Mtei awashauri viongozi CCJ wahamie CHADEMA

wa ccj ndipo utakapowekwa wazi....Coz inashangaza kama huelewi kuwa mara baada ya kuiong'oa ccm si inatakiwa muunde serikali?

Mnaunda serikali ikiongozwa na nani, kwa sera zipi zenye misingi ipi? Mkiungana CUF na CHADEMA halafu mnaunda serikali mnatuata sera zipi, za nani na kwanini?
 
itoke ili kiwe nini? hili ni swali ambalo hamtaki kujibu. Tutakuwa ni watu wajinga zaidi duniani kuuondoa chama tawala halatu hatujui tutaweka nini.. remember Somalia? Si walimuangusha Siad Barre? and then what.. Kenya walimuangusha Moi.. then What? Malawi walimuangusha Hastings then what? Zambia walimuangusha Kaunda then what?

Oops, one moment, now I can see
 
Mnaunda serikali ikiongozwa na nani, kwa sera zipi zenye misingi ipi? Mkiungana CUF na CHADEMA halafu mnaunda serikali mnatuata sera zipi, za nani na kwanini?
Ndugu yangu MMKJ rudisha roho yule wa zamani huyu MMKJ wa leo si yule tuliyemzoea aliyekuwa anatuletea tenzi na zomari za enzi zile, enzi zile hukuwa unauliza tujiunge upinzani ili iweje, enzi zile hukuwa unampinga Kikwete ili iweje, leo haya maswali umeyatoa wapi hii about turn inatia mashaka, rudi kundini utusidie kuyajibu hayo maswali ya 'ili iweje' tafadhari.
 
Mwanakijiji, ndugu yangu CCM itoke kwanza,zaidi ya hapo hamna nyimbo.

CCM watoke kwanza ili waingie nani? Kama ni CHADEMA tofauti yao na CCM itakuwa ipi?

Wameshindwa kuendesha uchaguzi wa Mwenyekiti, wameshindwa kuendesha uchaguzi wa Wanawake, wameshindwa kuendesha uchaguzi wa vijana mpaka wanaweka cronies wao akina Mnyika. Wakipewa madaraka hao unategemea wataheshimu hata tume ya uchaguzi?

Afadhali CUF angalau wanaheshimu demokrasia ndani ya chama chao.
 
CCM watoke kwanza ili waingie nani? Kama ni CHADEMA tofauti yao na CCM itakuwa ipi?

Wameshindwa kuendesha uchaguzi wa Mwenyekiti, wameshindwa kuendesha uchaguzi wa Wanawake, wameshindwa kuendesha uchaguzi wa vijana mpaka wanaweka cronies wao akina Mnyika. Wakipewa madaraka hao unategemea wataheshimu hata tume ya uchaguzi?

Hili bado ni jinamizi baya kwenye taswira ya CHADEMA, na ni ishara mbaya kwa nchi kama watashika dola.
 
CCM watoke kwanza ili waingie nani? Kama ni CHADEMA tofauti yao na CCM itakuwa ipi?
Kama wewe huoni tofauti wengine wanaona kuna tatizo gani ile ni CCM na hii ni Chadema moja ya sera yake ni utawala wa majimbo ambayo CCM hawana by the way si lazima kila mtu awe Chadema kama mtu haoni tofauti anaweza kuendelea aliko au anaweza kukaa bila chama hakuna haja ya kuwasemea waliokwenda ambako wewe hutaki, unaweza kutembelea tovuti ya Chadema inasema wazi kabisa kujiunga ni hiari na hata kuondoka ni hiari kama walivyofanya akina Kafulila.
 
Mnaunda serikali ikiongozwa na nani, kwa sera zipi zenye misingi ipi? Mkiungana CUF na CHADEMA halafu mnaunda serikali mnatuata sera zipi, za nani na kwanini?
Wewe mwenye chama hewa unayesajili wanachama hewa ulitaka usajili wa nini? ili uongoze nchi ipi? kwa uongozi upi ulionao? kwa wabunge wapi na madiwani wepi? au unafikiri serikali inaundwa na viongozi wawili tu wa kitaifa.

Serikali ya uingereza imeundwa na vyama viwili vyenye sera tofauti lakini kila chama kimekubali kuachia baadhi ya sera zake na kuchukua baadhi ya sera za mwingine na serikali ikaundwa kwa muda mfupi sana. Unataka kutuambia kabla ya uchaguzi Conservative walikuwa wanajua wataunda serikali na Liberal, kila chama kilijiamini kushinda lakini walikuja kuungana dakika za mwisho kabisa, kama wewe ni mfuatiliaji wa masuala ya siasa za uingereza Cons na Libs sera zao zilikuwa tofauti sana ukilinganisha na Labour na Liberal ambao sera zao nyingi zilikuwa zinafanana. Sera ni mkusanyiko wa mawazo ya watu ambayo yanaweza kubadilika muda wowote.
 
