Mtikila akamatwa na polisi kwa kumkashifu Rais

Mtikila anajipinga mwenyewe hasa anaposema maneno haya:-
Sikuingia katika siasa kwa njaa bali ni kuliubiri neno la mungu,” alisema Mtikila.

Hapa inaonyesha wazi kuwa lengo lake ni kuleta imani fulani ya kidini ktk siasa, kiasi kwamba nashindwa kuelewa anachopinga kuhusu mahakama ya kadhi na mahubiri anayotaka kuyaleta ktk siasa.

Maneno aliyoyasema ni mazito sana na kusema kweli yameniacha hoi, nashindwa kuamini kama maneno haya yamezungumzwa na Mtikila... its way out kwani Allah ni Mungu na unaposema Allah ni shetani sijui unachofundisha ni kitu gani. ndio matatizo ya Mkoloni haya kuwa Mungu ni GOD... period neno la mzungu nje ya hapo sio Mungu ila ni shetani.

Pili, sidhani kama ni busara viongozi wa dini kuingilia swala hili kwa sababu kutaleta matatizo zaidi ya kila hoja inayoweza kuwa solved kisiasa. Mathlan tukitumia imani za dini hata HIV itakuwa taabu sana kuipatia dawa.

Yawezekana kabisa kuwa waislaam wana makosa lakini sio swala la mhubiri wa dini nyingine kujiingiza katika sakata hili na kulifanya kuwa ni mashambulizi ya kidini. Nimeshauliza mara nyingi mbona waislaam hawaja unda kamati kupinga Jumapili kuwa siku ya mapumziko kisheria?...Tena basi Jumapili haihusiani kabisa na Yesu wala Mungu..sasa sijui shetani nani?

Kuna vitu ambavyo vinatakiwa kuachwa kama vilivyo kwani Ujamaa wetu haukujengwa kwa ku-question kila kitu kwa rangi zake bali tunatazama madhara yake kwa jamii nzima.

Jambo la mwisho ni kwamba kumekuwa na propaganda za nchi za magharibi kuhusu hili neno sheria kiasi kwamba limetumika vibaya kama vile neno Terrorist ama Jihad linahusiana na waislaam, wakati huo huo wapigania haki na Crusade ni maneno yanayokubalika pamoja na kwamba malengo ya wahusika ni moja ila inakuwa twisted kuondoa mrengo.

Ningeomba sana viongozi wa dini ya kikristu watueleze ubaya wa mahakama hii kwa jamii yetu ikiwa sheria za mahakama hizi zitawahusu waumini wa kiislaam tu katika maswala machache ambayo yametokana na kiapo chao cha ndoa. Ikiwa serikali inatambua shahada ya ndoa za kiislaam nashindwa kuelewa zinatambuliwa vipi na kwa sheria gani wakati ndoa hizi zinafungwa kwa sheria za kiislaam.

I wouldn't mind kama wakristu, Hindu, Budha ama Jews wataweza kuwa na suluhu za maswala ya kidini kupitia sheria za dini zao(kama zipo), kwani sintashangaa mwanamke wa kikiristu akidai taraka kwa sababu mumewe kaoa mke wa pili. The fact is kuna dini ama waumini wa dini wanaosema hawataweza kuoa/ kuolewa na mtu ambaye sio dhehebu lake. Je, huu ni ubaguzi ama ni haki ya mtu kuchagua mchumba amtakae kutokana na imani ya dini yake...

kwa hiyo tuwe na upeo mkubwa zaidi ktk swala hili zaidi ya kutazama rangi zetu na kwa waislaam ningependa sana kama kweli wanataka mahakama ya kadhi basi nao wafuate sheria za dini hasa katika maisha yao na sio kuvuta sheria ambazo zinaleta utata ktk maamuzi yake. Mathlan huwezi kuoa mke wa pili ikiwa huna ridhaa ya mke wa kwanza na sababu iwe wazi na kubwa kiasi kwamba kweli unaoa kwa kufikiria familia yako na sio nyege zako za chini. waislaam wengi Tanzania wana watoto nje ya ndoa zao jambo ambalo linaleta taabu ktk mgao wa mirathi na mahakama ya kadhi haiwezi kutoa haki sawa kwani sheria ya dini hairuhusu kuzaa nje ya ndoa. Nadhani swala hili halina waislaam wala wakristu haikubaliki pande zote. Matumizi ya mahakama ya kadhi itazidisha matatizo kwa waislaam wengi ambao wamefuata zaidi utamaduni wa mwafrika kuwa na wake wengi bila ridhaa ya yeyote yulew maadam mwanamme anajiamini badala ya sheria ya kidini.

