Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,854
Ninavyoelewa Mtanzania ni mtu mwenye uraia wa Tanzania i.e mtu aliyezaliwa UK na baba na mama waUK akachukua Uraia Bongo tunamwita Mtanzania hatumwiti Mwingereza.
Wangesema ni raia wa UAE ambaye ana asili ya TZ nadhani ingekuwa karibu zaidi na ukweli. Kwa hiyo huyo Julius na Mtoto wake hawawezi kujiita Watanzania.
Kwa hiyo mara Julius alipochukua uraia wa Marekani basi uTanzania wake umepotea? Ninavyojua mimi ni kuwa uingereza na uraia wa uingereza ni vitu viwili tofauti. Raia wa uingereza akichukua uraia wa Tanzania, anachopoteza ni uraia wake tu lakini uingereza unabaki pale pale. Vile vile humu ndani wako wenzetu wengi ambao bila shaka wana uraia wa nchi tofauti na Tanzania lakini wako mstari wa mbele kujivunia u-Tanzania wao. Nadhani wakati umefika wa kutofautisha uraia wa Tanzania na u-Tanzania.
Amandla.......