Mtatiro unapoteza muda CUF...karibu CHADEMA!

Changieni mada acha kukosoa mada.
Hapa ndo unajua nani ni nani.
ikiona hivyo ujue kilicholetwa jamvini ni cha kipumbavu bora kingekuwa cha kijinga ,hakina maana ,leta issues ya maana kuliko kuleta hisia .
uwanja wa ndege mwanza umejaa maji

 
ukisoma gazeti la mtanzania ya leo limeelezea mambo mengi kuhusu itatiro. Lakini kubwa zaidi ni hili la kutaka kuiendesha cuf kichadema zaidi. Mfano wanasema alishauri lipumba asiende siku ya kuapishwa kikwete na hata alishauri cuf watoke nje siku ya kupitishwa mswada wa katiba.

Hata mapendekezo ya kubadili mswada ambao umeshangiliwa sana na cuf yametoka kwake.

Mnakumbuka msimamo wake hapa jf kuhusu mswada ulikuwa tofauti sana na msimamo waliouchukua cuf. Kwa hali hiyo namshauri ajiunge tu chadema. Na gazeti limeeleza kuwa alimwandikia lipumba msg kusema kuwa cuf hakiwezi kumfikisha mahali anapotaka na lipumba akampa unaibu ili asiondoke.

Namshauri asiendelee kukaa kwenye chama ambacho yeye mwenyewe hashabihiani na malengo na itikadi yake. Viongozi wa cuf wanamlalamikia kama pandikizi la chadema ndani ya cuf , si maneno yangu ila gazeti hilo

pombe za weekend
 
He is a right person at the wrong Place, lets advise him to go where he deserve to be and thats no where more than CDM where true freedom fighters are, where people with vision to take Danganyika are
 
ITATIRO........................ULIMAANISHA gUTRAM iTATIRO MBUNGE WA ZAMANI WA ULANGA ?
 
Baada ya Faustin Sungura kujikomba jana kwenye mdahalo akikandia hoja ya haki ya kuandamana kwa sababu anazozijua mwenyewe, aliinuka kamanda Julius Mtatiro na kusema kwa ujasiri mkubwa kile Sungura alichoshindwa kusema tena akiwa amepoteza ujasiri kabisa. Wachambuzi wa public speaking mtaona wazi kabisa kuwa Sungura alikuwa akisema kana kwamba ameambiwa ukisema tofauti na haya umekwisha. Hakusema toka nafsini mwake bali out of pressure. Mtatiro alitetea demokrasia akijua wazi kuwa kama leo mtu mmoja amefanyiwa vile, basi kesho kuna mwingine aweza kufanyiwa vibaya zaidi na kumkanushia moja kwa moja mjeshi aliyemwakilisha Mkuu wa majeshi.

Tangu siku nyingi niliwahi kuwaambia baadhi ya vijana kuwa Mtatiro ni mwanasiasa mzuri ila nahisi yuko choo cha kike. Mifano inayoonyesha ni cha kike ni kauli ya mwenyekiti wake kufanya kampeni za waziwazi msikitini hivi karibuni na picha zake kupostiwa UTube na yeye kushindwa kukanusha.

Nadhani Mtatiro hujachelewa, msimamo wako tunaufahamu, wewe bado ni kijana...unangoja nini huko CUF? Toka ndugu yangu toka ukaungane na wapambanaji wenzako mkomboe nchi hii toka kwenye mikono ya mabeberu.
 
hata mimi nilikuwa nakiwaza sana hicho kitu kuwa ni kwa nini mtatiro yuko ccm B anafanya nini wakati vijana wenzake tuko chadema mtatiro mura si uje chadema alafu huyu jamaa ni mkurya au ni kabila gani kwa sababu haya majina ya mtatiro ni ya kwetu pare tarime mura thoka uko mura njoo chadema na ungekuwa uku wetu ungekuwa mubhunge haya kaka hizo ni changa moto unaweza zifanyia kazi

hata mimi nimemshauri sana ahame huko cuf, ambayo inatuhumiwa kuwa ni ccm b.
 
