Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Pamoja na kutumia gharama kubwa na pesa nyingi za walipa kodi wa nchi hii. Mwenge una madhara makubwa kwa jamii hasa katika suala la maambukizi ya ukimwi. Katika vijiji ambavyo mwenge unapolazwa huwa kuna matukio mengi ya ngono nzembe kutokana na wakimbiza mwenge kuchangamkia wanawake katika vijiji hivyo. Sasa hapa tujiulize, mwenge huu hulala vijiji vingapi tangu unapowashwa mpaka unapozimwa. Nimewahi kukimbiza mwenge katika wilaya ya Manyoni. Hali ilikuwa mbaya sana, kila mtu aliona ufahari kulala na mwanamke katika vijiji ambavyo mwenge ulilala. Naona mwenge umepitwa na wakati. Ni nini faida yake kwa sasa?