Mtanzania 'Gaidi' apandishwa Kizimbani Marekani (New York, Marekani)

LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,014
574
Mtanzania anayetuhumia kuhusika katika mashambulio ya mabomu dhidi ya balozi za Mareka mjini Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya mwaka 1998, Ahmed Khalifan Ghailan,ametajwa juzi na mwendesha mashtaka wa mahakama ya Manhattan nchini Marekani kama muuaji wa halaiki.

Ghalaini anatuhumiwa kuwa mwanachama wa kikundi cha Al-Qaeda katika eneo la afrika Mashariki kilichopanga na kufanya mashambulio hayo ya Julai 7 mwaka 1998.

Ghalain ambaye alikuwa ameshikiliwa awali katika gereza la Guantanamo nchini Cuba, ndiye mshukiwa wa kwanza katika gereza hilo kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya kiraia nchini Marekani.

Jaji Lewis Kaplan anayesikiliza kesi hiyo amesema huenda kesi ya Ghailani ikaendelea hadi mwakani.

Katika mchango wake wa mwisho katika kesi hiyo, mwendesha mashtaka wa mahakama Manhattan, Harry Cherttoff alisema, Ahmed Khalfan Ghailani ambaye alikuwa ameketi viti kadhaa upande wake kushoto, ni muuaji wa halaiki mwenye alama ya adamu ya mamia ya watu mikononi mwake.

Ghalaini, Mtanzania anayetoka Zanzibar, ana umri wa miaka 36 na anahusishwa sana katika kupanga mlipuko ya mabomu katika balozi za Marekani katika mji wa Nairobi na Dar es Salaam mwaka 1998 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia mbili.

Mshukiwa huyo alikana makosa hayo.
Mahakama ya Manhattan ipo hatua chache kutoka katika jengo la mnara wa World Trade Centre (WTC) ambapo shambulio la kigaidi la september 11 mwaka 2001, lilitekelezwa na wanachama wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Wachunguzi wanalinganisha uhusiano uhuo kama hatua kubwa ya kutanzua mashambulizi ya kigaidi.

Raisi Barack Obama wa Marekani alitoa amri ya kufungwa kwa mahakama ya kijeshi ya Guatanamo na washukiwa wanaoshikiliwa wafunguliwe mashtaka katika mahakama ya kiraia.

Azimio hilo lililpingwa vikali na wachunguzi kadhaa wakidai kuwa uzito wa kesi hizo za ugaidi haufai kushughulikiwa katika mahakama za kiraia



Source: Nipashe Nov 10, 2010
pg 15
 
Vipi hukumu yake iliendaje. Uzi una miaka 10 umekosa wachangiaji

ᴾᵘⁿⁱˢʰ ᵒⁿˡʸ ʰᵉ ʷʰᵒ ᶜᵒᵐᵐⁱᵗᵗᵉᵈ ᵗʰᵉ ᶜʳⁱᵐᵉ
 
Kwahiyo amefungwa kwenye gereza gani

ᴾᵘⁿⁱˢʰ ᵒⁿˡʸ ʰᵉ ʷʰᵒ ᶜᵒᵐᵐⁱᵗᵗᵉᵈ ᵗʰᵉ ᶜʳⁱᵐᵉ
 
Alishatoka huyu simba wa vita kwa sasa ghailan yupo Zenji ila akili zake hazipo sawa ata kdg kwani mtu anayemkumbuka ni mama yake tu basi. Jamaa nakumbuka alikua bingwa mara 4 katika tae kwan do, sijui ilikuwa vipi Ahmed akaingia kwenye matatizo haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom