo wengi sana tunaomuunga Mkono Mtikila juu ya Tanganyika, na Tundu Lissu kwa sasa ni muhimu sana katika harakati zetu hizi; Binafsi sina matatizo na muungano bali mfumo wake ambao ni mbovu na unatugharimu sisi kuliko wenzetu kwani hakuna kilichokuwa na gharama kubwa kama kupoteza utaifa...mimi ni mmoja ya "watanzania" wanaomuunga Mkono Mtikila, Lissu na wanaharakati wengine wote waliopo kwenye mstari wa mbele kutufufulia Tanganyika yetu;

Mchambuzi
Unasoma makala za Mzee Mwanakijiji hukusu Muungano?
Unasoma michango ya Nguruvi3 na JokaKuu kuhusu Muungano?

Hawa watu wanawafundisha wazanzibari kujitoa kwenye Muungano lakini hawashajihishi au kutoa elimu kwa wadanganyika kudai Tanganyika.

Katika JF hawa ni watu wa fikrapevu lakini linapokuja suala la kudai Tanganyika na serikali ya Tanganyika huwa wanakuwa kama kuku aliyemwagiwa maji. Huwa napata mashaka wakati mwengine kama Chai Chapati Maharage wamewaweka mfukoni au ni kuhofia utaifa wa Tanganyika dhidi ya utanzania?
Mbona utaifa mbili unawezekana? (dual nationality), mfano british lakini pia ni english, scotish au welsh.

Bado hata Lissu ameishia kauli ya kusema upo umuhimu wa kuirudisha Tanganyika, vitendo bado (awasilishe mswada bungeni unaodai kuirudisha serikali ya Nchi ya Tanganyika ili kumaliza hiki kiini macho.
Liko wapi kundi jipya la G55 au G110?

Hiki ni kipindi cha kutoa maoni kuhusu katiba mpya, hakuna anaetoa elimu kwa wananchi kudai serikali ya Tanganyika bali wapo akina MMjj na Nguruvi3 wanaotushajihisha tudai serikali moja.

Siasa za Tz zinaweza kumtia mtu maradhi ya moyo.

Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji karibuni katika hili kundi la kudai serikali ya Tanganyika na saa ya ukombozi ni sasa!
 
Nashindwa kuelewa watu ambao wanapinga ukweli, mateso na jitihada zote aliyezifanya Rev Mtikila juu ya nchi hii. Na si kweli kuwa mengi aliyafanya kwa merits zake binafsi. Alipoanza siasa 1988 alianza na haki za binadamu.kuanzia wafungwa wa kisiasa (waliofungwa kwa uhaini kwa nia kumpindua mwl Nyerere), freedom of speech, haki ya mikusanyiko, vibali vya mikutano toka kwa mkuu wa wilaya, passport kwenda Zenj, mgombea binafsi etc. leo hii ni nani anayenufaika kama sio watanzania? Waulizeni mnaowaona kuwa ni wana siasa leo hii ni nani aliwakusanya, kuwaunganisha na kuanziasha original NCCR. Mtikila is very far ahead from our normal, average politicians from thinking, analysis, presentation and performance.
Kwako wewe pengine maana mwaka 1988 sijui unazungumzia wagungwa gani alowatetea au kwenda mahakamani..Freedom of Speach ktk kesi gani, Haki ya makusanyiko ktk kasi gani..Pengine wewe unachannganya maana ni huyu huyu Mtikila aliyewahi kutukana wahindi na kuwaita magaba choli, akautukana hata Uislaam kwa sababu ya Zanzibar badala ya kujaribu kutuunganisha. Akiahidi kuwajaza watu UTAJIRI kila mtu mweusi atakuwa millionea. Pengine mnazungumzia Mtikila mwingine siye huyu alosababishwa wahindi na waarabu kujifungia majumbani wakiogopa kuawa.
 
Mchambuzi
Unasoma makala za Mzee Mwanakijiji hukusu Muungano?
Unasoma michango ya Nguruvi3 na JokaKuu kuhusu Muungano?

Hawa watu wanawafundisha wazanzibari kujitoa kwenye Muungano lakini hawashajihishi au kutoa elimu kwa wadanganyika kudai Tanganyika.

Katika JF hawa ni watu wa fikrapevu lakini linapokuja suala la kudai Tanganyika na serikali ya Tanganyika huwa wanakuwa kama kuku aliyemwagiwa maji. Huwa napata mashaka wakati mwengine kama Chai Chapati Maharage wamewaweka mfukoni au ni kuhofia utaifa wa Tanganyika dhidi ya utanzania?
Mbona utaifa mbili unawezekana? (dual nationality), mfano british lakini pia ni english, scotish au welsh.

Bado hata Lissu ameishia kauli ya kusema upo umuhimu wa kuirudisha Tanganyika, vitendo bado (awasilishe mswada bungeni unaodai kuirudisha serikali ya Nchi ya Tanganyika ili kumaliza hiki kiini macho.
Liko wapi kundi jipya la G55 au G110?

Hiki ni kipindi cha kutoa maoni kuhusu katiba mpya, hakuna anaetoa elimu kwa wananchi kudai serikali ya Tanganyika bali wapo akina MMjj na Nguruvi3 wanaotushajihisha tudai serikali moja.

Siasa za Tz zinaweza kumtia mtu maradhi ya moyo.

Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji karibuni katika hili kundi la kudai serikali ya Tanganyika na saa ya ukombozi ni sasa!

Huwa nina soma sana makala za wenzetu hawa, lakini huwa nina reserve my comments kwa sababu nimekuwa ninaandaa makala pole pole juu ya hoja za msingi kabisa za Lissu na Mtikila ambazo mimi nimekuwa mfuasi wa hoja zao kwa muda mrefu sana; Nikipata nafasi nitaiweka makala yangu mungu akitujalia uzima, nadhani by end of this month; Vinginevyo naunga mkono hoja kwamba "Saa ya Ukombozi ni Sasa";
 
Kesi zinazomkabili na namna anavyoshinda zinanifanya nitie mashaka.
Inawezekana ni mipango ya pamoja kutuonesha mapichapicha na kuuhadaa ulimwengu kuhusu mifumo ya demokrasia na haki ndani ya hii jamhuri.
Nahitaji muda wa kutosha kutafakari.
 
Nimebahatika kufika nyumbani anakoishi Mtikila apartment za Nationa Housing jijini Dar, nisingependa kutaja mahali.
Nilichojifunza kutoka kwake ni kweli mtu aliye wa kawaida lakini tajiri rohoni, na alicho nacho anakitumai kujenga na kutetea uhuru wa watanzania, demokrasia ya watanzania tofauti na wanasiasa wengi na wachungaji wengi ambao wanatanguliza kwanza kujenga mahekalu yao.

Amini, usiamini nilipata kuelewa vema sana ukweli na undani wa Mtikila kwani safari yangu ilianzia kutembelea ofisi za Chama chake si mbali kutoka barabara ya Uhuru karibu na sehemu iliyojaza machinga wengi tu. Lengo lilikuwa kumfahamu huyu Mtikila, na wakwanza kuwaona ni wanaofanya kazi katika ofisi yake ni watu wa kawaida tu, ametanguliza kuwaajiri walala hoi.

Kama ungeweza kupata picha ya maisha ya Mtikila, mazingira ya umaskini lakini akiwa tajiri rohoni, ni nadra mno wengi wetu hapa kufanya anayofanya, na hapa ndipo tunapoweza kuamini nguvu ya Mungu ainavyotumika indirect kupitia sisi binadamu.
He is humble and down to earth!, mara ya mwisho nakutana nae, kama kawaida yake, suti safi, briefcase kubwa na usafiri wake ni bajaj, besides uchungaji wake, hivyo kuishi kwa kutegemea Sadaka, he makes his living kwa kutegemea kesi!. Ile kesi ya mgombea binafsi, someone was funding him heavily ili akishinda, huyo someone ndio agombee kama mgombea binafsi!, unfortunately it didn't work out well, wameishia kugombana!. Akimaliza kesi moja, anafile nyingine na anaendelea kuvuta fungu, huku life goes on!.
P.
 
