Mtatiro Julius apata ajali mbaya Morogoro

marmoboy

Member
Mar 22, 2011
52
22
Wadau,

Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kwamba kamanda mpambanaji wa CUF na kiongozi wa kutumainiwa wa chama hicho JULIUS MTATIRO amepata ajali mbaya eneo la KILOMETA KUMI kutoka Morogoro mjini.

Mtatiro ambaye ni NAIBU KATIBU MKUU wa CHAMA CHA WANANCHI CUF Tanzania bara alikuwa akitokea IGUNGA ambako alikuwa na ziara ya siku 5 kuimarisha ngome ya chama chake katika uchaguzi mdogo ambao utafanyika hivi karibuni.

Inasemekana Mtatiro alikuwa anatumia gari yake aina ya TOYOTA LANDCRUISER yenye namba T438 AZG.

Katika gari hiyo alikuwemo yeye, dereva wake, mlinzi wake na ndugu KATANI AHMED KATANI mgombea mchakachuliwa wa CUF jimbo la TANDAHIMBA.

Taarifa zimenieleza kuwa gari hiyo ilikata STADI za tairi moja ya nyuma na tairi ikachomoka hivyo gari ilipoteza mwelekeo na kupinduka mara tatu.

SHUHUDA aliyenijulisha anasema mamia ya wakazi wa Morogoro wanaelekea eneo la ajali na polisi wamekwishafika eneo la tukio kutoa msaada.

Gari imeharibika vibaya.

Kwa sababu mtatiro alikuwa anatoka kwenye harakati za kuwakomboa watanzania tunamtakia maumivu ya pole yeye na wenzie.

Mungu awe pamoja na mpambanaji huyu anayeaminiwa na maelfu ya watanzania. Mungu amponye na amnusuru na sana. Mungu awalinde wapambanaji wote wa CDM na CUF.

SINA TAARIFA ZINGINE ZAIDI HADI HIVI SASA ILA GARI HAITAMANIKI.

Amina

UPDATES:

Ukweli ni kwamba, Mtatiro kapata ajali umbali wa kilomita 15 kabla ya kuingia mjini Morogoro wakati akitokea Igunga na ajali imetokea saa 11 unusu. Hata hivyo Mtatiro yuko salama na amepata majeraha kidogo. Huu ndio Ukweli wa tukio hilo wakubwa!
NYONGEZA: Gari alilokuwamo limeharibika vibaya kama mtoa thread hii alivyoeleza ingawa kidoooogooooo alifanya watu wapate mstuko mkubwa kwa kusema huenda watu waliokuwamo garini wasitoke hai. Mwenyezi Mungu kawanusuru walau hadi wakati huu.

Tuendeleeni na majukumu yetu wakubwa
Wamepelekwa hospitali, Mungu ni mwema.
 
natoa pole nyingi sana kwa Mtatiro na wenzake, tuwaombee watoke salama na wapone haraka na kurejea katika majukumu yao ya kawaida,

Mungu wetu ni mwema sana na amesikia sala zetu, amina.

tumhimidi Bwana kila wakati
 
aisee ngoja nifanye mchakato wa kupata habari kwa sababu niko hapa morogoro nitawapa habari
 
Wadau,
Taarifa zilizonifikia hivi punde ni kwamba kamanda mpambanaji wa CUF na kiongozi wa kutumainiwa wa chama hicho JULIUS MTATIRO amepata ajali mbaya eneo la KILOMETA KUMI kutoka morogoro mjini.

Mtatiro ambaye ni NAIBU KATIBU MKUU wa CHAMA CHA WANANCHI CUF Tanzania bara alikuwa akitokea IGUNGA ambako alikuwa na ziara ya siku 5 kuimarisha ngome ya chama chake katika uchaguzi mdogo ambao utafanyika hivi karibuni.

Inasemekana mtatiro alikuwa anatumia gari yake aina ya TOYOTA LANDCRUISER yenye namba T438 AZG.
Katika gari hiyo alikuwemo yeye,dereva wake, mlinzi wake na ndugu KATANI AHMED KATANI mgombea mchakachuliwa wa CUF jimbo la TANDAHIMBA.

Taarifa zimenieleza kuwa gari hiyo ilikata STADI za tairi moja ya nyuma na tairi ikachomoka hivyo gari ilipoteza mwelekeo na kupinduka mara tatu.

SHUHUDA aliyenijulisha anasema mamia ya wakazi wa morogoro wanaelekea eneo la ajali na polisi wamekwishafika eneo la tukio kutoa msaada.

Gari imeharibika vibaya na inasemekana ni vigumu kutoa mtu yeyote hai.

Kwa sababu mtatiro alikuwa anatoka kwenye harakati za kuwakomboa watanzania tunamtakia maumivu ya pole yeye na wenzie.

Mungu awe pamoja na mpambanaji huyu anayeaminiwa na maelfu ya watanzania. Mungu amponye na amnusuru na sana. Mungu awalinde wapambanaji wote wa CDM na CUF.

SINA TAARIFA ZINGINE ZAIDI HADI HIVI SASA ILA GARI HAITAMANIKI.

Amina.
Natoa pole saana kwa Ndg yetu mpambanaji wa CUF na watu ailoambatana nao Mungu awaponye katika sakata hili la ajali. Tafadhari zidi kutupa taarifa ya hilo janga, poleni saana tena!!!!!!!!!!!
 
Poleni sana wote waliopatwa na ajali,Mungu awape afya njema muendelee kulitumikia
taifa kwa moyo wote
 
Mwenyezi Mungu ni Mwema, naamini Mtatiro na wenzake wata/wametoka hai kwa kudra zake Allah!
 
Wadau wa moro jaribun kudadavua hbr from there, mungu awajalie wapambanaji wetu watoke salama.
 
I pray for all the casualities,may they be well as soon as possible in the name of Jesus Christ,Mungu atume msaada wake uhai wao uwe rescued.amen.
 
Very sad news kwa vyama vya upinzani, With God willings Mtatizo na wenzeka bado wanahitajika kututumikia.
 
Back
Top Bottom