Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Tatizo ni lipi? Kwani JPM hana speech writer? Si kweli kwamba hajui Kiingereza. Labda kama mnaona accent yake ni tatizo. Lakini kila rais wa Kiafrika ana accent yake anapoongea lugha ya kigeni.Mie naona ni wakati muafaka wa kuanza kutumia Kiswahili. Rais Chissano wa Msumbiji aliishafanya hivyo kwenye mkutano wa AU lakini akina JK hawakuaona umuhimu wa kumuunga mkono.Kama shida ni lugha ya Malkia, ataongea lugha yetu. Hii lugha yetu inatumika katika mikutano ya AU na wakalimani wapo. Rais wa China alikuja hapa na aliongea kichina, sioni ajabu Mkuu wangu wa Kaya akiongea Lugha yetu adhimu katika kikao cha kimataifa kwani atakuwa anaienzi lugha yetu. Kiswahili Oyeee!