Ndio maana neno mtanzania nimeliweka tofauti na mengine kimtazamo, au ulidhania nilikuwa nachezea tu key board? Kuhusu mimi kutomuelewa Nyerere, pengine upo sahihi, vinginevyo moja ya majukumu niliyojipa kwa muda wa zaidi ya miaka saba sasa ni kutafiti na kusoma juu ya philosophy ya Nyerere ili kuzidi kumuelewa;

Vinginevyo nayosema hapa ni mtazamo wangu tu, ndio maana wadau kama nguruvi3 huja na threads zenye title zilizojaa fikra na busara sana kama vile 'Duru Za Siasa: Mgongano wa Mawazo";

Ni matarajio yangu kwamba tutaendelea kugongana kimawazo!!
Siasa is all pervasive, but democracy and understanding where you belong is not subjected to our ideologies but rather of knowing thyself. Nyerere knew that what about you?
 
Pasco usifananishe machungwa na mapera.Mtikila usimfananshe na vyama vingine,unless ungemention DP vs chadema and so forth.Apples to appels please.
 
Last edited by a moderator:
Manake ni hivi: leo hii Mnyika anaweza kusimama na kusema aliyoyasema Mtikila na asifungwe. Alichofanya Mtikila kwangu (ni kweli kesi zinamsaidia binafsi) ni kutengeneza "precedence". Kuna kesi nyingi sana za kikatiba zinazohusiana na haya masuala ya kisiasa ambazo mahakama zinatumia hukumu ya kesi za mtikila kama reference. Kesi ile ya uhaini ya Zanzibar ni mfano mmojawapo tu.

Mzee Mwanakijiji, umeliona hilo hata wewe. Hilo ndilo lililonisukuma matukio ya karibuni tafrani katika mikutano ya vyama vya siasa kuvamiwa na polisi na kutokea mauaji, ndipo binafsi nilipoandika barua kwa Mnyika kumshauri sasa chadema watumie mamlaka za mahakama kudai haki zao, kuishtaki serikali kwa mauaji ya raia, kudai uchunguzi wa mahakama kisheria na kikatiba kuliko kubaki kulalamika mikutanoni na kuishia kuendelea kupambana na dola kwa vile hawajatanguliza kinga yao kisheria inayochezewa na serikali katika kuendesha vuguvugu la mageuzi nchini.

Suala la kutumia nguvu za kisheria mahakamani waziri mkuu Mizengo Pinda alishatoa ushauri mara kadhaa kuanzia purukushani za kule Arusha mara baada ya uchaguzi, lakini alitafsiriwa kama anawahadaa bila kujua kama baniani mbaya kiatu chake dawa, kama ushauri wake ungetiliwa maanani matatizo mengi ya mikutano ya hadhara na vibali mahakama ingetoa tafsiri zingefanyika kama Chungaji Mtikila afanyavyo, huenda kungekuwa na mabadiliko makubwa yenye kulinda haki na usalama wao mikutanoni kuliko kuendelea klalamika mikutanoni wakati makahama ziko wazi kutetea haki zao kikatiba.

Watanzania, vyama vya siasa na kila mwananchi
tunatakiwa kuzitumia haki zetu kikatiba
ambazo hulindwa na Mhimili wa Mahakama.
 
Mkuu Mkandara, asante kwa kuongelea ubinafsi!. Ni kweli Mtikila ni Mbinafsi, So does Chadema, CUF and NCCR-Magauzi!. CUF had to join CCM in GNU not because it wished, but because it had to under the principle of "If you can't beat them...
Mtikila ni Mbinafsi na ataendelea kuwa hivyo kwa sababu hapo alipofikia ni "All the he wants!" and doesn't expect anything more!, nimeshampa pongezi zake kwenye Kitendo Cha Rev. Mtikila Kugomea Arrest!, Kinastahili Pongezi ...

Pasco.

Pasco

Mbinafsi mkuu TZ ni chama cha Lowassa.