If and when every Muslim follow the sheria, then we can adopt some of the sheria kwa wahusika maadam serikali yetu inatambua na kuheshimu shahada hizo. Otherwise, mahakama hizi hazina nafasi kabisa ktk taifa ambalo watu wamekubali kuchanganya ndoa zao bila kujali rangi za dini ama race. Kusema kweli Kenya na Uganda wao waislaam na wakristu ni tabaka jingine ktk makundi ya makabila yao wakati Tanzania siku hizi watu wanaoana bila kujali dini...hesabu ya ndoa nje ya dini ama madhehebu ni kubwa sana pia watoto nje ya ndoa ni kubwa sana.. mahakama ya kadhi haitaweza kutoa haki sawa kwa wahusika na hasa watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
Naomba kuwakilisha!
 
....nahisi wanachama/watetezi wa mafisadi wameongezeka ghafla humu? njooni tuu tuwatoe nishai lakini vijitopic vya chama cha mafisadi vimezidi mno mpaka vinapoteza ubora wa mijadala...inabidi turudi kule kule kupambana na mafisadi for the betterment of our country sio mikutano yao na vizota au sijui wenyeviti,makatibu ni kupotezeana muda tuu hapa...tunataka sera za maana za nchi na kuwatoa wala rushwa na matapeli sio uchaguzi wa mafisadi tafadhari Mwiba,Punda,Kada na wengine mnajijua msitupotezee direction ya mijadala yetu na topic zenu za chama cha mafisadi kila kukicha...ooooh mara CCM itakufa lini/nani wa kuitoa CCM/CCM shoot back/wapinzani waionea gere CCM....inabidi tuanzishe forum pekee ya CCM,kweli CCM ndio wametuletea njaa sitaki hata kuwasikia!
 
hapo ^ (Koba) kama kweli nia yangu ni kupoteza direction yako/yenu basi hiyo nia ningeiweka wazi na SIOGOPI KUSEMA WAZI, lakini nilichokuwa nasema mimi binafsi tokea zamani, ni kutaka usawa katika mambo yote ccm, wapinzani, maendeleo ya taifa.

Kama ulikuwa hujui nini nilichokuwa nasimamia from the beginning basi ni rahisi kusema kwamba natetea ccm !

mtu akipingana kihoja na hoja za hao waliotoa majina ya watu waliowaita Mafisadi basi nae anakuwa mtetezi wa mafisadi ?since when ? usidhani kwa kuwa slaa katoka na hiyo list ya mafisadi ndio nikubaliane nae kila kitu, no way !
 
mtikila ni mtu wa kuogopwa.

anataka kupandikiza chuki za kidini ambazo hazipo! kweli tanzania ina freedon of speech, lakini isiwe kuwatukana wenzio, hasa kwenye sensitive issues kama dini na kinachoabudiwa.

kwa mtazamo wa mara moja, mtikila hawatakii mema watanzania wahali ya chini .

kwani hajui kama "vita vya panzi ziumiazo nyasi"?.
 
Mimi nadhani kwamba kama habari ile ya wamachinga, wananchi wanaangalia mipaka ya haki yao. Mtikila anafahamika kama mtu ambaye ana-push the limits, lakini anasaidia kuweka precedence. Kama atasaidia ku-define mipaka ya freedom of expression he will have done us all a huge service, he challenges and prods and pushes. Ni lazima mtu kama huyu asiwe 'mzima' but we do need catalyzers kama hawa. Kumwogopa si vizuri, tujaribu kuangalia sheria inasemaje. Kwani alipopeleka hoja ya independent candidate katika uchaguzi mbona tulimwona 'chizi' lakini after many years aliposhinda kesi tukaona kafanya la maana. We have to be open minded about this. Tusiogope kila kitu.
 
....nahisi wanachama/watetezi wa mafisadi wameongezeka ghafla humu? njooni tuu tuwatoe nishai lakini vijitopic vya chama cha mafisadi vimezidi mno mpaka vinapoteza ubora wa mijadala...inabidi turudi kule kule kupambana na mafisadi for the betterment of our country sio mikutano yao na vizota au sijui wenyeviti,makatibu ni kupotezeana muda tuu hapa...tunataka sera za maana za nchi na kuwatoa wala rushwa na matapeli sio uchaguzi wa mafisadi tafadhari Mwiba,Punda,Kada na wengine mnajijua msitupotezee direction ya mijadala yetu na topic zenu za chama cha mafisadi kila kukicha...ooooh mara CCM itakufa lini/nani wa kuitoa CCM/CCM shoot back/wapinzani waionea gere CCM....inabidi tuanzishe forum pekee ya CCM,kweli CCM ndio wametuletea njaa sitaki hata kuwasikia!


Ndiyo maana balozi za Marekani na Russia karibu kila nchi zinajengwa karibu karibu.
Hutakiwi kucheza mbali na adui yako.
 
Hivi kuna sheria ya kumfunga mtu kwa sababu katukana?....

Mzee, TZ kutukana ni kosa la Jinai. Si mtikila tu watu wengi washaenda selo. Ukitaka kuona design hizo nenda vimahakama vya mwanzo!!!

Mara nyingi matusi au lugha kali zinatoka mtu anapoishiwa hoja. Mtikila ambae wengi tunaamini ana hoja nyingi sijui kwanini huwa anakimbilia matusi/kashfa.

Niliwahi kumsoma ndugu yangu Mnyika akilalamika siku moja humu JF na wengi tulikuwa upande wake. Si suala la demokrasia wajameni, ni swala la ustaarabu na uungwana zaidi, na hapo ndipo demokrasia yetu inapotofautiana na mabwana zetu wa magharibi.

Hivi anachunga nini huko kanisani kwake!!!!
kondoo wa mungu (Binadamu) au kondoo kikwelikweli, maana kondoo ni hayawani hawaoni tofatu ya tusi na hekima!!!
 
WaTanzania wanajukumu la kupanua uwanja wa freedom of expression haraka iwezekanavyo. Kama Rais huyu ni vile Mtikila anavyodai basi ana uhuru kama Mtanzania yeyote yule kusema hivyo. CCM imelewa madaraka na ingawaje upinzania Tanzania bado ni hafifu inapaswa waTanzania opinion leaders kama nyinyi mliyopo hapa JF kukashifu tendo hilo la CID. Leo kwa Mtikila kesho wako kwako au kwa managers wa JF.

Kikwete anapaswa kuelewa zaidi kuliko wote uhuru huu wa kutoa maoni yako bila wasiwasi. Yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na basi kaelewa sana diplomacy.

CCM na vibweka vyake wawache uwoga. Mtikila ni Mtanzania kamili na ana haki ya kutoa maoni yake ila ni lazima ayandhibitishe kwa mifano au kwa kurejelea maandiko au vitendo vinavyoidhinisha mashtaka yake dhidi ya CCM.

Until the Tanzanian civil society realises that CCM's hegemonic power is a danger in disguise like what used to be the case with KANU in Kenya, UPC in Uganda and ZANU PF in Zimbabwe more will continue to be humiliated before their families by CCM's operatives and arms of government in Nyerere's paradise, Tanzania.

Muacheni Mtikila now!
 
Until the Tanzanian civil society realises that CCM's hegemonic power is a danger in disguise like what used to be the case with KANU in Kenya, UPC in Uganda and ZANU PF in Zimbabwe more will continue to be humiliated before their families by CCM's operatives and arms of government in Nyerere's paradise, Tanzania.

Muacheni Mtikila now!

I cannot agree with you more. The disturbing truth is that we do not have a credible civil society.
 
Kitila Mkumbo,
Unaposema hatuna Credible Civil Society una maana gani? isije kuwa unatazama kwa tafsiri ya mzungu kama vazi la koti na tai.

Mimi binafsi nadhani ni sisi wenyewe tunapotosha issue nzima kwa sababu tumeshindwa kusoma, kuchambua na kuelewa nini hasa kilichomsukuma Mtikila badala yake tumelenga mawazo yetu kwa mtu mmoja.

Nimesoma maelezo ya Mtikila hayafai kabisa kupongezwa kwa kazi yake wala jitihada zake ikiwa lengo lake ni kubomoa. Blasphemy hata siku moja haiwezi kuwa ni haki ya kutoa maoni hasa pale yanapopotosha watu. Ebu rudia kusoma maneno haya kisha nambie ni kiasi gani cha haki hiyo kinatafutwa hapa:-

YALE ALIYOYASEMA MTIKILA:
MCHUNGAJI Christopher Mtikila anasema Serikali na baadhi ya viongozi wanampango wa kulibadili taifa la Tanzania kuwa taifa la Kiislamu.

