Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Hoja ya Mtei kimsingi haijadiliki bila kuona idadi ya wingi tajwa. Kwa mfano kama ni 40 kwa 60 sioni shida na hoja yake inakuwa haina mashiko. Lakini mfano ni kuanzia 30 kwenda chini kwa 70 kwenda juu, nadhani kuna jambo la kufikiria na kurekebisha japo sio kisheria bali kinamna tunavyoishi, yaani hapa TZ kuna Katiba, Sheria, Kanuni/Taratibu na Mazoea.

Ili kujadili kwa kina hoja ya Mtei tunaomba kama kuna mtu anayo orodha kamili aiweke kwa wanaJF
 
Source Jambo Leo ~ Habari Leo. Labda ungesema ama tweet tungekuelewa.
Hii siyo reliable source......but/lakini kwa Zitto Kabwe everything is possible, binafsi nimeshachoshwa na Headlines za Zitto Kabwe na ndio maana sina hata hapetite ya kuchangia thread hii.
Ngoja niende kwenye thread za Kanumba huku kwenye jukwaa la siasa hakuna jipya ni same blah blah tu.
 
Hata Mtei alichoongea ni ukweli mtupu. Just a simple research inaonesha kuwa katika yale majina ya wajumbe wa tume ya katiba waislam ni wengi kuliko wakristo. Zitto kusema mzee Mtei azomewe ni ukosefu wa adabu, ingawa na mzee Mtei kwa hadhi yake hakustahili kuongea kauli kama hizo.

usipige sana mayoe wakiristo waliopo bara wata wawakilisha kwan zanzibar hapo mwanzo kulikua na ukiristo au ni wabara ndo walioupeleka??
 
sio fare kumshambulia mzee huyu. tujiulize, alilosema ni kweli au laa? kama ni kweli, shida iko wapi? kwenye inchi inayoingiwa na tensions za kidini kama hii ni muhimu sana kuliangalia kwa makini wazo la mzee huyu. kwa vyovyote ameona mbali! hata hivyo ni muhimu kuwa makini na zito kabwe.
 
asemao mtei ni ukweli, hata chongo anaweza kuona. naye si mtoto, anajua lizemalo. hata hivyo tuamini tuu kwamba waislamu hao watafanya kazi kwa maslahi ya umma na sio kutuletea udini.
 
Zitto omba radhi

Aombe radhi ya nini? Kama mzee mzima unaeza kusimama na kulipuka mambo ya kichochezi, tutamtofautishaje na yule chizi Jussa?
Huyu mzee amefilisika kimawazo, nilishasema hapa kwamba huyu mzee amechoka arudi zake kijijini akafuge makitimoto. Kuwa muasisi wa chama isiwe sababu ya kuongea upuuzi akitegemea watu watakaa kimya.
Huyu mzee ni tatizo ndani ya chama, nimesema haya na sitaogopa kusema haya na wala haitanipunguzia mapenzi yangu kwa CDM.
Bravo Zitto!!..
 
Kwa kuwa wote ni wana CDM, na Mzee Mtei ni kiongozi wake/baba/babu yake Zito, hakukuwa na haja Zito Kabwe kujibu hoja ya Mzee Mtei. Neno "kufilisika kimawazo" linazalilisha/linafisha moyo.
 
Haya ndio mambo hatukuyataka toka awali! rasimu ya muswaada wa mabadiliko ya katiba haikuletwa kwa wananchi waijadili, ndio maana unakimbilia kuuliza kama rais alizingatia taratibu au la. hauhoji uzuri wa taratibu hizo, ama zilivyowekwa. Utaratibu huu tayari unaonyesha ghilba imetumika. Hivi nani anawawakilisha wapagani kwenye hiyo tume, TUTARAJIE KUPATA KATIBA ITAKAYOKATALIWA NA WANANCHI!!!!!
Hapa tunaongelea maoni ya Mzee Mtei, right?
 
