mtanzania;Kada wa CCM awashukia Msekwa, Nape

Jul 24, 2012
81
6
[h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:46 Na Elizabeth Mjatta

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), David Msuya, amekitaka chama chake kubadilisha mfumo wa kumpata Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, ili nafasi hiyo iwe ya kugombea.

Msuya alisema mfumo wa sasa wa kumteua kiongozi huyo wa chama, unawanyima fursa watu wenye uwezo wa kushika nafasi hiyo na matokeo yake nafasi inapwaya.

“Mimi nataka nafasi hii iwe ya kugombea kama nafasi nyingine, yaani itangazwe na ikiwa hivyo na mimi nitachukua fomu kwa sababu naona naweza kushika nafasi hiyo, nina uwezo, nataka niingie niondoe mfumo mbovu uliopo.

“Sasa hivi mfumo ni mbovu, watu wanaomba kugombea nafasi za uongozi majina yanakatwa hovyo, mimi nipo muda mrefu ndani ya chama toka mwaka 1996, mambo haya hayakuwepo, lakini nashangaa kuona Pius Msekwa kama Makamu mwenyekiti hasemi chochote.

“Mimi naona sasa hivi Msekwa amechoka, inabidi nafasi ile aachie vijana kwa sababu nafasi yake ni kubwa, kwani inamwezesha kukutana na Rais, lakini nashangaa sioni kama anafikisha malalamiko ya wananchi kwa rais ili kufanya mabadiliko,” alisema Msuya.

Mbali na Msekwa, alisema pia kwamba, wapo pia baadhi ya viongozi wa chama hicho waliopo kisiasa na siyo kwa maslahi ya chama.

“Kwa mfano, mtu kama Nape utasema ni kiongozi wa aina gani, Nape ameingia kisiasa zaidi ya utendaji, matokeo yake amekuwa mtu wa kujibu hoja za wapinzani bila kuzifanyia utafiti wa kina.

“Wakati mwingine CHADEMA ni wajanja, wanatoa hoja kwa kututega, wanajua kabisa kwamba CCM ni dhaifu, lazima watajibu,” alisema Msuya.

Alisema kwamba, alitegemea Nape kama Katibu Mwenezi angeweka mikakati ya kuwafanya vijana wasitoke ndani ya chama, badala yake mwanasiasa huyo anaanza kuzungumzia majina ya watu na kujibu hoja za wapinzani.

“Kwa nini Nape asiangalie CHADEMA wanatumia mbinu gani kuwashawishi vijana kujiunga na chama chao, kwa nini asiangalie ni mbinu gani wanazitumia hadi kushawishi watu kujaa kwenye mikutano yao, haya mambo ya kukurupukia hoja aachane nayo na anatakiwa kuangalia mbinu za kukijenga chama,” alisema.

Alisema viongozi hao wameshindwa kuwajibika ipasavyo ndani ya chama hadi kukifanya chama kukimbiwa na vijana.

“Ushauri wangu ni kwamba, mtu anayeona ameshindwa kukitumikia chama aondoke, akae pembeni na si kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuchafua majina ya watu na kujibu hoja bila kuzifanyia utafiti,” alisema.
 
Ni mtazamo mzuri ingawa ni vigumu kwa CCM yenyewe kuja na mikakati ya kweli ya kuwavutia vijana wa leo kujiunga nacho na hata kuwa na mvuto wa kujaza washiriki wa mikutano ya hadhara kwa hiari. Nadhani there are too many factors influencing what we currently see from the party. Just to mention a few; utendaji mbovu wa viongozi wakuu katika serikalini inayoundwa na CCM, uhusika wa familia za viongozi wa chama na serikali katika kuendesha chama na shughuli za serikali, na influence ya viongozi wa serikali na wafanyabishara kwenye maamuzi ya chama. haya yote yanahitaji viongozi wa chama wenye uwezo mkubwa na full utilization of the party thinkTank sio design za watu kama Nape au Mwigulu ambao ni hodari wa kuattack na kushout bila kufikiria.
 
Msuya amewapa ukweli lakini amechelewa mno yaani ni kama kumwashia mgonjwa dawa hospt wakati ameshadead, nape ni kama jiwe hasikii na alishaambiwa mengi,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom