Mtanzania yupo rumande - washington dc.

Status
Not open for further replies.

Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
993
252
Ndugu Wanajamii,
kuna Mtanzania mwenzetu mmiliki wa kampuni ya "Mambo Jambo (USA) "amekamatwa Jumapili ya tarehe 18/01 na kufikishwa mahakamani Alhamis ya tarehe 22/01 .Dhamana ya Mwenzetu huyo ni $ 1.7m.Bado haifahamiki wazi makosa ya mwenzetu huyo,Watu wa Ubalozini wamefahamishwa Tukio hilo,Kwa ndugu mliopo DC na maeneo ya karibu,mnaweza kufuatilia kwa ukaribu habari za ndugu huyo,kama kuna chochote tufamishane kwa njia hii
 
Inaelekea ni kosa kubwa kutokana na ukubwa wa dhamana. Tusubiri tusikie kipi kilichojiri hadi akamatwe.
 
Je ndugu yetu ni tapeli?
Ndugu yetu Mzalendohalisi, nilitegemea kutokana na jina lako, ndugu yetu kapatwa shida, ungetanguliza uzalendo wa kuingiwa na huruma kwanza, haijalishi kafanya nini, ndipo tujue kulikoni na tutamsaidiaje, wewe ndio unakuja na swali hilo?.
Lets be positive and unite in times of need no mater what.
 
Kuna mambo mengine hamna utanzania mwenzetu! Madawa ya kulevya, ubakaji, uuaji n.k.
 
Kila kitu kitakuwa pouwa tu....Obama sasa ndo raisi na mwambieni mshikaji atatoka muda si mrefu....with Obama in office everything will be alright...
 
Tusiwe wepesi kuhitimisha,,tusubiri twone mwisho wake,si swala la Obama in the office,ni swala la kusaidiana kama Watz.
 
Acheni ushabiki, this guy must be in a serious shit big tym, mbona kina Othmani Njaidi na wenzake hamkushabikia!! Ndugu zake watahangaika naye thats the way it is, but for now tunaweza tu kumuombea ila kama amefanya short cuts zilizopitiliza kama drug dealing na nyinginezo basi namuombea long prison sentence. I'm out.

naomba kuwakilisha
 
Ndugu yetu Mzalendohalisi, nilitegemea kutokana na jina lako, ndugu yetu kapatwa shida, ungetanguliza uzalendo wa kuingiwa na huruma kwanza, haijalishi kafanya nini, ndipo tujue kulikoni na tutamsaidiaje, wewe ndio unakuja na swali hilo?.
Lets be positive and unite in times of need no mater what.

Ndugu,
Unajua deal kubwa kubwa hizi..sasa mimi Mtoto Mkulima..nitasidia hapo nini? Ikiwa madawa ya kuwevya je?

Ila nakubaliana nawe kuwa bado ni Mtanzania nwenzetu!
 
Kila kitu kitakuwa pouwa tu....Obama sasa ndo raisi na mwambieni mshikaji atatoka muda si mrefu....with Obama in office everything will be alright...

Nyani are you serious? Lini utaacha kebehi? Kuna kitu huyu jamaa amefanya ndio maana yuko ndani. Sasa je based on your assumption, ina maana Pres. Obama kazi yake ni ku bail waafrica just because he happen to have a dark skin hata kwa issues ambazo ziko mikononi mwa sheria na hazieleweki kama hii hapa?
 
narrow minded people will think that Obama is gonna turn water into milk or honey, folks for ur info ur deadly wrong.This sounds like a capital crime judging from the bail.I wish and pray that justice will take its course.
 
Wanajamii Habari ya mwenzetu kuwa ndani ni ukweli na imethibitishwa na ndugu na jamaa zake wa karibu ikiwa ni pamoja na rafiki yake wa kike (mzazi mwenzie) ambaye anaishi eneo/ nyumba moja na Mtuhumiwa,ndugu hawa wanaishi Columbia,Maryland........Jina la ndugu yetu huyo litatajwa hapa baadaye kwa idhini ya Kaka yake.

Ni jambo kubwa na linalosikitisha,ikiwa kama Jamii iliyostaarabika inabidi tusaidiane katika kuelimishana na kuelekezana baadhi ya mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa sheria,ni vyema ikumbukwe kuwa hatuko nyumbani...kwa maana hiyo ni vyema kuishi kwa kufuata na kutii taratibu za sheria.Tofauti ya hivyo tutakuwa tunajenga sifa mbaya na kuharibu jina Tanzania.....Tuna watoto na Wajukuu huko,tusiwaharibie maisha kwa sababu tu Baba/Mama zao tulishindwa kuishi katika misingi ya HAKI na USTAARABU.

Nimepata mshtuko mkubwa baada ya kuambiwa kuwa Watanzania nasi tumekuwepo kwenye macho ya sheria baada ya miaka ya karibu kuzidi kuonekana ktk vyombo vya sheria haswa kwa uvunjaji wa taratibu za maisha,ama kwa uizi,ubakaji,Ugomvi,Fujo (kelele),kutolipa pango, kuchinja mifugo hadharani au kulewa kupita kiasi.Kwa maana hiyo inabidi tuangalie upya tabia zetu ili kujenga Jamii yenye Heshima.

Ndugu yetu tunayemzungumzia, amepata matatizo kwa masuala yanayohusu "Ununuzi na uuzaji wa nyumba",matatizo hayo sio ya kwake tu,kuna ripoti kuwa kuna Watanzania wengine katika majimbo ya Arizona,Illinois,Minnesota na Texas ama wanaangaliwa au wamekwishaitwa kwenye vyombo vya dola kujibu mashitaka ya "Ujanja wa biashara za nyumba".Na baadhi ya ndugu hao ama wamekimbilia Canada au kurudi nyumbani kwa kuogopa mkono wa Serikali.......Pamoja na mashtaka hayo,ndugu yetu huyo wa Maryland ana mashtaka mengine karibu 40 yaliyosomwa kwake kwenye mahakama ya Rockville,MD.

Tuendelee kuelimishana na kuelekezana namna ya kuishi kwa kujali sheria....Lakini bado kwa umoja wetu nafikiri inapaswa kuangalia namna ya kumsaidia mwenzetu!!
 
Ndugu yetu Mzalendohalisi, nilitegemea kutokana na jina lako, ndugu yetu kapatwa shida, ungetanguliza uzalendo wa kuingiwa na huruma kwanza, haijalishi kafanya nini, ndipo tujue kulikoni na tutamsaidiaje, wewe ndio unakuja na swali hilo?.
Lets be positive and unite in times of need no mater what.

Hivi kuna msaada gani hapa? you must be kidding kama unafikiri tunaweza kuchangishana na kurise hiyo $1.7m hapa! Au unadhani huko kuna mambo ya kwenda kuongea na wakubwa au kuhonga ili atoke? Siamini kama vyombo husika vilikurupuka kumkamata huyu bwana, uchunguzi wa kutosha utakuwa umefanyika- tuiache sheria ifuate mkondo wake, if he is innocent atatoka tu na kama amekuwa akijihusisha na uhalifu let him pay the price na hii iwe fundisho kwetu sote.Kazi za boksi zipo kibao lakini kama unadhani utapata pesa za chapchap huku ughaibuni kwa njia za mkatomkato basi utegemee mambo kama haya!
 
...ni vyema ikumbukwe kuwa hatuko nyumbani...kwa maana hiyo ni vyema kuishi kwa kufuata na kutii taratibu za sheria.

Unasema tufuate sheria kwa vile hatuko nyumbani!

Sawa Mkubwa, tumekuelewa, tutavumilia mpaka tukirudi nyumbani!
 
kwa kweli hapo acha sheria ichukue mkondo wake, hao jamaa wako makini sana siku ya kukupeleka kwenye sheria wameshamaliza uchunguzi wote na kuwekewa bail kubwa namna hiyo ni kwa sababu ya uzito wa kosa lenyewe,
nadhani inatakiwa tuwe makini kwa kila kitu tunachofanya especially nje ya nchi ambako sheria na haki za binadamu zinafuatwa
 
Wanajamii Habari ya mwenzetu kuwa ndani ni ukweli na imethibitishwa na ndugu na jamaa zake wa karibu ikiwa ni pamoja na rafiki yake wa kike (mzazi mwenzie) ambaye anaishi eneo/ nyumba moja na Mtuhumiwa,ndugu hawa wanaishi Columbia,Maryland........Jina la ndugu yetu huyo litatajwa hapa baadaye kwa idhini ya Kaka yake.

Ni jambo kubwa na linalosikitisha,ikiwa kama Jamii iliyostaarabika inabidi tusaidiane katika kuelimishana na kuelekezana baadhi ya mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa sheria,ni vyema ikumbukwe kuwa hatuko nyumbani...kwa maana hiyo ni vyema kuishi kwa kufuata na kutii taratibu za sheria.Tofauti ya hivyo tutakuwa tunajenga sifa mbaya na kuharibu jina Tanzania.....Tuna watoto na Wajukuu huko,tusiwaharibie maisha kwa sababu tu Baba/Mama zao tulishindwa kuishi katika misingi ya HAKI na USTAARABU.

Nimepata mshtuko mkubwa baada ya kuambiwa kuwa Watanzania nasi tumekuwepo kwenye macho ya sheria baada ya miaka ya karibu kuzidi kuonekana ktk vyombo vya sheria haswa kwa uvunjaji wa taratibu za maisha,ama kwa uizi,ubakaji,Ugomvi,Fujo (kelele),kutolipa pango, kuchinja mifugo hadharani au kulewa kupita kiasi.Kwa maana hiyo inabidi tuangalie upya tabia zetu ili kujenga Jamii yenye Heshima.

Ndugu yetu tunayemzungumzia, amepata matatizo kwa masuala yanayohusu "Ununuzi na uuzaji wa nyumba",matatizo hayo sio ya kwake tu,kuna ripoti kuwa kuna Watanzania wengine katika majimbo ya Arizona,Illinois,Minnesota na Texas ama wanaangaliwa au wamekwishaitwa kwenye vyombo vya dola kujibu mashitaka ya "Ujanja wa biashara za nyumba".Na baadhi ya ndugu hao ama wamekimbilia Canada au kurudi nyumbani kwa kuogopa mkono wa Serikali.......Pamoja na mashtaka hayo,ndugu yetu huyo wa Maryland ana mashtaka mengine karibu 40 yaliyosomwa kwake kwenye mahakama ya Rockville,MD.

Tuendelee kuelimishana na kuelekezana namna ya kuishi kwa kujali sheria....Lakini bado kwa umoja wetu nafikiri inapaswa kuangalia namna ya kumsaidia mwenzetu!!

Jana tu ulipoanzisha hii thread nilijua kuwa jamaa ni mwizi....sina sympathy na hawa "mabingwa" wanaotaka fweza za fasta fasta ktk nchi za watu, ufisadi huko huko bongo hii ni nchi ya sheria, ukizivunja basi sooo ni lako mwenyewe!

Uki-google jina la hiyo kampuni yake unapata haya hapo chini:

MAMBO JAMBO, USA.
New entartainment company.
Established in 2001.
Based in arusha, tanzania.
We have recording studio in dar-es salaam, tanzania.
We have a radio station in arusha, tanzania (. Mj FM 93.0)
Our main office for entartainment and general supply is in Washington DC.
We supply everything all over the world includes food, electronics, building materials, etc Construction Materials Stocks ,Entertainment Projects ,Network Communications ,Truck & Parts ,
Business Type Distributor/Wholesaler
Products/Services Entartainment products, food, electronics, building materials
Our Markets Worldwide
No. of Employees 11 - 50 People

Mr. (nimefuta jina)
Address 8821 Goose Landing Cirlce, Columbia, Maryland, Tanzania
Zip Code 21045
Telephone +001 410 997-0992
Mobile 4109080923
Fax +001 410 997-0992
Website Mambo Jambo (Usa), Mambo Jambo (Usa)

Address hiyo imepinda, "8821 Goose Landing Cirlce, Columbia, Maryland, Tanzania." Toka lini??? Entertainment company gani ipo 'ivo?? Waajiliwa kati ya 11-50, hai-make sense (kwanini isiwe ni 11 au 50 badala ya huo uzushi wa 11-50??)...na maswali mengine kibao!!!

Watu waende shule, ukiwa na elimu hata ya community college hapa USA opportunities ni kibao wajameni! Hizi story wengine tumezichoka, mchango nitatoa kwa mtu mwenye issues na INS/ICE (noma yenyewe pia iwe ya kueleweka)....

Hata 'ivo pole mingi kwa huyo starring na familia yake, ndio ukubwa!!
 
Last edited:
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom