MTAZAMO WA MZANZIBARI KWA NCHI YAKE; Muungano wa mkataba ndio dira yetu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
ZANZIBAR DAIMA

MTAZAMO WA MZANZIBARI KWA NCHI YAKE

MENU

SKIP TO CONTENT




Mwakilishi wa Kiembesamaki na Waziri wa SMZ, Mansour Yusuf Himid


Nafikiria wengi tumeyasikia maneno ya Mheshimiwa Mansour Yusuf Himid, mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki na waziri mwandimizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nataka kwanza kumpongeza kaka yetu Mansour kwa ujasiri wake na mapenzi yake kwa Zanzibar na kwa Tanzania kiujumla.

Mheshimiwa Mansour amegusia suala muhimu katika mustakabali wa Muungano wetu, na ametuonyesha kwamba CCM ipo tayari kusikiliza maoni ya Wazanzibari juu ya mfumo gani wanaoutaka wa Muungano wa Tanzania.

Ameeleza kinagaubaga kwamba muungano unawezekana kuendelea katika mfumo mpya wa mkataba baina ya nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar kama vile muungano wa nchi za Ulaya.


Mheshimiwa Mansour hakumalizia hapo tu, bali amechambuwa kwamba katika dunia ya sasa ya utandawazi ni muhimu kujuwa kwamba muungano wa nchi mbili unawezekana ukaimarika zaidi bila ya nchi moja kupoteza utambulisho, uraia wala asli yake.


Akamalizia kwa kusema kwamba Zanzibar inaweza kufarajika zaidi katika mfumo mpya wa maelewano mazuri zaidi na Tanganyika katika mfumo wa kimkataba, huku baadhi ya sekta za serikali zikibakia ndani ya uongozi wa serikali husika na baadhi kubakia katika mikono muungano.


Aligusia pia kuhusu kiti cha Zanzibar kwenye Umoja wa Mataifa, kwamba tunaweza kurejesha kiti chetu bila ya kuvunja Muungano wa udugu baina yetu na Tanganyika katika mfumo huo mpya.

Kikwete, Seif na Karume wanastahiki sifa



Rais Jakaya Kikwete


Serikali ya Mheshimwa Dr. Jakaya Kikwete imejitahidi sana kuondosha zile kadhia za kukandamiza wananchi, na binafsi nampongeza Rais Kikwete kwa kuwa muwazi na mpenda demokrasia ya kweli. Wale wengi waliomsikiliza katika hotuba yake ya mwanzo tangu kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, watakumbuka kwamba alisisitiza kulisimamia suala la Zanzibar na kuhakikisha migogoro yote baina ya wanasiasa inamalizika na hata migogoro ya Muungano.


Tuanze na kuangalia namna gani hakuingilia muundo wa katiba mpya ya Zanzibar na namna gani amewaachia Wazanzibari kuamua nini wanachokitaka katika muundo wa serikali mpya. Haya maneno ya CHADEMA kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, ni kwa sababu ya mtazamo na msimamo wake juu ya Tanzania mpya yenye uhuru zaidi na Zanzibar mpya yenye nafasi inayoridhiwa na wananchi katika masuala ya muungano.


Wazanzibari tuwashukuru sana Dr. Amani Karume kwa kuweka msingi madhubuti wa serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na Maalim Seif kwa jitihada zao katika kuondosha dosari zilizodumu kwa takriban miaka 20.


Kukubali kuondowa tafauti zao za kisiasa na kukaa pamoja kushirikiana pole pole kuendeleza gurudumu la maendeleo ya nchi kumepelekea nchi kurejea katika hali ya utulivu na amani ambayo yapaswa kudumishwa.

Rais Shein na Makamo wake, Maalim Seif, ndio kikatiba na kidemokraisia waliopewa dhamana na asilimia 98 ya wananchi kuliongoza taifa hili la Zanzibar kwa kile wananchokiamini kuwa ndicho chenye maslahi mazuri zaidi kwa nchi.


Masuala ya uongozi hayataki wakuu wa nchi kufuata mada zinazopendwa sana tu na watu, bali ni kile wanachokiamini kuwa na maslahi kwa wananchi na taifa kwa jumla. Wananchi walio wengi ndio waliowapa haki ya mwisho ya maamuzi yao bila ya upinzani.


Anayekufa kwa sukari, hana haja ya kupewa sumu



Amani Karume (kushoto), Maalim Seif (kulia) mashujaa wa Zanzibar.


Kama kuna watu baina yetu wanaoamini kwamba serikali haipo sawa katika masuala fulani, kwa mfano ya kura ya maoni, basi njia iliyo madhubuti ya kupinga maamuzi ya serikali ni kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia katika uchaguzi unaofuata kwa kuenda kinyume na masharti ya wapiga kura wao.


Masuala ya kura ya maoni yanaweza kukubalika au kukataliwa na serikali bila ya serikali kuwajibika, kwa sababu ya ile idhini ya kura walizoshinda katika uchaguzi mkuu.


Mifano ipo tele katika nchi zilizojengwa katika misingi ya demokrasia kuliko Tanzania, mfano Uingereza ambako wananchi wengi kwa miaka wamekuwa wakililia kura ya maoni ya kuitoa katika Umoja wa Ulaya huku serikali zote tokea ya Labour na hadi sasa ya Conservative na LibDems kuwa wawazi kwamba hawako tayari kuwapa wananchi haki yao hiyo kwa sababu kubwa kwamba hilo halikuwa katika manifesto ya chama kabla ya uchaguzi na wananchi walijuwa hilo mapema na still wakawachagua.

Maombi yangu kwa sasa kwa jamii ya Wazanzibari kukaa chini na kutafakari njia mpya za kuimeguwa Zanzibar katika mfumo wa sasa potofu wa Muungano kwa kutoa masharti mapya ya namna gani muungano uendeshwe na kwa mfumo wa aina gani.


Kama lengo kuirejesha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, basi katika mfumo wa mkataba tunaweza kuirejesha serikali iliyohuru na kutambulika kama nchi kamili huku tukifaidika na muungano mpya uliojengwa kwa misingi ya usawa na umoja wa kimaendeleo. Tukumbuke Wazanzibari kwamba umoja wetu ndio msingi wa maendeleo makubwa ya visiwa hivi.


Tuangalie ugumu wa kura ya maoni katika mifano ifuatayo: kwanza, katika daftari la wapiga kura, wanaostahili kupiga kura ya maoni ni watu wasiozidi laki sita kwa Zanzibar yote. Takwimu kutoka Bara zinaonyesha kwamba Dar es Salaam peke yake kuna Wazanzibari 350,000. Je, Tanzania nzima?


Dhana kubwa inayowahofisha viongozi wa serikali juu ya kura ya maoni ni kwamba jee ikiwa 30% ya Wazanzibari wanaoishi Zanzibar wataukubali muungano wa sasa au wa serikali moja wakiungwa mkono na Wazanzibari laki tatu na nusu kutoka Bara, kweli kutakuwa na Zanzibar huru? Au kukiwa na matokeo ya kati na kati bila ya majibu sahihi itakuwaje?


Tukumbuke kwamba asilimia karibu 40 ya Wazanzibari waliyapinga Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya 2010. Sasa ikiwa watajumuika na Wazanzibari waishio Bara itakuwaje?

Kwa upande wa upinzani, mazingatio yao makubwa yalilenga katika Tume ya Uchaguzi ambayo imekuwa ikiilalamikia kwa miaka zaidi ya ishirini kuwa haitendi haki, wakitathmini kwamba matokeo pia yakitangazwa kinyume na matarajio yao itakuwa na athari gani kwa Zanzibar mpya?


Muungano wa Mkataba ndio suluhisho



Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume.


Suluhisho kubwa lililowafikiwa kwa wote ni kuwaachia wananchi kutoa maoni ya mfumo upi wanautaka na serikali kulinda maamuzi ya wananchi hao na ndio maana kura ya maoni ya kuwepo au kutokuwepo kwa Muungano imekuwa ngumu kupitishwa na wanasiasa wengi wa visiwani kwa hofu hiyo.

Katika mfumo mpya wa mkataba, Zanzibar itaweza kurejesha mamlaka yake iliyoyapoteza tokea kuunganika na Tanganyika na Zanzibar, huku Muungano ukilenga masuala ya kiserikali yasiyoingilia uhuru wa kitaifa au maamuzi ya maslahi ya taifa la Wazanzibari.


Ndio tukasema katika mfumo huu wa mkataba kila Mzanzibari ni mshindi, kwa wapenda muungano (wale asilimia 40 Zanzibar na Wazanzibari wanaoishi Tanzania
Bara) hawatakuwa na ile khofu ya kupoteza mali zao walizozichuma kwa jasho lao.

Wale wanaopendezewa kurejea kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanza, basi pia kiu yao itakuwa imepatiwa ufumbuzi, kwani muungano wa kimkataba hauondoshi utaifa wa nchi zilizoungana.


Na mwisho wasioutaka Muungano kabisa watakuwa na haki ya kuukataa kata kata katika kura ya maoni kwa yale yaliyopendekezwa kuwamo katika muungano au katika chaguzi zijazo.

Wazanzibari tusahau tafauti zetu na tuachane na masuala ya wapi asili zetu zimetokea. Tukae pamoja kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuirejesha Zanzibar katika ramani ya kimataifa.


Kubakia kwa muungano kunawezekana bila ya kupoteza utaifa wetu. Tutapokaa tukabishana na kupigana miongoni mwetu, basi ni sawa na vita vya panzi faida kwa kunguru.


Hivi tutathmini kwamba kura ya maoni ndio njia pekee ya kuirejesha Zanzibar katika mamlaka ya uhuru pekee? Ikiwa njia hii imeweza kutumiwa kuwagonganisha Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe, jee ni hekima kushikilia msimamo huo huku tukijuwa inaweza kuwagawa Wazanzibari katika makundi yatayoimega Zanzibar kidogo kidogo?


Kama ipo njia mbadala, kwa nini tusitumie kuleta msimamo mmoja wa Wazanzibari wote? Hebu tukae chini tufikiri kwani kura ya maoni hazijapigwa tokea mwaka 1995 mpaka 2000 na jee matokeo hayajulikani? Tafauti gani ya miaka ya nyuma na sasa wakati mfumo ndio ule ule?


Tufikiri namna gani Scotland imeweka mikakati ya kushinda kura ya maoni yao: kwanza, imepangwa kupigwa katika mwaka 2014 kwa sababu ndio historia ya Scotland ya kujitenga inapokuwa muhimu. Jengine ni kuhakikisha hata wale wenye miaka 16 wanapiga kura kwa sababu wanajuwa vijana wengi ndio wanaunga mkono kujitenga kwao.


Kwa sisi Wazanzibari, nini mkakati wetu katika kura ya maoni? Je, haitakuja kututia shimoni zaidi ikiwa Tume itaamua kutangaza matokeo yasiyo sahihi? Au tuseme haya masuala ninayoyauliza ni ndoto zaidi kuliko ukweli ulivyo?


Kama wametupa hadidu rejea katika kujadili katiba mpya wakisistiza kujadili kuvunja Muungano ni kosa la jinai, basi kwa nini tushindane nao kimaguvu wakati nafasi na sisi tunayo ya kuwapa hadidu rejea zetu ya namna gani mfumo mpya wa Muungano tunaoutaka? Hivi sote tukisema tunataka muungano wa kimkataba wenye lengo la kuirejesha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, hatutafaidika na Umoja wetu? Akushindae kwa matonge mshinde kwa kutoelea.


Mwandishi: Foum/Mzalendo.Net


Mhariri: Zanzibar Daima




 
Hii ni story ya Mwezi uliopita lakini ina Umaana... Wazanzibari kama ni Muungano wangependa Muungano wa Shirikisho

na sio Muungano wa Kikatiba; And they Highly rate Pres Kikwete kwasababu haingilii masuala ya Zanzibar, anaiachia

Serikali ya Zanzibar iyatekeleze...

SIO DHAIFU HATA KIDOGO WAO WANAVYOONA...
 
Akamalizia kwa kusema kwamba Zanzibar inaweza kufarajika zaidi katika mfumo mpya wa maelewano mazuri zaidi na Tanganyika katika mfumo wa kimkataba, huku baadhi ya sekta za serikali zikibakia ndani ya uongozi wa serikali husika na baadhi kubakia katika mikono muungano.
Hicho ndio kitu kile kile tulichonacho sasa hivi!

Viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla tuna matatizo makubwa sana ya kujieleza kwa lugha yetu hii ya Kiswahili, ndio maana wanasiasa hawaeleweki. Sasa hivi kwenye Muungano kuna Mkataba na kuna mambo ambayo sio ya Muungano na kuna mambo ambayo ni ya pamoja. Sasa katika hayo yanayoelezwa hapo juu ya mfumo "mpya" ni yepi mapya hapo?

Kama tunataka kuiga mfumo wa European Union basi tujue kule hakuna jambo la pamoja linaloshughuliwa na "serikali ya Muungano." Nasema tena, Europe hakuna Muungano wa serikali. Europe hakuna Muungano period. Europe kuna "Umoja."

Ukisikia muungano wa sarafu ya Euro au Visa ya Schengen ha Ulaya usidhani kuna serikali ina process Schengen Visa, unapoomba Visa unatuma maomba specific kwa nchi ile unayotaka kwenda. Ukisikia Muungano wa sarafu Europe usidhani kuna wizara ya fedha ya Muungano. Kiserikali kila mtu la lwake. Kila nchi ni dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Na hapa kwetu hivyo hivyo ndivyo tunavyotaka iwe, kila upande uwe ni dola huru yenye mamlaka yake kamili.
 
Huyo Mwakilishi Mansour Yusuf Himid ambaye ana udugu na Amani Karume na elimu ya Form 4 tu, na anawageuza Mawaziri wenzake wengi wa kiume mfano yule aliekuwa wa Uchukuzi ambae rasmi ndie Basha wake. Wizi wa Ardhi uliokidhiri alipokuwa ndie waziri wake, sasa hivi wanashikana mashati Aga Khan na Kempinski Hotel ya bwana Bawardi wa Dubai, hawa wawili waliuziwa ufukwe wa Mji Mkongwe majengo yote ya Serikali ya Registrar, na hili dili limefanywa chap chap kwenye dakika za majeruhi kati ya Amani Karume na Shemeji Mansour, haya na mengine mengi yalisababisha Wazanzibari wengi na sio Wakristo wa Zanzibar (sisi) ambao makaburi yao yamegeuzwa mahoteli ya Dr Karume, misemo kuwa wakitoka tu madarakani hawa WATONYONGWA au japo kufilisiwa dhulma zote, ndipo wakalazima kutafuta kujinasua eti kuunganisha vyama Zanzibar ili ipatikane serikali ya wote ili wote wapate kula, ikumbukwe jitihada za Karume na wenzake za yeye Karume kuongezewa muda kwa kisingizio aendeshe kwa muda kwanza serikali ya mseto ila wakashindwa kwa amri toka Dodoma, hapo ndipo choko choko za kujuta kuwa na chama kimoja na bara yakawa ndio malalamiko. Hakuna Ufisadi kama wa Zanzibar duniani
 
Hicho ndio kitu kile kile tulichonacho sasa hivi!

Viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla tuna matatizo makubwa sana ya kujieleza kwa lugha yetu hii ya Kiswahili, ndio maana wanasiasa hawaeleweki. Sasa hivi kwenye Muungano kuna Mkataba na kuna mambo ambayo sio ya Muungano na kuna mambo ambayo ni ya pamoja. Sasa katika hayo yanayoelezwa hapo juu ya mfumo "mpya" ni yepi mapya hapo?

Kama tunataka kuiga mfumo wa European Union basi tujue kule hakuna jambo la pamoja linaloshughuliwa na "serikali ya Muungano." Nasema tena, Europe hakuna Muungano wa serikali. Europe hakuna Muungano period. Europe kuna "Umoja."

Ukisikia muungano wa sarafu ya Euro au Visa ya Schengen ha Ulaya usidhani kuna serikali ina process Schengen Visa, unapoomba Visa unatuma maomba specific kwa nchi ile unayotaka kwenda. Ukisikia Muungano wa sarafu Europe usidhani kuna wizara ya fedha ya Muungano. Kiserikali kila mtu la lwake. Kila nchi ni dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Na hapa kwetu hivyo hivyo ndivyo tunavyotaka iwe, kila upande uwe ni dola huru yenye mamlaka yake kamili.

Taso,

..nakubaliana na wewe 100% kwamba Europe hakuna muungano. pia kuna mapendekezo mapya kwamba tuwe kama Swiss.

..kwa upande mwingine, viongozi/wanasiasa wa Zanzibar ni kati ya hao wa-Zanzibari 350,000 wanaoishi Dar-Es-Salaam. Viongozi/wanasiasa wengi sana wa Zanzibar wamewekeza huku Tanganyika. Nilikuwa naangalia listi ya wananchi waliogawiwa viwanja kigamboni nikakuta jina la Balozi Seif Iddi, makamu wa pili wa raisi wa Znz. Alhaj Aboud Jumbe amejibana kigamboni tangu atimuliwe ktk uongozi. Hiyo ni mifano michache tu.

..sasa mazingira hayo ndiyo yanayowafanya wanasiasa wa Zanzibar wawe njia panda ktk suala la kura ya maoni na kuupinga muungano ktk ujumla wake. ndiyo maana unasikia hizi "sitaki-nataka" za kuvunja muungano, na kuleta "muungano wa mkataba."

..kwa mtizamo wangu, watu wachague MALI au UZANZIBARI. wale wote walioko Tanganyika wapewe nafasi ya kuwa raia wetu, asiyetaka arudi kwao Zanzibar. Baada ya hapo, kila nchi ijitegemee kwa kila kitu. Kama tutapenda kusaini mkataba wowote ule ni vizuri ukawa multilateral, na zaidi uwe umepitishwa ktk jumuiya kama EAC au SADC.
 
taso,

..nakubaliana na wewe 100% kwamba europe hakuna muungano. Pia kuna mapendekezo mapya kwamba tuwe kama swiss.

..kwa upande mwingine, viongozi/wanasiasa wa zanzibar ni kati ya hao wa-zanzibari 350,000 wanaoishi dar-es-salaam. Viongozi/wanasiasa wengi sana wa zanzibar wamewekeza huku tanganyika. Nilikuwa naangalia listi ya wananchi waliogawiwa viwanja kigamboni nikakuta jina la balozi seif iddi, makamu wa pili wa raisi wa znz. Alhaj aboud jumbe amejibana kigamboni tangu atimuliwe ktk uongozi. Hiyo ni mifano michache tu.

..sasa mazingira hayo ndiyo yanayowafanya wanasiasa wa zanzibar wawe njia panda ktk suala la kura ya maoni na kuupinga muungano ktk ujumla wake. Ndiyo maana unasikia hizi "sitaki-nataka" za kuvunja muungano, na kuleta "muungano wa mkataba."

..kwa mtizamo wangu, watu wachague mali au uzanzibari. wale wote walioko tanganyika wapewe nafasi ya kuwa raia wetu, asiyetaka arudi kwao zanzibar. Baada ya hapo, kila nchi ijitegemee kwa kila kitu. Kama tutapenda kusaini mkataba wowote ule ni vizuri ukawa multilateral, na zaidi uwe umepitishwa ktk jumuiya kama eac au sadc.

mkuu hapo kwenye red kwa maoni yangu sitapenda wapewe nafasi wao kuamua wapi wanataka kuishi kama wakiamua kuuvunja muungano na wao warudi kwao zanzibar wakaijenge nchi yao kwa pamoja wakibakia huku bado kutakuwa kuna chokochoko woote warudi kwao kama walivyofanywa south sudan wengi walipoteza kazi zao kwa kurudishwa kwao. Tuachane kwa amani full na sio vipande vipande walioolewa bara ndio watakuwa wanahaki ya kubakia tu.
 
mkuu hapo kwenye red kwa maoni yangu sitapenda wapewe nafasi wao kuamua wapi wanataka kuishi kama wakiamua kuuvunja muungano na wao warudi kwao zanzibar wakaijenge nchi yao kwa pamoja wakibakia huku bado kutakuwa kuna chokochoko woote warudi kwao kama walivyofanywa south sudan wengi walipoteza kazi zao kwa kurudishwa kwao. Tuachane kwa amani full na sio vipande vipande walioolewa bara ndio watakuwa wanahaki ya kubakia tu.

UKI,

..I know how u feel about this, and how tempting it is kuchukua hatua ulizopendekeza.

..tatizo ni kwamba walioko huku Tanganyika wanapenda muungano--wanafaidika nao.

..hawa siyo wale wanaoulaani muungano, na kuzusha tuhuma za ajabu-ajabu dhidi ya wa-Tanganyika.

..hivi unafikiri mtu kama Bakhresa anataka kurudi Zanzibar na kupoteza baadhi ya mali zake huku Tanganyika?

..pia suala hili halipaswi kuamuliwa kwa hasira, kisasi, au nia ya kukomoana. wa-Tanganyika tunapaswa kutumia busara na ustaarabu ktk kushughulikia suala hili.
 
UKI,

..I know how u feel about this, and how tempting it is kuchukua hatua ulizopendekeza.

..tatizo ni kwamba walioko huku Tanganyika wanapenda muungano--wanafaidika nao.

..hawa siyo wale wanaoulaani muungano, na kuzusha tuhuma za ajabu-ajabu dhidi ya wa-Tanganyika.

..hivi unafikiri mtu kama Bakhresa anataka kurudi Zanzibar na kupoteza baadhi ya mali zake huku Tanganyika?

..pia suala hili halipaswi kuamuliwa kwa hasira, kisasi, au nia ya kukomoana. wa-Tanganyika tunapaswa kutumia busara na ustaarabu ktk kushughulikia suala hili.

mkuu tukitazama kwa upande wa pili ni nani ambae anataka kumkomoa mwenzake watanganyika unajua tulivyo wapole ki ukweli tungekuwa kama wazanzibar mpaka muda huu kusingekalika maana tumetukanwa sana kuonekana tunawaona kama wao ni watumwa suala la kurudi kwao wao wenyewe walikuwa wameshaweka vitisho kuanzia kwa watanzania bara wanaoishi huko na kufanya kazi huko kuwa wasifanye kazi katika idara za utalii na mahotelini huko suala hilo liliingia hadi kwenye baraza la mapinduzi la zanzibar bahati nzuri sikumbuki ni kiongozi gani alilitolea ufafanuzi mzuri wakaelewa ila wengi walikuwa tayari hawataki wabara wafanye kazi huko sasa hapo ni nani mwenye kisasi na mwenzake suala la mwenye viwanda huku ataendelea kufanya kazi zake ila ataitwa mwekezaji wa kigeni na sheria itakayotumika kwake ni kama mwekezaji wa kigeni wengine ambao hawana kazi maalumu au kazi ambazo zinawezwa kufanywa na watanganyika warudi kwa usalama tu na walioajiriwa serikali au mashirika binafsi wafuate utaratibu kama wageni kutoka nchi ya jirani zetu na wawe na work permit kwa mtindo huo tutaenda vizuri na tutaheshimiana hapa sidhani kama kutakuwa kuna kukomoana ila tukisema haki haki ipatikane kwa usawa na sio mwingine awe na kipaumbele zaidi kuliko mwingine kwa hilo kwakweli si busara tunataka tusibaki na manung'uniko yoyote awe mtanganyika au mzanzibar na hata wabara walioko huko wafuate utaratibu unaostahili kutokana na sheria za zanzibar. najua walioko huku hawapendi kuvunjika muungano kwa maslahi yao kwa sababu wamewekeza vya kutosha bara ila ni nani mwenye maamuzi zaidi ya kura ya maoni ya wananchi? waache wapige kura waamue suala la kutukanwa kila aina la tusi sioni kama ni busara zaidi ya kupandikiza chuki la lawama baadae hiyo sio haki kabisa aisee let them go pleaseeeeeeeeeeee!!!!!!!
 
Mimi nafikiiri waZnz wapo wazi kabisaaaaaaaaaaaa katika huo muungano wenu. Tatizo lipo kwa waDanganyika ambao wapo mguu ndani mguu nje. hawajui walitakalo.Kama wabara wote wataungana na kupaza sauti zao kama wanavyofanya waZnz pasi na shaka yoyote mambo yatakuwa shwari.

Mimi nashauri hii mliyonayo ndio fursa adhimu sana ya kutunga katiba mpya kueleza concernj zenu badala ya kulalamikia hapa JF. Mimi naamini kama wabara wata acha unafiki na kuwa wakweli katika suala la muungano basi kuna mengi sana maovu yatapungua na kuondosha malalamiko, dhulma na kejeli zote zinazotokea sasa kuhusu muungano wenu.

Tumieni mabadiliko ya Katika yenu kueleza nini mnachotaka katika muungano wenu.
 
Back
Top Bottom