MTANZANIA: CCM mnahangaika na Lowassa, CHADEMA wanachanja mbunga!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, June 15, 2011
Na Deodatus Balile

INANIWIA vigumu jinsi ya kuanza makala hii, kwani safu hii imekuwa na utaratibu wa kuja na kupotea. Inapotea si kwa nia mbaya, bali kutokana na mbanano wa majukumu unaonilazimu wakati mwingine kukesha bila kusinzia au kushinda bila kula, hii yote ikiwa ni harakati za kulijenga taifa hili na familia yangu kwa ujumla. Natumaini sijakukera mpendwa msomaji, ila nashukuru kwa wale wenye kunitumia barua pepe na wakati mwingine kunipigia simu kuhoji kulikoni mbona siandiki.

Leo katika safu hii naandika kitu ambacho pengine umekisoma, umekisikia mara nyingi na wakati mwingine unaelekea kusahau baadhi ya matukio. Ingawa sikuwa na muda wa kutosha kwa takribani miezi minne hivi, lakini nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mwelekeo wa siasa za nchi hii. Nilifuatilia na kushitushwa na uteuzi wa mdogo wangu Nape Nnauye kuwa Katibu Mwenezi wa CCM, eti tu kwa sababu alionyesha uwezo mkubwa wa kumtukana aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Matusi ya Nape yalianzia kwenye ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), ambapo mara zote bwana mdogo huyu alikuwa akitoa kauli za kuonyesha ujenzi wa jengo hili haufai kwa mbegu chakula wala dawa, lakini bosi wake Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete, wakati anaweka jiwe la msingi akasifia uamuzi wa Baraza la Wadhamini kuingia ubia na mwekezaji kujenga jengo hili.
Sitanii, hapana shaka hapa Nape hakuridhika. Aliugulia maumivu, lakini akaendeleza vurugu zake hadi Umoja wa Vijana wa CCM wakamnyang'anya kadi ya uanachama. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, bila shaka kwa mawazo yake akasikiliza redio na kusoma magazeti, bila kupima uzito wa hoja za Nape, akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya. Wapo waliodhani alimteua kumpoza machungu baada ya kunyang'anywa kadi, lakini wenye busara walishangazwa na uteuzi huo.

Kama hiyo haitoshi, Kikwete kwa mara nyingine akaishangaza dunia kwa kumteua Nape kuwa Katibu Mwekezi wa CCM. Nafasi hii inampa fursa ya kuingia kwenye Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa CCM. Kwa ujinga ule ule, Nape akadhani amepata fursa ya kupambana tena na Lowassa. Na ni siri iliyo wazi kuwa Nape hakuwa akipigania jengo la vijana dhidi ya Lowassa, bali hasira za kambi ya Lowassa kuiangusha kambi ya John Malecela na baadae kambi ya Profesa Mark Mwandosya kwenye king'ang'anyilo cha urais mwaka 2005.

Hakuna ubishi, kwamba hata Nape wakati anasoma makala hii, moyo wake unakumbuka yaliyotokea nje ya ukumbi wa Chimwaga Dodoma usiku wa mkutano mkuu wa CCM wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM, mwaka 2005. Kama ameyasahau mimi sitayasema gazetini, ila akamuulize aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT wakati huo Halima Mamuya, kisha atapa majibu jinsi upepo wa kisiasa unavyoweza kuvuma kutoka kusi kwenda kasi kwa kasi ya ajabu.

Sitanii, baada ya kuteuliwa kwa mwendelezo wa hasira zile zile zilizotokana na Lowassa kufanya vyema kazi yake ya kampeni hadi mgombea wa kambi yao akateuliwa kuwa mgombea urais wa CCM, Nape na John Chiligati, tena mimi namhurumia sana Chiligati. Ndiyo ana historia ya utumishi ndani ya CCM, lakini amejikuta akitumikia masilahi ya makundi pasipo kujua.

Wawili hawa wakaingia mitaani kwa mbwembwe, tena kwa kasi ambayo kwa wote wenye akili walijua huo ulikuwa moto wa kifuu au waswahili wanasema nguvu ya soda. Wakafungua midomo yao kwa upana waliotaka wao, maana walikuwa wamepewa kisemeo. Nape Mwenezi akiwa na Chiligati Naibu Katibu Mkuu (Bara). Wakatangaza waliyoyaita maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM, kuwa eti Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge ndiyo magamba wafukuzwe ndani ya chama kwani kwa ufisadi ndiyo waliopunguza ushindi wa CCM kutoka asilimia 81 hadi 61.

Wanatumia hoja za wizi wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) zinazodaiwa kukwapuliwa na Kampuni ya Kagoda na Kampuni ya Richmond. Sitamzungumzia Samuel Sitta, lakini namshukuru Mungu kwani anaipenda nchi hii. Kwa hasira zake za kukosa wadhifa fulani serikalini, aliamua kutumia uspika kuivuruga Serikali. Narudia na nasema pasipo woga, kuwa kama Sitta angepata kipindi cha pili cha uspika, nchi hii tungepigana vita.

Sitta hakuwa Spika, bali alikuwa kocha mchezaji. Ndiyo wale wale akina Nape Nnauye. Ndo wale wale mitume 12, waliokuwa wakidhani wanawambia wananchi kuwa Lowassa, Rostam na Chenge ni mafisadi wameiba fedha za EPA na Richmond, bila ushahidi, lakini pia bila akili yao kuwafahamisha kuwa walichokuwa wakifanya ni kukimaliza CCM mbele ya macho ya umma. Ni hawa hawa waliokidhofisha chama kwa kuwambia wananchi kuwa CCM ni chama cha mafisadi kinakumbatia mafisadi.