Teh teh teh

si mda mrefu mwanakijiji na Kishoka mtaitwa vibaraka/jasusi (The traitors) wa ccm ama lile fagio mrefu wa RA umemifagia kama inavosadikika na baadhi ya wana jf kwamba ulimpitia Zitto.

Wasu haya umeyatoa wapi? sisi sote tunajua kuwa mwanakijiji na Kishoka wote hawa ni wapiganaji, unajua kila kukicha naendelea kutambua kuwa kuna tatizo katika uwakilishaji wa hoja hapa jamvini, lakini naomba tutambue kuwa ni kwa nini tunagombea fito wakati tunajenga nyumba moja?
 
Wasu

Teh teh teh
Nimejaribu tu kuoanisha mwenendo mzima na jinsi itakavyokua unajua hata Zitto beef lake na baadhi ya wana jf lilianza hivi hivi.

Nakubaliana na wewe kuwa fito inayopiganiwa ni moja LAKINI unajua ugomvi unaanzia wapi? teh teh teh
Tatizo ni kwamba hiyo fito itajenga nyumba lakini nyumba inayotegemewa kujengwa ni tofauti. Kweli ufito ni mmoja na lazima ujenge nyumba lakini mshindi wa fito hiyo atajenga nyumba yake na si ile nyumba ya pamoja.
 
GS,

Tatizo ni kuwa tuna sehemu kubwa kati yetu ambao tunang'ang'ania ushabiki na kuamini kuwa Chadema ndicho chama mbadala. Labda ni ule mvuto wa Dr. Slaa, Chacha Wangwe, Zitto na Kitila. Lakini, hatuwezi kuendelea kuburuzwa kama enzi zile za kuwa Chipukizi wa CCM ambazo tulivutiwa na kunogewa na kusahau kuwa wadadisi na kuhoji mambo.

Humu ndani ya JF, kuna ngome kubwa sana inayoilinda Chadema, wala sitashangaa kuwa sehemu kubwa ya wana JF ni washabiki kama si wanachama wa Chadema. Sasa ukiandika kuwakosoa Chadema, fukuto litakalokufuata ni kubwa la kubezana na wala si kujenga hoja au kujibu hoja.

Mambo ya ubinafsi na kushambulia nafsi na si kuchambua hoja huanza, na ndio maana sehemu kubwa ya majadiliano hapa yamegeuka si kuchambua hoja na kujenga hoja za kukubaliana au kupingana bali ni kudai Mwanakijiji kapotoka au kaanza ku-dilute the message kisa kaongea dhidi ya Chadema.

Kama umeona, Shalom kanirukia na kudai eti nafuata nyayo za Mwanakijiji, na siku nikionyesha uhuru wa mawazo atatoa zaka! EBO!

Watu wameichoka CCM, lakini hawajui kupanga hoja ziuzike kwa kila roho Tanzania ili CCM ianguke. Ukitoa ushauri kwa mtazamo mwingine, unitwa msaliti au hujui unachokisema. Lakini kama nilivyomwwambia Dr. Slaa kwenye ile mada yangu ya Udhaifu wa Operesheni Sangara, ni kuwa huu ni mwaka karibu 20 tangu vuguvugu la Chadema na Upinzani kuanza kudai ni lazima CCM iondoke na kuondolewa, lakini kila siku zinavyozidi kusonga mbele, unaona CCM inazidi kushika hatamu pamoja na migongano waliyonayo ndani mwao.

Najiuliza kama Watanzania wameichoka CCM kama tunavyodhania, iweje ile kasi liyofanywa na TAA na TANU kumn'goa mkoloni ilifanikiwa kwa haraka, lakini vyama vya upinzani vinashindwa kuiangusha CCM? Je tuendelee na majaribio kuamini TLP, Chadema, CUF, NCCR, DP na hata sasa kukimbilia mgombea huru ndiyo suluhisho mpaka lini kama si kwa vyama hivi kujipima na kuanza kujiuza kwa kutuambia Itikadi zao ni zipi ili tuwe na uchaguzi basi wa kuamua tumtakaye?

Hatuwezi kujenga mfumo bora wenye msingi mzuri wa kisiasa bila kuwa na utambulisho wa kiitikadi ambao utatoa tofauti za kichama na kuwapa Watanzania uwezo kuchagua itikadi wanayopenda, sawa na dini zilivyo.

Hivyo tunaacha kujenga hoja, tunaanza shambuliana kisa hatutaki kusikia kukosolewa na hivyo kuwaacha CCM wakiendelea kukenua meno na kutamba ushindi mwingine ile Jumatatu bada ya uchaguzi mkuu.

Una uhakika kuwa sababu ni hiyo au wewe ndio mtazamo wako ni huo?ina maana CCM hakuna viongozi wenye mvuto hata mmoja?na CUF je hakuna kabisa?kama hili ni kweli kuwa watu wanaing'ngania CHADEMA kwasababu ya viongozi wao humu ndani ya JF then Slogan ya JF ibadilishwe..Kama sisi tunafanya hivyo,sijui walioko kule sitimbi mabao hawajapata kufikfiri chochote kuhusu nchi hii na makando kando yake.
 
naona demokrasia inaelekea kubaya....nini maana ya vyama vingi? pia mimi naamini mshindi aliyepitia njia ngumu ndiye shujaa wa kweli... hamkumbuki yaliyomkuta Nelson Mandela? MKOMBOZI WA KWELI LAZIMA APATE VIKWAZO VINGI......SIKU YA UKOMBOZI INAKUJA
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu heshima mbele.. I respect U so mucha kwa moyo ulokuwa nao lakini mkuu wangu hapa unachemsha vibaya sana. Unafikiria mbali sana kabla hujamaliza hatua ya kwanza, in a sense ni sawa na mtoto anayeulizia mgawanyo wa mirathi kabla baba hajafa!

Ebu fikiria hili moja rahisi sana, kulingana na hoja zako ktk mada nyinginezo unaonyesha kukiri kwa moyo na kubaini hapa kwamba CCM ipo nyuma ya kuhakikisha CCJ isisajiliwe..as to say without CCM hiyo CCJ ingesajiliwa! - Na kweli CCJ wameshindwa kusajiliwa na hamna jipya isipokuwa kutapatapa na itikadi zenu mkononi of which has no value kwa mlalahoi.

Tukio hilo tu nadhani ungefikiria makosa yaliyofanyika kufikiria ya kesho kabla hujamaliza ya leo. Kuweka matumaini makubwa ya Ushindi hali CCM anayeweza kukuzia imesimama imara. Na pia CCJ kukosa support ya wananchi (UMOJA) pia inachangia sana. Fikiria tu kama wananchi wote wangekuwa nyuma ya CCJ kuhakikisha haki inapatikana... Haikutokea hivyo kwa sababu CCJ kama wao, wamefikiria mengi ya kesho pasipo kuweka sawa ya leo na kibaya zaidi ni zile fikra za kwamba nguvu ya Itikadi inaweza shinda nguvu ya umoja kumwondoa adui mmoja..

Sisi Watu wa Kanda ya Ziwa, tukimwona Chatu hatufikirii ya kesho isipokuwa tunafahamu madhara yake.Hukusanyika tukamchua na kumtupa porini mmbali kabisa na mifugo yetu..Hata siku moja hatujadili yatakayofuata baadaye kutokana na kumtupa chatu porini ati kitafuata nini. Kila stage ya matukio ina mwanzo na hitimisho lake, mifugo ina maradhi ya tunatamtafuta mganga veterinary lakini hatupangi ugawanaji wanyama ikiwa ng'ombe hao watakufa..

Ni imani yangu siku zote kwamba mtu yeyote anayefikiria UMOJA ni UZEMBE ni sawa na anasema kwamba UMOJA huo wapo Walemavu, Maskini na Wajinga hivyo hapatakuwepo na nguvu ya Umoja ila udhaifu..Kwa hiyo hatuwahitaji. Katika Siasa za Demokrasia haya ni makosa makubwa sana ya kiutawala kwa sababu Chadema, CUF au vyama vingine ni wananchi kama wewe wenye Uhuru wa kuchagua imani yao ya itikadi pasipo kuvunja haki ya wengineo. Mjumuiko wa tofauti ya itikadi hizi huru kisheria ndio unajenga Taifa moja la kidemokrasia la Watanzania.

Na Uhuru kama huu ndio umetuwezesha sisi wote Waislaam, Wakristu, Budha, Hindu kutuweza kupata Uhuru wa kuabudu na leo tunaishi pamoja kila mmoja wetu akiabudu dini yake... Hatuwezi kutengana kiimani tulipoitafuta haki ya Kuabudu ati kwa sababu wale ni Wakristu au Waislaam who will lead who na nani watakuwa viongozi.Tukianza ku question ibada za wengine tutapoteza kabisa maana ya sheria ya haki hivyo kuifanya dini unayoipendelea kuwa superior zaidi ya nyinginezo..hapo ndipo mwanzo wa Ubaguzi unapoanza na fikra zinapoanza kuwa finyu..

Mkuu wangu nitamalizia tu kwa kusema itikadi ya CCJ ni bora tu kwa wale wanayoiamini sii lazima watu wote tuikubali na kutoikubali kwetu hakuwezi kuwa sababu ya kutounganisha nguvu zetu kupambana na adui yetu wote. Yote ulozungumza kuhusiana na itikadi ya CCJ yataweza kupimwa tu ktk utekelezaji kinyume cha hapo itabakia ni imani tu..Ukimsoma Salim. A. Salim ktkmada mojawapo humu JF utagundua kwamba matatizo ya Afrika sio itikadi ila Utekelezaji wa malengo yenyewe. Na hapa ndipo tulipokwama sasa hivi malengo ni kumwondoa CCM tunasuasua tukibishana kuhusu itikadi, sera, uongozi na kadhalika hali Chatu huyu Anakonda wetu CCM akiendelea kutumaliza..
 
itoke ili kiwe nini? hili ni swali ambalo hamtaki kujibu. Tutakuwa ni watu wajinga zaidi duniani kuuondoa chama tawala halatu hatujui tutaweka nini.. remember Somalia? Si walimuangusha Siad Barre? and then what.. Kenya walimuangusha Moi.. then What? Malawi walimuangusha Hastings then what? Zambia walimuangusha Kaunda then what?

Mkuu Mwanakjiji CCJ ikiitoa CCM itafanya nini?
 
Mzee Mwanakijiji, Mkuu wangu heshima mbele.. I respect U so mucha kwa moyo ulokuwa nao lakini mkuu wangu hapa unachemsha vibaya sana. Unafikiria mbali sana kabla hujamaliza hatua ya kwanza, in a sense ni sawa na mtoto anayeulizia mgawanyo wa mirathi kabla baba hajafa! Ebu fikiria hili moja rahisi sana, kulingana na hoja zako ktk mada nyinginezo unaonyesha kukiri kwa moyo na kubaini hapa kwamba CCM ipo nyuma ya kuhakikisha CCJ isisajiliwe..as to say without CCM hiyo CCJ ingesajiliwa! - Na kweli CCJ wameshindwa kusajiliwa na hamna jipya isipokuwa kutapatapa na itikadi zenu mkononi of which has no value kwa mlalahoi.
Mkuu Mkandara

Uliyosema ni kweli tupu adui wetu ni mmoja badala ya kushirikiana kumuua nyoka tunaanza kunyang'anyana fimbo, anachokifanya MMKJ sijui kama anakijua ni sawa na ulivyosema anafikiria mambo ya mbele zaidi ya kutoa kisiki kilicho karibu kwanza anasema tuungane ili iweje badala ya kujiuliza kwanini hatuungani kuna tatizo gani.

Ni kweli MMKJ anaonekana ni mpambanaji lakini wakati mwingine huwa anakosea step kudhani anaweza kushinda peke yake na kudhani mawazo yake yote ni sahihi matokeo yake ni kuanzisha hiki na kuacha kile bila kukimalizia. Na adui mara zote huwa anangalia palipo na weakness ni rahisi kwa alivyo kuingizwa mkenge au hata kununuliwa.

Kabla ya ujio wa CCJ MMJK aliweza kujijengea heshima humu JF kwa alivyokuwa anajenga hoja bila upenzi baada ya kuileta CCJ akadhani wote waliokuwa wako nyuma yake watasupport mawazo yake matokeo yake ikawa ndivyo sivyo, sasa amebaki kulazimisha pasipolazimika na kuwageukia waliobaki na misimamo yao na kuanza kuwalaumu viongozi kama kina Slaa kuwa hawajafanya kitu.
 
Mkuu Mwanakjiji CCJ ikiitoa CCM itafanya nini?

we have a program of the first 100 days na the first year..