Anadai kwamba rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi ni mjumbe tangu akiwa madarakani na alichaguliwa na taifa la Iran ili ahakikishe anayabadili mataifa ya Tanzania na Afrika Kusini kuwa ya Kiislamu.

Baadhi ya vikundi vya kiislamu vinavyo hubiri neno la mungu kwa dhehebu hilo, vinaruhusiwa kufanya hivyo pasipo mipaka huku vikundi vya kikisto kama biblia nijibu vikizuiwa na kupewa masharti.

Alisema hiyo ni dalili za rais mwenyewe ambaye nae, anamaovu mengi kulilazimisha taifa kuingia katika imani moja za Kiislamu.

“Maaskofu bila kujua sasa hivi wanakubali kuitwa Ikulu kisha kuandaliwa ftari, wao wanakula wanafurahi. Hawajui kwamba ni mikakati ya kusilimishwa inafanywa kwao,” alisema

Ukimuona mchungaji ameanza kuogopa kukemea maovu kwa kuhofia roho yake basi huyo ni ‘Mchungaji feki’ anasema Mtikila.

Kuna asiyejua misikiti yote nchini inafanya kazi ya kuuchafua Ukrito, inahubiri waungane ili wauteketeze kabisa.

Alisema kipindi cha uchanguzi watu, wakiwemo wachungaji waliogopa kutaja ushirikina wa Kikwete huku waking’ang’ania ni chaguo la mungu huo ulikuwa unafiki.

Mtikila alisema kwanza hata ‘Alah mtume wanaomuabudu waislamu ni shetani na ushahidi ninao naweza kutoa ushahidi hata mahakamani, wataalamu wameniletea nyaraka zote zinazoonyesha.

“Waislamu wanajiandaa kuanza kuwachinja wakatoliki lazima tuwe makini, roho ya woga ni roho ya shetani lazima tuwe jasiri kupambana,” alisema.

Kitila, How low can someone be kwenu nyie mpate kuona sababu hasa ya mawazo ya mtu huyu. Huyu kasukumwa na imani yake binafsi tena mtu huyu kiongozi. Just imagine Kiongozi mwingine yeyote wa Kiislaam asimame na kuweka madai kama hayo.. nini hatma yake. Sijawahi kusikia na wala sintategemea kuona kiongozi yeyote wa kisiasa ama kidini this LOW!
 
Mkandara, kwa upande wa Mtikila nadhani tunapomsikiliza au kusoma habari zake tuelewe anajaribu kufanya nini na kwanini watu makini ni lazima tushuku malengo yake.

a. Mtikila ana tatizo na Uislamu. Hili halifichiki. Madai ya Tanzania kufanywa nchi ya Kiislamu hayajaanza kwa Mtikila na yamekuwepo kwa muda. Tatizo ni kuwa hakuna mtu anayejitokeza kuyaonesha kuwa ni madai ya woga na yasiyo na msingi. Kama Tanzania itakuwa ni nchi ya Kiislamu haitakuwa kwa nguvu au kiujanja.

Hata hivyo anataka kutumia matukio ya sehemu nyingine duniani kutishia watanzania. Anachoshindwa kuelewa ni historia tofauti sana ya Uislamu katika eneo letu la Afrika ya Mashariki. Nimeandika kwa kirefu katika mfululizo wa makala yangu kuhusu Mahakama ya Kadhi (inayoanza kesho kwenye "Kulikoni") na kuoensha kwanini Mtikila hawakilishi mawazo ya Wakristu wengi na hawezi kuwakilisha Wakristu wengi.

b. Lakini la pili ni anajaribu kutest uhuru wa maoni katika Tanzania. Katika hili anakabiliwa na changamoto ya kusema mambo ya kichochezi (waislamu wanataka kuwachinja wakatoliki) nadhani hilo litamfunga. Lakini kusema vitu ambavyo ni kinyume na imani nyingine nadhani hiyo Katiba itamlinda. Katiba ilimlinda yule bwana aliyesema kuwa "Yesu si Mungu" kwa vile hayo ni mafundisho yanayopatikana katika Kurani. Hivyo akisema kitu ambacho anaamini ni mafundisho ya Kikristu au yanatokana na mafundisho ya Kikristu atalindwa na Katiba.

