Mtikila kutinga kortini posho za wabunge

Wazo zuri sana ila mahakama haitatoa haki maana serikali imejikita humo......
 
Hapo ndipo anaponikosha Mtikila, alijifuza kuwa kuingia mitaani hakuna tija unaishia kula mkong'oto na kulala rumande.

Hivyo ndivo inavyotakiwa, hata ukidhulumiwa record zitakuwepo na vizazi na vizazi watazikuta na kujifunza.
 
mtikila kutinga kortini posho za wabunge send to a friend
thursday, 02 february 2012 21:32
0digg
hussein issa,
kitendo cha wabunge kujiongezea posho kutoka sh70,000 hadi sh200,000 bila idhini ya rais, kimemkera mwenyekiti wa chama cha democratic (dp), mchungaji christopher mtikila ambaye sasa amesema anajiandaa kwenda mahakamani kufungua kesi ya kughushi dhidi ya viongozi wa taasisi hiyo ya kutunga sheria.

Mtikila aliliambia gazeti hili jana kuwa kama kweli rais kikwete hajasaini posho hizo, basi bunge limeghushi na kuliibia taifa na kitendo hicho hakiwezi kuvumilika.

Alisema tayari ameanza maandalizi ya kesi hiyo kwa kuwatafuta wanasheria wa ndani na nje ya nchi watakaosimamia mahakamani hadi haki itakapotendeka.

Alisema mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo ni spika wa bunge anne makinda, wa pili ni naibu wake job ndugai na baadaye wabunge wote wanaosaini nyongeza hiyo ya posho isiyokuwa na baraka za rais.

"huku ni kughushi na kuhujumu uchumi wa nchi, bunge kujiongezea posho bila idhini ya rais! Ni wizi wa kawaida kabisa ambao ni kosa la jinai. Niko mbioni kukamilisha taratibu na hakika ninaenda mahakamani," alisena mtikila.
Kwa mujibu wa mtikila, mbali na bunge kesi hiyo pia itamhusisha mwanasheria mkuu wa serikali.

"yeye atahusika kwa sababu ameliona hilo na ameendelea kukaa kimya. Huu ni uzembe na sheria zinasema kutenda au kutotenda kunakoleta madhara ni kosa."

mtikila alisema anasikitika kuona viongozi waliopewa fursa ya kuwatumikia wananchi, wanatumia fursa hiyo kuwajumu na hii haivumiliki.

“nitaenda mahakamani kwa sababu hili suala sio la mchezo kabisa linaumiza wananchi,” alisema.
Hata hivyo mtikila hakusema lini atafungua kesi hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa bado anaendelea na maandalizi ya kutafuta wanasheria.

Mtikila alieleza kuwa matatizo yanayolikabili taifa kama hili la wabunge kujiongezea posho kinyemela, linatokana na matatizo ya katiba ambayo watanzania wanapaswa kujipanga kuyaondoa katika mchakato huu wa katiba mpy
hili jamaa sometimez lina akili....hii ilitakiwa kufanya na chama "kikuu cha upinzani" lakini bahati mbaya nacho kimelewa ulevi wa posho kwa kuwa kuna watu wa zito wa chama hicho wananufaika na kilevi hicho,sasa wako tila lila mpaka miwani inadondoka hawaoni tena au wanaona kwa makengeza!
 
Bora Mtikila aende atusaide kutusemea-maana kwa nchi hii ni yeye tu mwenye guts za kwenda mahakamani na kushtaki serikali

Tunawaomba wabunge wote waliokuwa wanazipinga hizo posho wamsaidie mtikila kwa kumpatia data zote nasi watanzania tuwe pamoja kumwunga mkono mchungaji wa Mali za watanzania aliyejitokeza kufungua mashitaka kwa wale wote waliohusika kuizinisha hizo posho kinyemela.hongera sana mtikira.
 
Tatizo letu watanzania wengi hawajauelewa mchango wa Rev. Mtikila katika kuleta demokrasia Tanzania.

Ni Mtu anayefungua kesi sio kwa mnufaa yake Bali kwa manufaa ya watanzania wote. Mtu yoyote anayebeza juhudi zake katika Nyanja ya sheria basi atakuwa na upungufu wa busara kichwani.

Akifungua kesi asisahahu kufungua na kesi nyingine kuishtaki serikali kwa kupuuzia Madai ya madaktari kitendo kilichosababisha mamia ya watanzania kufa katokana na kukosa huduma za afya. Haki ya kuishi inayoelezwa kwenye Katiba ni pamoja na haki ya kupata matibabu ya kutosha ya bure.
 
Back
Top Bottom