Janjaweed
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 13,157
- 10,654
Suala la udini ni suala ambalo muasisi wa taifa hili julius nyerere alilipigia sana kelele kipindi cha uhai wake.Leo katika hali ya kushangaza watu wawili kutoka vyama vikuu viwili vya upinzani tanzania wamenukuliwa wakitoa kauli zenye chembe chembe ya dalili za kutaka kuigawa nchi na wananchi kwa kutumia kigezo cha dini,watu hawa wawili ambao chonde chonde nawaomba watazania wenzangu tuwapuuze ni muasisi mwenye sauti kubwa ndani ya chadema bwana Mtei na kiongozi mwanadamizi na mwenye sauti kubwa ndani ya cuf ISMAIL JUSSA.
Akiuzungumzia uteuzi wa wajumbe wa tume ya katiba bwana mtei bila haya alitoa kauli ya kilevi kwamba eti tume hiyo imejaa waislam!sina uhakika kama mzee huyu alikua na uhakika na anachokisema ama alikua anataka kusema labda tume hii ina watu wengi wenye majina ya kiislam..all in all timing ya kuitoa kauli hii ilikua ni mbovu hasa ikizingatiwa kwamba ndio kwanza tume imeteuliwa ikiwa hata haijakutana huyu mzee anaamua kuivuruga kwa makusudi ili siku ziende tukifike kwenye uchaguzi bila katiba mpya kama jk vile anataka iwe.
Ya Jussa sina haja ya kuyarudia yote kwa kuwa kila mtu humu unajua matatizo ya jussa kwenye udini kali kuliko zote ni pale aliposema chama chake kimeshindwa uzini kutokana na jimbo hilo kujawa na wakristo!
Hawa wawili ndio viongozi wetu wanaozitumia dini kufanikisha malengo yao,ndio mana nikaswema MTEI na JUSSA NI WATU HATARI SANA KWA TAIFA,TUWAOGOPE KAMA UKOMA,NAPENDEKEZA RAIS KIKWETE AFANYE MAAMUZI MAGUMU KWA KUWAKAMATA NA KUWATIA NGUVUNI MARA MOJA ILI IWE FUNDISHI KWA WENGINE WENYE MAWAZO YA KIJINGA KAMA HAWA WAWILI.
Nawasilisha
Then utakua na matatizo makubwa ya akili.... nikadhani utazungumzia Rostam, Mkapa, EL, JK, Kighoma Malima, Mramba, Balali
Mwasisi wa udini unamuacha halafu unakurupukia watu wawili tu tena wasio na mamlaka kihivyo