Mtatiro: Kuna njama zinapangwa ili wajumbe wa bunge la Katiba waongezewe Posho

Mtamile

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
2,838
1,267
Kupitia ukurasa wake facebook Mtatiro amesema hivi

Julius S. Mtatiro
NCHI HII ITAMALIZWA;
Tunafahamu kuwa kuna njama zinapangwa ili wajumbe wa bunge la
katiba ati waongezewe fedha zaidi.
Hoja hii imetolewa leo hii na mmoja wa wajumbe huku ikionekana
kuwa maarufu na inayoungwa mkono na baadhi ya wajumbe, hasa
wabunge wa CCM.
Binafsi na wenzangu wengi tumepanga kutumia kila uwezo kuzuia
nia hiyo OVU, ifikie wakati tuambiane ukweli vinginevyo nchi hii
watu watakufa masikini.
Shilingi laki tatu tunazopewa kwa siku zinatosha kabisa, ambaye
hazimtoshi aongeze za kwake, na ambaye anaona hawezi kuongeza
zake aondoke Dodoma ili kupisha wanaoweza kutunga katiba kwa
posho ya shs 300,000 waendelee.
Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na CHENJI inabaki, zinatosha
kula, kulala, kumpa dereva na kuishi Dodoma.
Lazima sisi tunaotunga katiba tufahamu kuwa maisha ya wananchi
ni muhimu na kwamba wana mahitaji yasiyokwisha hata baada ya
bunge hili.
Baadhi yetu tulioko humu bungeni tutakataa jambo hili kwa
maneno na vitendo. Wakipitisha kwa wingi wao tuta-boycott
kuzipokea.
Kenya pale mnakumbuka hoja ya wabunge kujiongezea mapesa
ilipingwa vikali na wananchi waliandamana hadi nje ya ukumbi wa
bunge. Hapa Tanzania hata zikiongezwa milioni kila siku hutaona
mwananchi anachukua hatua kwa vitendo, kuoneshwa
kutoridhishwa kwake.
Tuna tatizo kubwa sana, sisi viongozi na wananchi wetu. Kuna mtu
anasema, viongozi ni zao la jamii hiyohiyo.
Tuungane pamoja kusimamia jambo hili, ninyi mlioko nje na sisi
tulioko ndani.
SOURCE: Mtatiro Facebook
 
Hiyo siyo NJAMA, wenyewe wanasema huo ndiyo mpango mzima. Watu wamekwenda kupiga KURA na kubadili matakwa ya wananchi, halafu wanataka mavumba ya kumwaga.
 
Naomba kwenye katiba hii wananchi tupewe nguvu kikatiba ya kujichukulia sheria mkononi pale tunapoona watawala wanatupuuza, na kwa kuanzia ni kwamba once watanyofoa mawazo ya wananchi (ambao ni wengi) kwenye rasmu hii waliokwenda kuiboresha wakirudi mtaani turuhusiwe kuwachapa bakora!
 
Kenge anapenda sana mayai na akiyakuta sehemu yuko tayari ashindwe kutembea lakini ayameze yote. Lakini ukimsogelea uwe makini anajua kujilinda sana kwa kutumia mkia wake. Kazi kwenu Watz.
 
Naomba kwenye katiba hii wananchi tupewe nguvu kikatiba ya kujichukulia sheria mkononi pale tunapoona watawala wanatupuuza, na kwa kuanzia ni kwamba once watanyofoa mawazo ya wananchi (ambao ni wengi) kwenye rasmu hii waliokwenda kuiboresha wakirudi mtaani turuhusiwe kuwachapa bakora!

mkuu unataka kuwacharaza viboko kama vya shuleni kabisaa? kama ndo hivyo mimi nitamshughulikia mbunge wangu Ngeleja
 
mkuu unataka kuwacharaza viboko kama vya shuleni kabisaa? kama ndo hivyo mimi nitamshughulikia mbunge wangu Ngeleja

Yes mimi nipo namsikiliza bwana Idd Azan kila siku ngoja ateleze kisha arudi kitaa, labda aishie kwao huko Magomeni ila kinondoni asikatize....
 
Ni kigezo gani mtatizo ametumia kuridhika na laki tatu? mbona hajakataa kiasi hicho kama alivyofanya ZITTO kama kweli ana uchungu na nchi hii?
 
matatiro, usijali bro, nyongeza ni sehemu ya rushwa ya sisiem ili agenda zake zipite.

pili kama nchi ikichukuliwa na upinzani masisiem watakuwa wafanya besara wakubwa kwani njama za kuua au kufilisi waliopo kwa kutumia ile mashine imeshasukwa. Kila mwenye mashine anatoza VAT. Bidhaa moja vat hata mara 4 sawa tu
 
Nimemchukia tu mtatiro kwa kutaja jina la chama changu makini. Nawajua wapenda posho kuwa ni akina Lema, Masawe, Lyimo nk wote hao wanajulikana ni wa chama gani
 
vizuri, tunasubiri kuona hili,labda safari hii hatua zitachukuliwa na wananchi!
 
matatiro, usijali bro, nyongeza ni sehemu ya rushwa ya sisiem ili agenda zake zipite.

pili kama nchi ikichukuliwa na upinzani masisiem watakuwa wafanya besara wakubwa kwani njama za kuua au kufilisi waliopo kwa kutumia ile mashine imeshasukwa. Kila mwenye mashine anatoza VAT. Bidhaa moja vat hata mara 4 sawa tu
Mkuu, mwambie akatae hiyo laki tatu kwani laki moja tu inamtosha.
 
Mambo mengi ya ajabu ajabu yamebaki kutokea Tannganyika pekee! Wanaona Watanzania watawafanya nini? Kama kuiba wanaiba mchana kweupe hakuna wakuchukua hatua, kama kuua wako tayari tena mchana kweupe nani atasimamia haki Tanganyika ilihali wananji pamoja na hao wanaoijifanya ni wenye nuru(wasomi) akili zao zimejaa giza. Hata wakipewa milioni kwa siku hakuna atakaye thubutu kuiacha wala atakayelamika wala kuchukua hatua. Hii ni nchi ya Mazombi hata awe nani bado ni zombie tu.
 
.............Laki tatu tunazopata zinatosha kila kitu na CHENJI inabaki, zinatosha
kula, kulala, kumpa dereva na kuishi Dodoma................

Yaani nimecheka kweli hapo. Huyu huyu Mtatiro nimjuaye ameenda na dereva huko? Aseme ukweli bana. Yeye ameenda na nyumba ndogo na kila mtu aliyepo huko anajua
 
Back
Top Bottom