Mtei yuko right - AN NUUR

Status
Not open for further replies.
Hili gazeti limesema kweli tupu; Hongera mzee Mtei; inahitajika usawa katika sekta zote za uma na sio kwenye Tume tu. HONGERA MZEE MTEI
 
hichi kizee siyo lugha ya ustaarabu.Pia usichukie watu,chukia wanachokifanya.
 
Mwisho wa udini katika teuzi za rais ni 2015, bila kujali rais atatoka chama gani.
 
Gazeti la kiislam la AN-NUUR katika hali ya kushangaza limeibuika na kuunga mkono kauli ya mwanasiasa mdini Edwin mtei na kuwataka eti watanzania kumpongeza mzee huyo,hii nchi kama siielewielewi vile..



Binafsi sioni msingi wa hoja ya Mtei.Kama Raisi amechagua wajumbe hawa kwa kuzingatia,ujuzi na uzoefu wao siono kama kuna tatizo.Ila kama aliichagua kwa lengo watu wa dini fulani au kabila fulani basi hapo kuna matatizo,ingawa hili atuwezi kulielewa,raisi mwenyewe anajua.Watanzania wenzangu mimi nafikiri kama ikifika wakati dini ya mtu inakuwa kigezo namba moja na si ujuzi alio nao,hii ni hatari kwani sio tu kwamba itazorotesha ufanisi,bali pia tutakuwa tunapiga hatua kuelekea kwenye machafuko,migongano ya kidini.Mungu Ibariki Tanzania
 
Huyu Mzee wangu kalizua..mana watu watataka uwiano wa Kidini na haiishii kwa Ukristu na Uislam tu...twende mbali mpaka kwenye Ukatoriki, Anglikana na Ulutheri, kwenye Usuni na Ushia, kwenye dini za asili, Butha na Uhindu. Tukimaliza hapo tuje kwenye uwiano wa kijinsia. Tukimaliza hayo uwiano wa kikanda, kikabila nao utupiwe macho.
 
hawa jamaa wanasema mtei yupo sahihi kwa sababu siku zote wanasema chadema chama cha kidini watu wanakataa, sasa Mungu kaamua kuweka hadharani kupitia mwanzilishi wa chama ili watu wote wajue.
Wanasema Mtei yupo sahihi kwasababu anacho kisema ndo malengo ya chama chake. kwahiyo ndo maana wanasema hajakosea. Amedhamilia kudhihilisha udini. Mimi hayo maneno niliyasikia jana kwenye radio Iman walipokuwa wanajadili hiyo maada kuhusu mtei.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom