Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,082
Monday, 14 June 2010 20:54 0diggsdigg
Tausi Ally na James Magai
KWA mara nyingine tena Mwenyekiti wa Chama Cha Demokratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila anayekabiliwa na kesi ya uchochezi amemkataa hakimu mwingine tena wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Mtikila amechukua uamuzi huo wa kumuomba hakimu huyo Genivitus Dudu kujitoa katika kesi yake hiyo siku chake tu baada ya kesi kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa mashtaka ambao pia ulitolewa kwa njia ya luninga mbele ya hakimu huyo anayemtaka ajitoe Genivitus Dudu.
Dudu ni hakimu wa pili kukataliwa na Mchungaji Mtikila katika kesi hiyo ambayo Mtikila anadaiwa kumwita Rais Kikwete kuwa ni gaidi, huku hakimu mwingine wa tatu, Salome Mwandu akiwa amejitoa mwenyewe.
Katika barua yake aliyomwandikia hakimu Dudu kumtaka ajitoe katika kesi yake hiyo, Mchungaji Mtikila alidai kuwa hana imani na hakimu huyo kwa kuwa hatamtendea haki, huku akimtuhumu kufanya kazi kwa maslahi ya upande wa mashtaka.
Mchungaji Mtikila alitoa mfano wa tuhuma zake kwa hakimu Dudu kuwa alikuwa akijadiliana na upande wa mashtaka kuhusu kesi hiyo bila kuhusisha upande wa utetezi jambo ambalo alisema ni upuuzaji mkubwa wa kanuni ya kisheria ya haki na usawa.
Hoja nyingine aliyoitoa Mtikila katika barua yake hiyo ya kutokuwa na imani na hakimu huyo alidai kuwa amekuwa akikataa maombi yake hasa pale wakili wake, Mpale Mpoki alipoomba kesi hiyo iahirishwe angalau kwa muda wa wiki moja ili waweze kujadiliana na kujiandaa kwa ajili utetezi.
Kosa linadaiwa kutendeka mwaka 2007, hivyo si rahisi kwa mtu yeyote kukumbuka kila kitu kichwani, lakini ulikataa vikali kukubalkiana na ombi hilokwa maslahi ya haki anasisitiza Mtikila katika barua yake hiyo na kuongeza
Wakili wangu alipinga kupokewa kwa mkanda wa video kwa kuwa alikuwa hajaona kilichomo ndani kama ilivyo mantiki kwamba mtu anaweza akakubali au akakataa kitu baada tu ya kujua kilichomo, lakini ulikataa kuuchezesha mkanda huo ili kumpa nafasi ya kukubali au kukataa mkanda huo usipokewe.
Pia Mtikila anamlalamikia hakimu huyo kwa kutupilia mbali pingamizi aliloliweka kupitia kwa wakili wake juu ya kupokelewa kwa maelezo yake anayodaiwa kuyatoa polisi (caution statement) na mkanda wa video ambavyo viliwasilishwa mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi katika kesi hiyo , lakini pia jakimu huyo alikataa .
Kabla ya kumkataa hakimu Dudu jana, Mtikila pia alishawahi kumkataa Hakimu Waliarwande Lema kwa madai kuwa hana imani naye akidai kuwa hataweza kumtendea haki kwa sababu ameonyesha kuwa na kisirani na ukatili dhidi yake., ndipo kesi hiyo ikapangwa Hakimu Salome Mwandu.
Hata hivyo Hakimu Salome naye alitangaza kujitoa katika kesi hiyo siku hiyo hiyo kwa maelezo kuwa awali alikuwa na kesi nyingine ya Mtikila hivyo kama angeendelea kuisikiliza kesi hii kulikuwa na uwezekano wa haki ikaonekana haijatendeka.
Katika kesi hiyo Mtikila anadaiwa kuwa Oktoba 21, mwaka jana maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ilala, jijini Dar es Salaam Mtikila alitoa maneno ya uchochezi yenye dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.
Inadaiwa kuwa alitoa maneno hayo ya uchochezi kuwa Papa alikuwa na mgeni ambaye ni gaidi, ninaomba niseme haya kwasababu ninasema mimi, Rais Kikwete ni gaidi.
"He is a terrorist ".
Ilidaiwa kuwa siku hiyo, Mtikila alitoa maneno mengine ya uchochezi ambayo yalikuwa na chuki na dharau ambayo yangeweza kusababisha watu kukosa imani na serikali yao.
Aidha, Mhungaji Mtikila pia anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwamba: uteuzi wa "Jakaya Kikwete siku zote unaongozwa na imani yake ya dini kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi....''
Mtikila akataa hakimu tena