Kwamba tume ina majina mengi ya kiislamu(kiarabu!) hiyo ni fact. Lakini wamechaguliwa kwa sababu ya majina yao au dini yao hilo ni debatable. Na kwa kweli ukiangalia sana ni majina ya wajumbe kutoka Zanzibar ndio yanayofanya hiyo tume ionekane ina waislamu wengi! Binafsi bado siamini kuwa waliochaguliwa wamechaguliwa kwa sababu ya dini au majina yao!
 
sio fare kumshambulia mzee huyu. tujiulize, alilosema ni kweli au laa? kama ni kweli, shida iko wapi? kwenye inchi inayoingiwa na tensions za kidini kama hii ni muhimu sana kuliangalia kwa makini wazo la mzee huyu. kwa vyovyote ameona mbali! hata hivyo ni muhimu kuwa makini na zito kabwe.

Kusema kwamba tume ina waislam wengi hapo ni kweli, na kimsingi hakuna mwenye tatizo na hili kuwa wako wengi
Tatizo ni maoni yake kwanini wako wengi, toka lini tumeanza kutumia kigezo cha dini?

Muulize Mtei CDM viti maalum kwanini wameteu wakristo wengi
Muulize kwanini uongozi CDM una wakristo wengi
Muulize kwanini wamemsimamisha Padri kugombea urais
Muulize kwanini kanisa mara zote lipo upande mmoja kimsimamo na CDM
Au muulize kwanini inadaiwa wakanda ya kaskazini wanajiona wanyechama

Majibu atakayo kujibu ndio hayo alitakiwa kutumia busara kutambua kwanini tume ile ina waislam wengi
Maana kimsingi maswali hayo yataulizwa tu na mtu anayeangalia mambo kwa mtazamo wa kidini na kikanda, vinginevyo maswali yote niliyataja hapo juu hayana mashiko kama maoni yake yasivyo na mashiko.

Nakuhakikishia tukianza na uwiano wa dini hatutaishia hapo......makabila na hadi koo zitaingia
FIKIRI MARAMBILI MKUU.......
 
Mie siliamini hilo Gazeti la JAMBO LEO..........Kwa kuwa ZITO NA MZEE MTEI, ni member humu JF, sichangii mpaka nipate kauli zao juu ya jambo hili............Maana mnaweza kutoa mapovu na kutafuna michanga kwa kushambuliana humu, mwisho wa siku unaiskia "MTU MMOJA AMBAYE HAKUTAKA KUTAJWA JINA LAKE AMEDAI KWAMBA MHE. ZITO AMESEMA KWAMBA MZEE MTEI AMEFILISIKA KIMAWAZO.................."
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Hapo ndiyo inabidi tukubali kuwa hii hoja ya kusema;"Tz watu hawaheshimu mawazo ya watu wengine".Iweje mtu atoe mawazo yake binafsi halafu wengine waanze kumshambilia tu bila kujali kama mtoa hoja amekiuka sheria yoyote.Haijalishi ni mawazo yasiyo na mashiko kiasi gani ilimradi mtu hajavunja sheria ni lazima tuyaheshimu.Kutokukubaliana na hoja ya mwenzie haitoi fursa ya kuanza kushambuliana.
Nadhani ilikuwa inatosha kusema yeye(zitto) hakubaliani na hoja ya mzee mtei na kutoa sababu zake,lakini kufikia hatua ya kusema kwamba eti mzee mtei amefilisika kimawazo naona kama hajamtendea haki.
 
Mkuu unajua ni kiasi gani tunavyo washambulia waislam humu ndani kwa kudai uwiano sawa kama anaodai Mtei
Unajua akina shekh Ponda na Baseleh tumeisha waita majina gani na kuwadhihaki kwa kiasigani kwa kutoa maoni kama aliyotoa Mtei
Who the hell is Mtei.......................for me Basaleh, shekh Ponda nawaweka daraja moja katika hili
 
jamani eeeh,mimi naona hakuna haja ya kumsakama huyo mzee mtei kwani aliyeleta siasa za udini katika nchi hii hamumfahamu?
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.
Source Jambo Leo ~ Habari Leo. Labda ungesema ama tweet tungekuelewa.
tangu juzi naona hawa ndio wanashughulika na hii habari.

Mwenye habari iliyo huru juu ya hili suala tafadhali atujuze

chama cha dini ya kikristo........chakosoa waislamu kuwemo kwenye tume......muislamu aliyeko kwenye chama hicho akosoa...! HEADING ILITAKIWA ISOMEKE HIVYO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom