Mtikila kula valentine uswahilini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
HATIMAYE Mchungaji Christopher Mtikila liyekuwa rumande kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya uchochezi na kutoa lugha ya matusi kwa Rais Jakaya Kikwete, amepata dhamana.

Kesi hiyo ambayo ilikuja leo kwa ajili ya mshtakiwa kudhaminiwa baada ya Hakimu Warialwande Lema kumfutia dhamana kutokana na kutofika mahakamani.

Katika kesi hiyo mshtakiwa anadaiwa kuwa mwaka 2007 alifanya uchochezi na kutoa lugha ya matusi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wiki mbili nyuma kesi hiyo ilikuwa ije kwa ajili ya kusomwa maelezo ya awali lakini mshtakiwa hakuwapo mahakamani pamoja na wakili wake.

Hata hivyo mshtakiwa huyo aliiomba mahakama imfungulie dhamana ambapo Januari 25, mwkaa huu, dhamana ya mshtakiwa ilifunguliwa lakini mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa ya kuwa na wadhamini wawili.

Katika masharti hayo wadhamini kila mmoja ametakiwa kumdhamini kwa sh milioni moja ambapo wakili wa mshtakiwa ni Mapare Mpoki.

Kesi hiyo itakuja Februari 8, mwaka huu, kwa kutajwa na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kwa masharti ya kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila ruhusa ya barua ya mahakama na kutokosa kufika mahakamani katika tarehe aliyopangiwa.

Pia mshtakiwa akikosa kufika mahakamanini atafungiwa dhamana na kutopata dhamana tena
 
hii iwe fundisho na kwa wengine;anatukana wakunga wakati ajavuka mto
kidumu chama
 
Back
Top Bottom