Mtikila anamshtaki JK, tumchangie pesa

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Nimesoma kwenye Mwananchi Paper kuwa Mtikila atamshitaki Hussein Mwinyi, Shimbo, Mwamunyange kama hawatajiuzulu, pia JK atashtakiwa kama hatawafukuza kazi.

Pia zinatakiwa Million 50 kwa sababu ni kesi nzito. Ameomba michango, jamani tuchangie hata buku 10 kila mtu aliyeguswa.

Pia Mtikila amesema tutumie nguvu ya umma kama Misri, tunisia.

Naomba mtu mwenye mawasiliano na Mtikila amshauri atupe namba ya akaunti, ZAP au Tigo pesa tuchangie kwa ajili ya kesi
 
Nadhani kesi sio suluhisho la matatizo ya Tanzania kwa sababu watatumia mwanya huo kuichelewesha kesi hadi mambo yaende mbali.
Mbona suluhu ya mambo haya iko wazi? Nakumbuka ile miaka ya 1994/5, alipoibuka mzee wa magabachori (kumradhi, sina nia ya kubagua) ambapo vijana wa Dar walihamasika kweli. Kwa nini leo haiwezekani kwa wezi na wazembe wanaoiingizia Tanzania katika mizigo isiyoihusu?
 
Asanteni wadau kwa michango yenu.

Ni kweli Taifa la Tanzania halijasimama imara kwa maana kwamba Mahakama haiko huru na Bunge pia limechakachuliwa.

Maovu ni mengi na watawala wanatumia upole/woga/ujinga wa watanzania kuendelea kukandamiza demokrasia.

Sasa jawabu ni maandamano tu, ila nani wa kuanzisha??

Iundwe kamati ya wanaharakati ambayo itafanya kutokea kusikojulikana (incognito) ili kuwa salama. Mfano facebook itumike, simu.

Siku ya kwanza: Watu wakianza kwenda kwenye Viwanja kama Jangwani, Mwanza kule, Mbeya, Iringa, Arusha. Siku ya pili:Then watu wengine kama wafanyakazi wa mashirika na serikali wataunga mkono; Siku ya tatu, watu wa vijijini nao watajiunga.

Tukisubiri viongozi au vyama vya upinzani waanze, haitawezekana maana watakamatwa au majina yao yatachafuliwa.

Haya twende, tuanze. Tuanze na page ya facebook, tutengeneze rington ya ukombozi ambayo itahamasisha.

Mpango mzima ni ukombozi, mwageni mpango mkakati hapa
 
Sasa jawabu ni maandamano tu, ila nani wa kuanzisha??

Hizi ni fikra mgando, haiwezekani jawabu likawa ni moja tu, fanya homework yako utajua kuna zaidi ya njia 1000 na hata kwa watu wanaoitumia njia hii huwa wanaitumia kama last resort.
 
Hizi ni fikra mgando, haiwezekani jawabu likawa ni moja tu, fanya homework yako utajua kuna zaidi ya njia 1000 na hata kwa watu wanaoitumia njia hii huwa wanaitumia kama last resort.

Majalala yamepungua huyu nae ni kero!
 
Jamani watanzania tutazidi kulalamika, hamna matendo yoyote jamani

inashangaza sana...kila kukicha sisi ni kulalama tuuu,mara ooh gharama kubwa za umeme,mara kupanda kwa gharama za maisha mara mgao wa umeme,mara mwinyi na mwamunyange wajiuzulu,sijui dowans kufanyeje...lakini mmh!Tumekuwa wazuri mno wa kulalama na kuweka mikakati ya kukabiliana na hayo kwa midomo tu,hakuna matendo!Nadhani bado hatujawa tayari kutumia nguvu yetu kupambana na majangili hawa.Tuache bla blah,tuache woga,tuyafanya haya tuyaandikayo hapa jf kwa vitendo wandugu!
 
Mtikila mnamjua lakini hicho kichwa kwa pesa mnamchangia hizo pesa, hapo hapo anakwenda Caspian ofisini kwa Rostam Aziz kuchukuwa pesa zingine kuna kesi hapo!
 
Nimesikia wanajeshi 9 ambao ni viongozi wa juu jeshini, wa kongo wamehukumia miaka 10 mpaka 20 na kuondolewa jeshini kwa kosa la kubaka, kwa nini hawa waliosababisha vifo vya rai kwa uzembe wasifungwe na kuondolewa jeshini. Licha ya kuwa tulisikia wakisema jeshini hakuna kujiuzulu basi wafunguliwe mashtaka kwenye mahakama ya jeshi hawatufai
 
Back
Top Bottom