Hili la "to join CCM" unafunika kombe tu. Sio siri kuwa CCM wameshinda chaguzi kwa kishindo na sio kwa kura.
Kama kuna la kukemea basi tukemee ubinafsi wa chama kinachoshinda kwa kishindo na ung'ang'anizi wa mamlaka ya jamhuri yetu wakisaidiwa na vyombo vya dola.

Kama wataendelea na ushindi wa kishindo,watatuletea balaa katika nchi yetu.

Haya "maisha bora" tuliyonayo yanatutosha, wasisababishe na amani ipotee. Litakapoanza, mziki wake ni kama wa Congo, Libya, Ivory Coast. Hatutatambuana tena.
 
Nashindwa kuelewa watu ambao wanapinga ukweli, mateso na jitihada zote aliyezifanya Rev Mtikila juu ya nchi hii. Na si kweli kuwa mengi aliyafanya kwa merits zake binafsi. Alipoanza siasa 1988 alianza na haki za binadamu.kuanzia wafungwa wa kisiasa (waliofungwa kwa uhaini kwa nia kumpindua mwl Nyerere), freedom of speech, haki ya mikusanyiko, vibali vya mikutano toka kwa mkuu wa wilaya, passport kwenda Zenj, mgombea binafsi etc. leo hii ni nani anayenufaika kama sio watanzania? Waulizeni mnaowaona kuwa ni wana siasa leo hii ni nani aliwakusanya, kuwaunganisha na kuanziasha original NCCR. Mtikila is very far ahead from our normal, average politicians from thinking, analysis, presentation and performance.
Mtikila uzuri wake ni straight forward "politician".Kwamfano hii kesi ya kumwita JK gaidi ameshinda.Huwa hatafuti sympathy za kila mtu.Ana misimamo yake na anaisimamia.Ni mtanganyika halisi.Ni mpigania haki na mpenda mabadiliko,tatizo lake si "mwanasiasa" wa kitanzania.Na hapo ndo maana anapata shida kwenye siasa za Tanzania.
 
He is humble and down to earth!, mara ya mwisho nakutana nae, kama kawaida yake, suti safi, briefcase kubwa na usafiri wake ni bajaj, besides uchungaji wake, hivyo kuishi kwa kutegemea Sadaka, he makes his living kwa kutegemea kesi!. Ile kesi ya mgombea binafsi, someone was funding him heavily ili akishinda, huyo someone ndio agombee kama mgombea binafsi!, unfortunately it didn't work out well, wameishia kugombana!. Akimaliza kesi moja, anafile nyingine na anaendelea kuvuta fungu, huku life goes on!.
P.

Kwanza tuassume kuwa ni kweli unachosema. Siyo kitu cha ajabu na cha kushangaza. Hapa Marekani kwenye civil rights movement kuna kitu wanakifanya ambacho ni kuchukua watu ili wafungue kesi fulani mahakamani zinazohusiana na haki. Hawa wanaweza kuwa compensated na kugharimiwa na taasisi hizo (say ACLU). Lengo ni kile wanachokisema ni "trial cases" ambapo wanataka kuchallenge legality ya issue fulani.

Kama ni kweli anatumiwa na anakubali kwenda mahakamani au kushtakiwa chini ya tishio la kifungo na adhabu. Kwa kweli anastahili kuwa compensated handsomely.
 
Mtikila uzuri wake ni straight forward "politician".Kwamfano hii kesi ya kumwita JK gaidi ameshinda.Huwa hatafuti sympathy za kila mtu.Ana misimamo yake na anaisimamia.Ni mtanganyika halisi.Ni mpigania haki na mpenda mabadiliko,tatizo lake si "mwanasiasa" wa kitanzania.Na hapo ndo mana napata shida kwenye siasa za Tanzania.

Mushi 1 umenena, maana wengi waliona hapa kumwita Kikwete ni gaidi kihunzi kilikuwa kigumu kukiruka, lakini amini usiamini amechopoka, anajiamini na hana wasiwasi na anachokisema.
 
Back
Top Bottom