Nitakuhakikishia kuwa baada ya mwaka mmoja; hakuna kesi yoyote ya ufisadi au jambo la ufisadi lililozungumzwa tangu mkapa litabakia midomoni mwa Watanzania.... huu ni mfano mmoja tu.. na hili ndilo tishio la CCJ.. they know what we want to do... hatutaki kuiondoa CCM ili iondoke halafu ndio tujue tunataka kufanya nini...
 
ooh no... unaanza kuniwekea maneno mdomoni mwangu.

a. Sijawahi kusema kina slaa "hawajafanya kitu".. nitakuwa mwongo na uongo siupendi kama ninavyochukia kuambiwa nimesema nisichosema. Nachagua maneno yangu vizuri sana.

b. Najua jawabu la kwanini "hatuungani" kwani linahusiana na jibu la "kwanini tuungane". Unauliza swali lile lile kwa namna tofauti; ni sawa na kuuliza kwanini gari limekwama kwenye matope halafu ukasema hilo swali haliulizwi kwanini gari halitoki kwenye matope.. utaona jibu ni hilo hilo moja.

c. Mojawapo ya mambo niliyojifunza katika maisha yangu haya mafupi ni kuwa sifuati makundi au upepo; sitafuti kuungwa mkono au kufanya watu wakubaliane nami ili nijue nimefanya vizuri. Katika vitu ninavyoamini niko tayari na radhi kuwa pekee na mpweke alimradi najua dhamira yangu iko safi katika hicho. Kama kitaonekana kimekosewa (kama nilivyosema kuhusu CCJ) niko tayari kulipa gharama yake na kuishi na matokeo yake lakini siwezi kuogopa kuchukua msimamo ninaoamini ni sahihi ati kwa sababu baadhi ya watu walioniunga mkono watageuka. Believe me.. hili halinipi shaka hata kidogo.

d. Ngoja nikutoe shaka kabisa.. hata kesho ukiniona napigia debe Chadema ni pale nitakapoona tumaini lililopo ndani yao; nilikuwa natumaini sana nao labda kuliko mtu mwingine yeyote. Lakini nimekuja kuelewa the same malady that afflicts CCM ndiyo hiyo hiyo imeikumba Chadema na hilo ndio tishio. Chadema ingeweza kuwa chama kikubwa kweli kweli na cha mabadiliko lakini kimepoteza nafasi nyingi za kufanya hivyo na matokeo yake kimegeuka purely chama cha matamanio ya madaraka tu. Hilo si tatizo.. tatizo ni kuwa hawatuambii wanataka madaraka ili wafanye nini?

Tukiliuliza swali hilo tuaambiwa "it doesn't matter.. tutoe kwanza CCM madarakani then tutajua cha kufanya" hili si jibu la watu makini.
 
we have a program of the first 100 days na the first year..

Nitakuhakikishia kuwa baada ya mwaka mmoja; hakuna kesi yoyote ya ufisadi au jambo la ufisadi lililozungumzwa tangu mkapa litabakia midomoni mwa Watanzania.... huu ni mfano mmoja tu.. na hili ndilo tishio la CCJ.. they know what we want to do... hatutaki kuiondoa CCM ili iondoke halafu ndio tujue tunataka kufanya nini...
Sasa MMKJ unaanza kuchekesha kwani kuna chama kisicho na program, mmeshindwa program ndogo tu ya kuandaa watu 200 mtawaweza hao mafisadi, huo mfano wako kila mtu anaweza kuusema hata TPP huwa wanasema hivyo hivyo tatizo ACTIONS...........
 
ooh no... unaanza kuniwekea maneno mdomoni mwangu.

a. Sijawahi kusema kina slaa "hawajafanya kitu".. nitakuwa mwongo na uongo siupendi kama ninavyochukia kuambiwa nimesema nisichosema. Nachagua maneno yangu vizuri sana.

Sawa inawezekana hujawataja kwa majina lakini huoni kusema Chadema hakuna inachokifanya ni sawa na kuwasema viongozi, utatofautishaje uongozi wao na chama au tuseme uongozi wao (Slaa, Mbowe,Zitto nk) mzuri kwenye familia zao tu na si kwenye chama tueleze uzuri wao uko wapi.

b. Najua jawabu la kwanini "hatuungani" kwani linahusiana na jibu la "kwanini tuungane". Unauliza swali lile lile kwa namna tofauti; ni sawa na kuuliza kwanini gari limekwama kwenye matope halafu ukasema hilo swali haliulizwi kwanini gari halitoki kwenye matope.. utaona jibu ni hilo hilo moja.
Hujajibu swali kwanini hatuungani na mfano wako ni irrelevant, kukwana kwa gari inawezekana ni uzembe wa dereva kaambia hiyo sehemu inatitia akakaidi, kutotoka si lazima uwe uzembe wa dereva.
 
Back
Top Bottom