Mimi ni mmoja wa Watanzania ninayeamini kwamba Naibu katibu mkuu wa CUF ndugu Julius Mtatiro ana influence kubwa kisiasa tatizo hana jukwaa la kusimamia ndani ya chama dhaifu cha CUF japo simjui kiundani(wadau mtamchambua). Naamini Bwana Mtatiro anapoteza tu muda kwa kuwepo kwenye chama kinachopoteza umaarufu kila uchao kwa kitendo chao cha kufunga ndoa na CCM.Mfumo wa vyama vingi sio tu mwanzo wa mabadiliko ya kweli, bali vyama makini ndio mwanzo cha mabadiliko ya kweli yenye tija kwa taifa.Viko wapi NCCR,UDP,TLP n.k., yale matusi ya vyama vya msimu toka CCM hayajawagusa kwa sababu tu wao ni matawi ya CCM. Tanzania kuna chama kimoja tu cha upinzani. Ndugu Mtatiro, CHADEMA:A S 103: ndio chama sahihi kwa ndoto zako za kisiasa. Tafakari..Usipoteze muda..Fanya Maamuzi!
huyu jama namkubali sana, msimamo wake kuhusu mikopo wa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2006-2008 ulitusaidia walio wengu kusoma pale udsm. ni mwana mapinduzi halisi.., maana jamaa aliwahi kukesha pale nje ya bodi akishinikiza tupewe mikopo na tukapata kweli.

baada ya kumaliza chuo alikuwa mwanachadema, japo sina uhakika sana kama kadi alikuwa nayo, lakin alishiriki harakati za chadema, aliomba nafasi pale makao makuu viongoz hawakumpatia nafasi wakidai asubiri kwanza akomae katika chama..

cuf kwa kujua how potential he was at udsm, wakamnyakua na kumpa ukurugenz wa haki za binadam. mpaka saiv amefikia hapo alipo.

alijiunga cuf kwa sababu aliona chadema hawakujali umuhimu wake kwa wakati ule, ila kimsingi anaikubali chadema kama first choice, basi tu njaa zilimpeleka chadema.
 
Aje CDM alaf utamlipia kod ? Mwache apambane huko huko kwanza, pakmshinda atarud... ila ni kat ya vijana wachache saana wa CUF ( pamoja na mh. MAGDALENA SAKAYA)wenye uwezo wa hal ya juu, katika kujenga hoja zenye maslah ya taifa, bila kumsifia mkoloni.. BIG UP JEMBE MTATIRO.
 
By MAYOO
Binafsi namheshimu huyu jamaa kwani alikuwa mpiganaji mzuri wa haki wakati tuko udsm. Nakusihi angalia tz inakoelekea ndugu yangu ndo hiyo uliyokuwa ukiiota ktk maisha yako? Mbona watu wa mara si wanafiki, hawapendi wanakuambia, uking'ang'ania kama nyambali wanaku-displini, iweje kaka upoteze muda wako huko ccm b? Hao cuf wamekuweka ili kujisafisha na udini tu.

Unamainisha ni kama vile alivyoekwa pro.Safari na Chadema ili kujisafisha na udini?

Hujielewi wewe!!
 
Ni suala la muda tu, Julius Mtatiro, Magdalena Sakaya au Buruhani Bwegie ipo siku watahama au watafukuzwa CUF. Wapi watakwenda, kila mtu anajua!!
 
Tatizo CUF walishafunga ndoa na SSM sasa naye kama kiongozi si alikubali ndoa!!! Apewe kwanza talaka au akaombe talaka tatu ndipo apeleke maombi kwa chama cha kizalendo!!! Maombi yatafikiriwa na kupitiwa kwa kina isije ikawa ni pandikizi kama Shibuda!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom