OMARI Gumbo wa Mtibwa Sugar atakuwa na haki ya kukumbuka na Watanzania baada ya kufunga bao safi na la ushidni kwa njia ya penati katika dakika ya 60 na kuiwezesha timu yake kutwaa kombe la Tusker baada ya kuifunga Mamlaka ya Mapato Uganda (URA) bao 1-0.
Penati iliyosababisha bao hilo ilitokana na beki wa URA, John Karangwa kumchezea vibaya Idrissa Rajabu aliyekuwa akichanja mbuga ndani ya eneo la hatari la timu hiyo kutoka Uganda.
Gumbo alipiga penati safi iliyomwacha kipa Abey Dhahiri, akiruka upande wa kulia na mpira kutinga wavuni upande wa kushoto. Katika mchezo huo, Mtibwa ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini ubutu wa washambauliaji wake uliioksesha mabao ya wazi hasa kipini cha kwanza