Kwa hivyo kwenye suala hili ni kuangalia ni wapi ambapo amevuka mstari wa kutofautiana maoni na wapi amefikia mahali pa kuleta uchochezi.
 
Kitila Mkumbo,

Kitila, How low can someone be kwenu nyie mpate kuona sababu hasa ya mawazo ya mtu huyu. Huyu kasukumwa na imani yake binafsi tena mtu huyu kiongozi. Just imagine Kiongozi mwingine yeyote wa Kiislaam asimame na kuweka madai kama hayo.. nini hatma yake. Sijawahi kusikia na wala sintategemea kuona kiongozi yeyote wa kisiasa ama kidini this LOW!

Mkandara ndio hivyo tena, hndio hapo wazungu wakasema huwezi ukala keki na ukawa nayo wakati huohuo. Maadamu tumeamua kuwa katika ulimwengu wa demokrasia inabidi tukubali raha na karaha zake. Karaha ni pamoja na to tolerate the intolerable, otherwise Mtikila ametoa maoni yake jinsi anavyoona mambo, ana haki; sisi wengine tunawajibu wa kupima anayoyasema na ama kukubaliana nayo au kuyakataa kadri nafsi zetu zinavitutuma. Kwa kusema aliyoyasema haina maana kwamba ndio ukweli au uongo, hayo ni maoni yake. Kwani mimi nikisema nachukia ukristo au uislamu inamaanisha kwamba ukristo au uislamu umeshakuwa mbaya au ni mimi ninavyojisikia? Je, sina haki ya kujisikia ninavyotaka? Na je, si haki ya kutoa hisia zangu kwa kadamnasi?

Ajabu ni kwamba wewe hapa tayari umeshapitisha hukumu kabla hata mzee wa watu hajaenda mahakamani, jamani mwee, haipaswi kuwa hivyo. Una haki ya kuyadharau na kuyakataa aliyeyaongea Mtikila, lakini huna haki ya kumhukumu kwa mujibu wa sheria zetu na dini zote pia!

Wamwachie, wampeke mahakamani sheria ifuate mkondo wake. Mambo ya kuwekana lupango ni ya kizamani sana.
 
Watu kama akina Mtikila ni hatari kwa Taifa maana anawaamsha waliolala.kusema kweli Waislam wa Tanzania na kusini mwa Afrika kwa ujumla ni watu baridi sana,kuna kesi nyingi hawa watu wamebamizwa ikiwemo Tanzania kama ile ya kujiunga na umoja wao ambapo Msumbiji japo hakuna waislamu wa kiasi kikubwa lakini wapo kwenye umoja huo Waislam wa Tanzania hadi hii leo wamewekwa kwenye kona na hawana matumaini,pia ukitazama kwenye post nyingi za juu za uongozi wa tanzania basi waislamu ni wachache sana,lakini hawa akina Mtikila watawaamsha watu hawa na kuanza kudai kila kona tena kwa nguvu za hoja,na mifano hai ipo,hivyo alichokisema Mtikila kinaweza kuleta zaidi ya madai ya hayo mahakama yao ya kazi,ni kitu ambacho waslamu wenyewe wamekionyesha kuwa si mambo ya kukatana miguu wala mikono zaidi ya kesi zao za ndoa na kurisiana mali.Hata katika mabenki ya Ulaya siku hizi zipo sehemu zinafunction kwa hesabu za waislamu,huko hamna faida na ukikopa wanasema unalipa kilekile ulichochukua na hakujatokea wakristo kudai wanaleta na kulazimisha Uisilamu katika nchi zao zaidi ya wengine kunyemelea aina hizo za kuweka mahesabu na kukopa,huyu jamaa amevuka mipaka kwa kumchanganya na raisi kitu ambacho kitamletea tabu raisi katika utendaji na maamuzi yake,balozi wa uingereza wa marekani wamewandalia futari waisilamu,na waisilamu wamekwenda na wamekula sasa nina wasi wasi kuwa mtikila huenda ameletewa ujumbe kutoka mbinguni.
 
Hivi kuna sheria ya kumfunga mtu kwa sababu katukana?...
Ningependa kujua hili hata ktk nchi za magharibi kwani sijawahi kusikia mtu akifungwa kwa sababu kamtukana rais wa nchi. Ila nilichowahi kusikia ni mtu kuifukuzwa kazi na kuwekewa kauzibe asipate ajira tena ktk fani alokuwa nayo. Mara nyingi huombwa aombe msamaha laa sivyo fitna inajengwa na hata kama kuna mashtaka huwa ktk mahakama ndigo za kijamii.
Kutukana Kutokana na sheria ya nchi yetu ni kosa si Mkutana Rais tu hata Kumtukana Mwananchi yeyote tu.
 
Mimi sijui mnaomtetea Rev.Mtikila kwenye hili mnasukumwa na nini?Hivi ni dini gani iliyohalalisha matusi tena kwa kuonyesha jeuri anakubali ?Hivi ni KWELI PAMOJA NA MAPUNGUFU YA RAIS WETU NI KWELI NI GAIDI?Wote tunaelewa Dunia yetu ya Leo hii Ukiitwa Gaidi unawekwa kundi gani na jumuiya Za kimataifa?
Jamani heshima ni kitu cha bure sasa Mtikila kuna mengi mazuri ameyafanya ya kutetea Haki na Nilimuunga Mkono Lakini Kwa Hili NAFIKIRI AMEVUKA MPAKA WA UHURU WAKE WA KUJIELEZA!
NA ANAVUNA ALICHOPANDA.
Hapa tunamsema kila siku Rais ni katika kurekebishana na kuchangia mawazo Lakini Hatumtukani Kuna hata watu humu wakitukanwa wanakuja juu na wengine kuomba aliyefanya hivyo aadhibiwe KWA MODERATOR?Je Ni kwanini inakuwa hivyo?
 
Mtikila ana matatizo yake binafsi,lakini ina bigger picture,tatizo ni zaidi ya "ukorofi wa Mtikila" bali UOGA na UNAFIKI.Hivi Mtikila ndio mtu wa kwanza kuonyesha upinzani wake dhidi ya mpango wa kurejesha mahakama ya Kadhi?Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wametamka bayana kwamba hawaungi mkono wazo hilo

Kuna UOGA wa kujadili mustakabali wa Taifa pindi linapokuja suala la dini.Kisingizio kikubwa ni eti "serikali haina dini bali wananchi wana dini zao" au "ni dhambi kuchanganya dini na siasa".Kuna UNAFIKI kwa sababu serikali imekuwa inakwepa kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kidini kwa kudhani ipo siku matatizo hayo yatapotea yenyewe.Mie ni Mkristo lakini nafahamu "substance" kwenye hoja za baadhi ya Waislam kuhusu maendeleo yao katika elimu (it's a complicated issue lakini serikali inabeba lawama kwa kuamua kukaa kimya as if haisikii malalamiko hayo).

Let's be honest,je Maaskofu hao waliopinga suala la kadhi walikuwa wanajiwakilisha wao wenyewe au ni reflection ya attitudes za waumini wao?Serikali iliwajibu nini?So far,msimamo wa serikali kuhusu suala la kadhi ni zaidi ya kichekesho.Wakati wa kampeni,CCM iliahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo (ufumbuzi pekee kwa Waislam ni kurejesha mahakama hizo) lakini baada ya kurejea madarakani kumekuwa na dandana nyingi kuliko vitendo.Maswali ambayo serikali (kwa niaba ya taifa) inatakiwa kuyajibu na kuyatolea maamuzi ni pamoja na JE HISIA ZA WASIO WAISLAM NI ZIPI KUHUSIANA NA SUALA HILO?ZINA MANTIKI?ZIKIPUUZWA AU KUFUATWA ZITALINUFAISHA/ZITALIATHIVRI VIPI TAIFA?

Mtikila ni opportunist,lakini just like Hitler,Musolini,Le Pen,etc watu hao wanapata fursa ya kuropoka wanavyoropoka baada ya kutengenezewa mazingira mwafaka ya kufanya hivyo.Busara inahitajika katika kuendelea na kesi hiyo kwani kuna maswali magumu kwa watawala wetu kuyajibu pindi yakitolewa mahakamani.
 
Mimi sijui mnaomtetea Rev.Mtikila kwenye hili mnasukumwa na nini?Hivi ni dini gani iliyohalalisha matusi tena kwa kuonyesha jeuri anakubali ?Hivi ni KWELI PAMOJA NA MAPUNGUFU YA RAIS WETU NI KWELI NI GAIDI?Wote tunaelewa Dunia yetu ya Leo hii Ukiitwa Gaidi unawekwa kundi gani na jumuiya Za kimataifa?
Jamani heshima ni kitu cha bure sasa Mtikila kuna mengi mazuri ameyafanya ya kutetea Haki na Nilimuunga Mkono Lakini Kwa Hili NAFIKIRI AMEVUKA MPAKA WA UHURU WAKE WA KUJIELEZA!
NA ANAVUNA ALICHOPANDA.
Hapa tunamsema kila siku Rais ni katika kurekebishana na kuchangia mawazo Lakini Hatumtukani Kuna hata watu humu wakitukanwa wanakuja juu na wengine kuomba aliyefanya hivyo aadhibiwe KWA MODERATOR?Je Ni kwanini inakuwa hivyo?

Inabidi utulie upitie tena maandishi ya wachangiaji wenye maoni tofauti hapa. Hakuna anayemtete au kumkandamizi Mtikila hapa. Hapo kinachogomba ni uhalali na haki ya mtu kutoa hisia zake pamoja na kupinga mtu kuhukumiwa nje ya mahakama kama baadhi yenu mnavyofanya hapa. Nyie mnatia Mtikila hatiani kama nani? Tunapinga vilevile hii tabia ya kumsweka ndani badala kumfikisha mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Ni hilo, kwamba alitukkana matusi na kama amevunja sheria, ni mahakama ndiyo yenye uwezo wa kuamua, sisi hapa hatuwezi!

Mwisho ni swala zima la uvumilivu. Tunachosema ni kwamba huwezi kukuza demokrasia bila uvumilivu. Sasa demokrasia inahitaji uvumilivu pamoja na wananchi kama Mtikila. Bila uvumilivu hakuna demokrasia. Sasa wewe ukiambiwa ni gaidi na wakati unajua sio gaidi, tatizo liko wapi? Au mtu akikwambia wewe ni mwanamke wakati wewe inajulikana kuwa ni mwanamume ndio kusema utageuka kuwa mwanamke? Ingekuwa ni hivyo akina Bush na Blair wangeshafunga watu wangapi katika utawala wao? Leo hii mchana nilikuwa naangalia katuni inayomwigiza Gordon Brown, ni ya ajabu na ya kudhalilisha mno, tena kwenye BBC. Lakini Gordon anaendelea na uPM wake bila kutetereka wala kunyooshea watu vidole achalia mbali kusweka watu ndani. Sasa sisi mtu kusema wewe ni gaidi imekuwa nongwa? Ndio kusema urais wako unapungua thamani? Nani mwenye wajibu hapo, Mtikila kuthibitisha kauli yake au huyu aliyeambiwa ni gaidi kuthibitisha kwamba yeye sio gaidi? It take two to tangle!
 
Kitila,
Mkandara ndio hivyo tena, hndio hapo wazungu wakasema huwezi ukala keki na ukawa nayo wakati huohuo. Maadamu tumeamua kuwa katika ulimwengu wa demokrasia inabidi tukubali raha na karaha zake. Karaha ni pamoja na to tolerate the intolerable, otherwise Mtikila ametoa maoni yake jinsi anavyoona mambo, ana haki; sisi wengine tunawajibu wa kupima anayoyasema na ama kukubaliana nayo au kuyakataa kadri nafsi zetu zinavitutuma. Kwa kusema aliyoyasema haina maana kwamba ndio ukweli au uongo, hayo ni maoni yake. Kwani mimi nikisema nachukia ukristo au uislamu inamaanisha kwamba ukristo au uislamu umeshakuwa mbaya au ni mimi ninavyojisikia? Je, sina haki ya kujisikia ninavyotaka? Na je, si haki ya kutoa hisia zangu kwa kadamnasi?
Noo mjomba hapa unakosea kabisa kwani hiyo demokrasia haizungumzi hivyo hata kidogo. Blasphemy haina demokrasia wala nafasi ktk serikali yeyote ile na ndio maana kuna watu wametengwa ya jumuiya fulani kwa sababu ya maneno makali kama haya. Huwezi kunambia leo mzungu akikuita wewe kwa kutumia N word ni haki yake wala wewe kumwita mwanamke mbwa jike ni haki yako ya kimsingi.

Tukumbuke kwamba haki hutolewa pale unapoemlezea haki zako wewe na sio kumpangia mtu mwingine imani fulani. ndio maana tunapinga sana imani ya waislaam wenye siasa kali wanapojaribu kueneza propaganda za dini.
tatizo lako nawe unatazama upande mmoja wa shilingi. Leo hii hakuna demokrasia hiyo hiyo kwa waislaam ama nchi za kiislaam zinazoendesha propaganda kama hizi kuhus Amerika, tena ndani ya Amerika na nchi za nje viongozi wengi wametiwa ndani kwa sababu tu wamejaribu kueneza chuki za wananchi kwa Marekani.

Sasa nikuonyeshe kwamba mimi natazama pande zote ni kwamba nakubaliana kabisa na hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi kama hao ambao malengo yao ni kuunda Uadui kati ya waislaam na Marekani na nafahamu kwa uhakika unakubaliana na hili. Ila inapokuja kwa waislaam wengi wenu mnaona hii ni haki ya huyo Mtikila kuponda na kutukana dini nyingine hali haikubaliki kama blesphamy itatumika kuhusu Yesu.

Mwanakijiji,
Yule Muislaam aliyekingwa na sheria baada ya kusema 'Yesu sio Mungu" haimfanyi yeye kuwa na haki tunayozungumzia, pili sio kabisa imani ya Kikristu kuwa Yesu ni Mungu kwa tafsiri unayotaka wewe kuifikiria ama kuieneza. Labda unashindwa kuelewa tofauti kati ya mtu anayesema Yesu sio Mungu na yule anayesema Mungu (Allah) ni shetani na he can prove it!..

Yesu sio Mungu - This is the matter of faith between two religion on GOD na pengine ndani ya Ukristu kuna madhehebu yanayosema kuwa Yesu sio Mungu kutokana na tofauti za tafsiri za baadhi aya fulani lakini unaposema Allah ni Shetani, this is beyond mafundisho ya dini yoyote ile iwe toka Biblia ama kitabu chochote. Ni mawazo ya mwendawazimu asiyefaa hata kupanda jukwaa la dini kwani haifundishi kitu na pili ni ufinyu wa Elimu.
Kwa hiyo utaona kwamba Mtikila kamtumia JK ama Mwinyi kama ni nyenzo ya kupitishia ujumbe wake as a fact lengo lake ni kuukashifu Uislaam. Huyu Mtikila sio mtu wa kawaida ni kiongozi wa dini na pili kiongozi wa kisiasa.... Ni mtu hatari sana.

Kufungwa hawezi kufungwa kwa sababu sijaona sheria ya matusi kutumika kama ni kosa la jinai nchi nyingi hadi majuzi tu walipoona jinsi gani watu wanaweza kuwa brainwashed na mafundisho kama haya. Na hasa imetokea tu baada ya kuona haki hiyo ikitumiwa na waarabu against the west ndio wamekuja fahamu madhara ya matusi kama haya lakini before that no one cared. Akina Salman Rashdie na yule mwanamke wa Kisomali wamepewa hifadhi na serikali za nje lakini yule mwamerika ambaye yuko Pakistan akitoa maneno ya kujenga chuki kama hiyo ni Fugitive number one!...

Haya ndio yale yale niliyosema toka zamani kuhusu haki hizi toka nchi za magharibi..
Ni kosa kwa mwanamke wa kiislaam kuvaa Ushungi, Nikab ama Hijab nchi za Ulaya lakini ni halali kwa mzungu kuvaa kamtula nchi za Kiarabu hata kama waarabu wenye nchi hawataki.
This is double standard!
 
Mtikila yeye kasema Kiwete rafiki wake na nyie mnapinga..MAFISADI wanambinu nyingi watakuwa wamemtuma ajaribu kupunguza kasi
 
Ni Vyema Hili Suala La Udini Lisije Likasababisha Mapigano Ya Wenyewe Kwa Wenyewe!kwani Ni Wazi Tunaelekea Huko!uchochezi Wanaouzungumzia Nafikiri Unahusiana Na Hayo Mambo Ya Mahakama Ya Kadhi!shughuli Ipo!kama Kikwete Alishawaahidi Wasilamu Kabla Hata Ya Kuingia Madarakani Then Yuko Kwenye Hard Times Coz Sidhani Kama Hiyo Issue Itaridhiwa Na Wananchi Wote Bila Malumbano!
 
Back
Top Bottom