Mtendaji amkata masikio mgoni wake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
AFISA mtendaji wa kijiji cha Marambeka wilayani Bunda, mkoani Mara, Kipa Kigombe (52), amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, akituhumiwa kumkata masikio, Shaga Isaka, kwa madai ya kumfumania akifanya mapenzi na mke wake.

Mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Hamza Mtogwa, aliiambia mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Joackim Tiganga, kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 21, mwaka huu majira ya saa 6:30 usiku, katika kijiji cha Marambeka.

Alidai kuwa ofisa mtendaji huyo alimfumania Shaga Isaka (20), mkazi wa kijiji hicho, akifanya mapenzi na mke wake aitwaye Mariamu Kipa (22), baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mtuhumiwa baada ya kupata taarifa hizo aliamua kufuatilia na ndipo alipofanikiwa kuwakuta wagoni wake ndani ya nyumba wakifanya mapenzi.

Inadaiwa kuwa baada ya ofisa mtendaji huyo kumfumania kijana huyo, alimshambulia kwa kipigo na kutaka kumkatakata kwa panga lakini wananchi waliofurika katika eneo hilo walimzuia lakini alifanikiwa kuyakata masikio ya mlalamikaji.

Kwa mujibu wa Inspekta Mtogwa, mtuhumiwa aliamua kufanya kitendo hicho kwa madai ya kutaka kumuachia alama mgoni wake ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wanaotembea na wake wa watu.

Afisa Mtendaji huyo amekana mashtaka yake na yuko nje kwa dhamana.
 
statistics:
mume miaka 52
mke miaka 22
mgoni miaka 20

sasa hapo kati ya mume na mgoni nani saizi ya huyo dada. ndoa zingine unakuta structure yake tu in potential nyingi sana za migogoro.

huyo babu aloa mtoto wake na si mke wake.

huko vijijini kuna kazi kuhusu haki za wasichana kuliko huku mijini, pengine kabinti ka watu kaliachishwa masomo na si ajabu kameenda kuwa kake ka kumi kwa yule mzee na si ajabiu kameishazaa mara sita mpaa sasa kwa umri huo!

tamwa nendeni huko haraka mfute kesi ya ugoni na muanzishe ya haki za binadamu(msichanan)
 
supported ila dogo alitakiwa kuheshimu ndoa.Ttizo ni pale unawezekana walisoma pamoja au ndio binti alilazimishwa aolewe na mzee , yaani taabu tupu.

singles muwe makini sana kutafuta mke, kuwa na mke ukijua kabisa hautamuamini, kwa nini ujipe presha??
 
Mmmh.. sasa kila mmoja ana makosa..mgoma droo. Ila mwanamke aah..hajaadabishwa. Labda ataambiwa arejeshe mang'ombe ya mahari ..
 
Jamaa anastahili status ya 'temporary insanity' kwani alishuhudi mali yake halali ilikuwa inamegwa na mwizi naye kutokana na 'uchizi' alioupata baada ya kushuhudia kadhia hiyo alishtukia kang'oa sikio la mgoni wake.
 
AFISA mtendaji wa kijiji cha Marambeka wilayani Bunda, mkoani Mara, Kipa Kigombe (52), amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Bunda, akituhumiwa kumkata masikio, Shaga Isaka, kwa madai ya kumfumania akifanya mapenzi na mke wake.

Mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Hamza Mtogwa, aliiambia mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi, Joackim Tiganga, kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 21, mwaka huu majira ya saa 6:30 usiku, katika kijiji cha Marambeka.

Alidai kuwa ofisa mtendaji huyo alimfumania Shaga Isaka (20), mkazi wa kijiji hicho, akifanya mapenzi na mke wake aitwaye Mariamu Kipa (22), baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mtuhumiwa baada ya kupata taarifa hizo aliamua kufuatilia na ndipo alipofanikiwa kuwakuta wagoni wake ndani ya nyumba wakifanya mapenzi.

Inadaiwa kuwa baada ya ofisa mtendaji huyo kumfumania kijana huyo, alimshambulia kwa kipigo na kutaka kumkatakata kwa panga lakini wananchi waliofurika katika eneo hilo walimzuia lakini alifanikiwa kuyakata masikio ya mlalamikaji.

Kwa mujibu wa Inspekta Mtogwa, mtuhumiwa aliamua kufanya kitendo hicho kwa madai ya kutaka kumuachia alama mgoni wake ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wanaotembea na wake wa watu.

Afisa Mtendaji huyo amekana mashtaka yake na yuko nje kwa dhamana.

Huo Mtenange wa kibinti cha miaka 22 anauweza? maana anamzidi miaka 30.
 
Back
Top Bottom