Mtazamo wangu: CCM ipi ni safi kati ya hizi?

Siasa za Makundi zilizonogeshwa na Kile kilichoitwa "Kujivua Gamba Ili Kukinusuru Chama" sasa zimepelekea kutokea Makundi Makubwa ndani ya CCM yanayohatarisha Ustawi wa Chama hicho ( Tuendelee kuomba Mungu Kife Kabisa). Kwa Mtu anayefuatilia kwa Karibu Kabisa Mienendo na Minyukano ndani ya Chama Kicho Chenye Fikra zinazofanana Uzee wake ataona kwamba CCM sasa imegwanyika katika Makundi yafuatayo

1. CCM -Sitta: Hili ni lile kundi ambalo baada ya Kushindwa kanzisha CCJ sasa linaonekana kwamba linataka kuanzisha Chama ndani ya Chama. Hili ni kundi ambalo linajitahidi sana kutaka kuaminika kwa Watanzania kwamba ni Watakatifu ndani ya CCM. Nyuma ya kundi hili wamo akina Nape, Ole Sendeka, Kilango, Mwakyembe. Kundi hili linapambana kuhakikisha kwamba mwaka 2015 linafanikiwa kumpenyeza Mgombea wao wa Urais. Ni kundi ambalo limejaa wanafiki tukianzia na Samwel Sitta ambaye leo anaiita Kampuni ya Dowans aliyozima Mjadala wake Bungeni kuwa ni ya Kihuni. Huyu Babu ni Mnafiki anayeongozwa na Visasi vya Kuukosa Uwaziri Mkuu 2010. Ni kundi ambalo linaonekana kutumia Kujivua Gamba kama turufu ya kuwamaliza wabaya wao wa Kisiasa.

2. CCM-Lowasa: Hili ni lile kundi linaloamini kwamba Lowasa hakuwa na kosa katika kashfa ya Ricmond na kwamba Lowasa aliamua Kujitoa Sadaka ili kukiokoa Chama. Kundi hili linaona kwamba yule aliyejitoa Sadaka ili kukiokoa Chama dhidi ya Hasira ya wananchi sasa amekuwa Kafara. Ni kundi lenye Nguvu sana na Nguvu ya hili kundi ilidhihirika pale Lilipowazuia wale "Mitume" katika kundi la kwanza kukanyaga Igunga katika kipindi cha Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga. Ni Kundi ambalo linaamini kwamba Katika CCM hakuna aliye Msafi wa Kumyooshea Kidole Mwezake kwamba ni Fisadi. Ikumbukwe kwamba Lowasa anashutumiwa kwa Ishu ya Richmond pekee. Wachambuzi wa Mambo wanauliza kwamba Iweje IPTL iwe haramu lakini Richmond iwe Nongwa? Wanauliza vipi Kagoda, Deep Green , Meremeta, Tangold mbona Haziguswi? Kundi hili limeapa kufa na CCM

3. CCM-Membe. Hii ni CCM ambayo inategemea kudra na Huruma za Mwenyekiti, Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kundi hili liko kwenye Kundi la Kukosa maana kwa Sasa Mwenyekiti hana nguvu za kuamua nani awe Mgombea Uraisi. Ni Kundi ambalo linajaribu kujipendekeza zaidi katika Kundi la CCM-Sitta kama Fisi likingoja Mfupa Uanguke.

Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kwa Hali ilivyofikia ndani ya CCM ni Kudra za Mwenyezi Mungu zitakiwezesha chama hicho kikongwe kabisa Kupita salama katika Uchaguzi wa 2015

4-CCM-JF. Katika mtandao wa hapa jamii forums pia Makada wa CCM wametofautiana Kimtizamo na Kitu pekee kinachowaweka pamoja ni pale inapokuwa CCM against CDM.

4.1-CCM-Rostama: Hii ni CCM ambayo haitaki kusikia kwamba Rostam ni Gamba ni CCM ambayo kwao Rostam ni Role Model. Ni CCM inayoongozwa na Mwanamama FaizaFoxy na Malaria Sugu. Ni CCM ambayo imeapa kufa na Rostam

Raha ya dunia hii ni kuwa you can not by anyway obstruct someone's feelings......Tatizo kubwa ni kuwa binadamu ana upendo, upenzi na mapenzi kwa vitu ambavyo vinaweza kuwa nonsense kwa wengine.....ili ni tatizo kubwa. Binadamu ana uhuru wa kuchagua na ana uhuru wa kuficha jambo lake la moyoni.

CCM yeyote uliyotaja hapo juu ina wapenzi wao na sababu zao..kuna watu walimpigia kura mgombea ubunge wa UPDP kwani walimpenda ,ili hali kwe wengine alikuwa anaonekana mvuta bangi.

Kwa mtazamo wangu, CCM zote ulizosema kama ni CCM tu ni mbaya , na ubaya wa CCM ulianza tangu enzi za Nyerere..CCM haijawahi kuwa nzuri labda kama utataka kuipindisha historia. Ubaya wa uzuri wa CCM hakuondoia ukweli kuwa ni chama ambacho kipo madarakani kwa kuchaguliwa na wananchi hata kama ni watano tu!

Ili ku-convince ccm lovers kuwa ni chama kibaya , inatakiwa influential power ya kuwaondoa watu kutoka kwenye hiyo line...na huwa hawatukanwi bali kueleweshwa, ili lisipoeleweka vizuri. wapenzi wa CCM wataipenda tu na utakapowaita wajinga ndipo watakapozidisha MAPENZI YAO KWA CCM!!!
 
Hili suala la UVCCM kufungua Matawi Arusha limewatisha CCM-Sitta yaani hawa jamaa ndio wanajiona wao katika CCM ndio wanastahili kufungua Matawi. Very soon watasema kwamba hawayatambui hayo Matawi

Sio matawi, ni mashina yale yanakuwaga tu na vibendera. Ni kama vijiwe vya wakereketwa
 
Kwa kuwa umesema ni mtizamo then umemwag upupu mie nakucha na huo mtizamo wako maana ndiyo unavyo tizama .Endelea kuijadili CCM wewe.
 
politics is never short of cynicism and hypocrisy na hapa naona CCM sitta ni best-bora hypocrites wa kisiasa kuliko bora liende akina Membe au CCM-lowassa ya wanafiki wa kisiasa na wenye uchu wa madaraka na ukwapuaji wa hatari ya kuifilisi kabisa nchi akina RA na wenzake...
 
Siasa za Makundi zilizonogeshwa na Kile kilichoitwa "Kujivua Gamba Ili Kukinusuru Chama" sasa zimepelekea kutokea Makundi Makubwa ndani ya CCM yanayohatarisha Ustawi wa Chama hicho ( Tuendelee kuomba Mungu Kife Kabisa). Kwa Mtu anayefuatilia kwa Karibu Kabisa Mienendo na Minyukano ndani ya Chama Kicho Chenye Fikra zinazofanana Uzee wake ataona kwamba CCM sasa imegwanyika katika Makundi yafuatayo

1. CCM -Sitta: Hili ni lile kundi ambalo baada ya Kushindwa kanzisha CCJ sasa linaonekana kwamba linataka kuanzisha Chama ndani ya Chama. Hili ni kundi ambalo linajitahidi sana kutaka kuaminika kwa Watanzania kwamba ni Watakatifu ndani ya CCM. Nyuma ya kundi hili wamo akina Nape, Ole Sendeka, Kilango, Mwakyembe. Kundi hili linapambana kuhakikisha kwamba mwaka 2015 linafanikiwa kumpenyeza Mgombea wao wa Urais. Ni kundi ambalo limejaa wanafiki tukianzia na Samwel Sitta ambaye leo anaiita Kampuni ya Dowans aliyozima Mjadala wake Bungeni kuwa ni ya Kihuni. Huyu Babu ni Mnafiki anayeongozwa na Visasi vya Kuukosa Uwaziri Mkuu 2010. Ni kundi ambalo linaonekana kutumia Kujivua Gamba kama turufu ya kuwamaliza wabaya wao wa Kisiasa.

2. CCM-Lowasa: Hili ni lile kundi linaloamini kwamba Lowasa hakuwa na kosa katika kashfa ya Ricmond na kwamba Lowasa aliamua Kujitoa Sadaka ili kukiokoa Chama. Kundi hili linaona kwamba yule aliyejitoa Sadaka ili kukiokoa Chama dhidi ya Hasira ya wananchi sasa amekuwa Kafara. Ni kundi lenye Nguvu sana na Nguvu ya hili kundi ilidhihirika pale Lilipowazuia wale "Mitume" katika kundi la kwanza kukanyaga Igunga katika kipindi cha Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Igunga. Ni Kundi ambalo linaamini kwamba Katika CCM hakuna aliye Msafi wa Kumyooshea Kidole Mwezake kwamba ni Fisadi. Ikumbukwe kwamba Lowasa anashutumiwa kwa Ishu ya Richmond pekee. Wachambuzi wa Mambo wanauliza kwamba Iweje IPTL iwe haramu lakini Richmond iwe Nongwa? Wanauliza vipi Kagoda, Deep Green , Meremeta, Tangold mbona Haziguswi? Kundi hili limeapa kufa na CCM

3. CCM-Membe. Hii ni CCM ambayo inategemea kudra na Huruma za Mwenyekiti, Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kundi hili liko kwenye Kundi la Kukosa maana kwa Sasa Mwenyekiti hana nguvu za kuamua nani awe Mgombea Uraisi. Ni Kundi ambalo linajaribu kujipendekeza zaidi katika Kundi la CCM-Sitta kama Fisi likingoja Mfupa Uanguke.

Wachambuzi wa Mambo wanasema kwamba Kwa Hali ilivyofikia ndani ya CCM ni Kudra za Mwenyezi Mungu zitakiwezesha chama hicho kikongwe kabisa Kupita salama katika Uchaguzi wa 2015

4-CCM-JF. Katika mtandao wa hapa jamii forums pia Makada wa CCM wametofautiana Kimtizamo na Kitu pekee kinachowaweka pamoja ni pale inapokuwa CCM against CDM.

4.1-CCM-Rostama: Hii ni CCM ambayo haitaki kusikia kwamba Rostam ni Gamba ni CCM ambayo kwao Rostam ni Role Model. Ni CCM inayoongozwa na Mwanamama FaizaFoxy na Malaria Sugu. Ni CCM ambayo imeapa kufa na Rostam
Kama vile uchambuzi ulikuwa bado unaendelea eeenh? Umekatika ghafla kama unavyokatika umeme wa Tanesco! Endelea kuchambua kama 'Karanga'. Kisha usichoke! Utuchambualie na CDM, CUF......n.k.
 
wana jf,mtu kama sendeka au kilango malecela sio watu wa kusema eti ni wapiganaji,wanampigania nani kama sio matumbo yao? Kma sendeka jimbo lake mwenyewe ameshindwa kufanya maendeleo siasa za upiganaji ndo ataweza? Kama ameweza kuwatelekeza watoto wake wa kuzaa hata hapo kwenye upiganaji si atakuwa mnafiki tu? Amejichimbia Bwawa kwa ajili ya ng'ombe zake lakini kutafuta maji salama kwa ajili ya wana wa simanjiro hakuna,amebaki kuendeleza siasa za mvutano kati yake na existing NGO's kama vile ILARAMATAK LORKONEREI. Ningekuwa mchungaji ningesema shindwa CCM shindwa!!!! Na wote tuseme shindwa

CCM haina mpiganaji wala nini wote wamefyata katika kutafuta tumbo street,waache kudanganya watanzania kywa wao ni wapiganaji,hao ndio wapiganaji koko.
 
Back
Top Bottom