Mtatiro atangaza maandamano ya CUF kupinga DOWANS

Hili la Dowans inabidi lituungnishe watanzania wote wazalendo bila kujali itikadi ili seikali ipate somo. Hivi hawa hawoni kuwa kuilipa kampuni hewa ni kuhujumu uchumi?
 
Ni jambo la kheri kwa nchi yetu lakini kama kweli wana nia ya thati ya kuzuia malipo haya katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif naye awepo kwenye hayo maandamano.
 
Naona watu wanaleta upinzani mpaka kwenye mambo ya msingi.
Watanzania umefika wakati pale mtu akiongea jamboi la msingi lenye manufaa ya umma na taifa lkwa ujumla tumuunge mkono.
Swala la dowans ni ni sawa na janga la kitaifa na hizi danadana za mambo ya ufisadi nia sawa na homa ya ya taifa.
Kama tunataka kuondokana na kwikwi hii basi katika mambo ya muhimu yatupasa tuungane ili kupigana na adui yetu mmoja naye ni fisadi sio kuendekeza ilani za vyama vyetu katika keki ya taifa.

Wito wangu kwa vyama vingine vikae chini na CUF ili kuweza kuunganisha nguvu siku hiyo na maandamano kuwa ya nchi nzima. Kelele za haki sawa au peoples power zenye utengano hazimzuii kuku kukimbia na panzi mdomoni na mkikaaa kimya panzi ataliwa tu.

Huu ni wito kwa wanaharakati wote, wanasiasa wote ili kweli nguvu ya umma ionekane na kusikika.

Pamoja tunaweza na kuweka itikadi zetu pembeni kwa masaa machache tu. WAO WANA DOLA SISI TUNA MUNGU NA NGUVU YA UMMA HAKIKA TUTASHINDA.
 
Mtatiro anatumiwa tu na CUF kuimarisha chama lakini kazi yake ikiisha atatimuliwa kama walivyotimuliwa akina James Mapalala, Rwakatarwe, Tambwe Hiza na wengineo. CUF walikuwa wanaitaka serekali ya SMZ na wameshaipata, na kazi yao imeshaisha. Nataka nimwone Maalimu Seif kwenye maandamano. Kama hayupo, then ni porojo tu. in fact CUF sio chama cha upinzani kwa sasa.

lazima wewe utakuwa ccm, unakatisha tamaa wanamageuzi. watanzania tunataka maisha bora si ushabiki wa vyama.
 
Hili la Dowans inabidi lituungnishe watanzania wote wazalendo bila kujali itikadi ili seikali ipate somo. Hivi hawa hawoni kuwa kuilipa kampuni hewa ni kuhujumu uchumi?

Maneno kama hayo ndo yanatakiwa kutamkwa na mtanzania this time. maisha magumu tuungane kutafuta mbadala. tuache ushabiki wa vyama. period.
 
CUF ISISUMBUE WANANCHI,DOWANS LAZIMA WALIPWE NA HILI WATANZANIA LAZIMA TULIJUE,HAMNA UJANJA HAPA SASA CHA KUANYA NIKUPANGA MPANGO WA KUWASHTAKI WALIOWAPOTOSHA TANESCO NA SIO KUANDAMANA KUPINGA MALIPO YA DOWANS

WANASHERIA WA SHERIA ZA MIKATABA WANAJIULIZA MASWALI MAWILI TUU KUJUA KAMA DOWANS WATALIPWA AU LA

DOWANS WALIZALISHA UMEME- ndio

TANESCO WALIPOKEA UMEME WA DOWANS-ndio

TANESCO WALIVUNJA MKATABA NA DOWANS VISIVYO HALALI-ndio

TOSHA KABISA,HAPA MAANA YAKE NI KUWA DOWANS WANA HAKI YA KUPATA HAKI KUTOKA MKATABA WAO NA TANESCO
 
Hivi kesi iliyochukuliwa maamuzi mahakamani ilikuwa ni kati ya Dowans na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au ni kati ya DOWANS na TANESCO? Na mbona Tanesco wapo kimya sana au wao wanahusika zaidi na kutoa ratiba za kukata umeme?
 
Back
Top Bottom