Waliifanya kazi hii kwa miaka mitano, lakini kwa mshangao katika siku 72 za kampeni mwaka 2010, wakawa wanapita kwa watu kujenga hoja dhaifu isiyojengeka kuwa CCM ni chama safi. Wananchi wale wale waliowambia CCM inanuka rushwa, ndiyo hao hao waliokwenda kuwaomba kura wakiwambia CCM haina rushwa ndani yake bali mwanachama mmoja mmoja. Tena washukuru Mungu, wananchi bado wana huruma na CCM. Kwa moto uliokuwapo, isingeshangaza kukuta leo CCM wangekuwa wanakaa upande wa kushoto kwa Spika Bungeni na wanaunda Baraza la Mawaziri Kivuli.

Sitanii, kwa ujinga tu, na neno hili ujinga naomba nielekweke kuwa hapa nimelitumia kwa maana ya ukosefu wa ufahamu, Nape na Chiligati wakadhani wanaweza kupotosha umma kwa kuwambia kuwa imeamuliwa Rostam, Lowassa na Chenge wapewe barua za kufukuzwa ndani ya CCM kwani wao ndiyo magamba. Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, alibaini kuwa hoja ya kutoa barua inakiua chama. Alilpokutana na wahariri pale Peacock Hotel Dar es Salaam, akalazimika kusoma maazimio ya NEC na hakuna sehemu iliyokuwa inataja watu hawa kupewa barua ndani ya miezi mitatu.

Nilikuwapo, na kwa kiwango cha hali ya juu cha utovu wa nidhamu, Nape akajaribu kumdhalilisha bosi wake Mukama mbele ya wahariri. Kwa muda tulishuhudia sinema ya bure. Wakati Mukama akisema hakuna maazimio ya aina hiyo, Nape akasema wakubwa hawa walitajwa kwa majina bila woga. Tena Nape huyo ambaye Mwalimu Julius Nyerere ametoka madarakani wakati yeye bado ananyonya, akadiriki kumsigina Mukama kwa kusema yeye (Nape) ni CCM ya Nyerere. Wengi tulishangaa na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda, hakuuma maneno akamwambia Mukama kuwa kwa mwenendo huo, CCM inakufa.

Nape aliendelea kufanya mikutano ya hadhara na kuropoka mengi kadri alivyoweza. Akafika mahala akatangaza kuwa wafanyabiashara ni magamba ndani ya CCM waondoke CCM ibaki kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Lakini wakati akitoa kauli hiyo, hakueleza falsafa ya nchi hii ni ipi. Iwapo Tanzania bado ni taifa la Ujamaa na Kujitegemea, ni Mabepari au tuko kama China ambapo mwaka 1979, kiongozi mashuhuri wa China, Deng Xioping alivyoongoza chama chake cha Kikomunisti kubadili mwelekeo wa kwa kutangaza taifa moja na mifumo miwili (one country two systems).

Xioping aliruhusu ukomunisti kuendelea lakini pia biashara (Nape anaita ubepari) kufanyika ndani ya China. Ni kutokana na uamuzi huu, China lililokuwa taifa masikini miaka 32 iliyopita, leo ni taifa la pili kwa utajiri duniani, likitanguliwa na Marekani tu. Japan wametangaza kuwa China imewaengua katika nafasi ya pili, sasa nao wanapambana kukuza upya uchumi wao kuhakikisha wanapanda tena.

Sitanii, Nape aliyekuwa akitutangazia kwenye mikutano ya hadhara kuwa ifikapo Julai; Lowassa, Rostam na Chenge wanapewa barua za kufukuzwa ndani ya CCM, leo akiulizwa anauma midomo. Badala yake amekirukia Chadema, anakwenda Rukwa anaeleza mambo ya aibu mbele ya jamii. Anatumia ishara za vidole viwili wanavyonyoosha Chadema kutamka maneno nisiyoweza kuyaandika gazetini. Hii ni dalili ya kutojiheshimu. Ni dalili ya kuwa na kiongozi asiye na chembe ya maadili katika jamii.

Chadema sasa wanatumia udhaifu wa CCM kuwa na viongozi chepechepe wa aina ya Nape na Chiligati wenye kuropoka kisha wakafungwa gavana midomo yao kujenga chama chao. Wanachanja mbunga wakiwaeleza wananchi umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Wanazungumza lugha wanazopenda kuzisikia wananchi kama kushusha bei ya mfuko wa saruji, bati na kilo ya misumari isizidi Sh 5,000.

Wiki hii Chadema wanazungumza kukata posho za wabunge, ambapo wanasema wabunge wanalipwa mara mbili kwa kazi ile ile. Hapa hoja ni sahihi kabisa. Kwamba mbunge analipwa mshahara kwa kazi ya ubunge, analipwa posho ya kujikimu Sh 80,000 kila siku anapokuwa Dodoma, kisha analipwa Sh 70,000 kila siku anapoingia kwenye ukumbi wa Bunge. Hili ndilo lenye kuleta mgogoro. Kila awaye anajiuliza hawa wanatutumikia sisi walala hoi au wamekwenda kuchuma utajiri bungeni?

Sitanii, hii ni fursa nyingine kwa Chadema kuzidi kukonga nyoyo za wapigakura. Na haya ndiyo magamba halisi kwa CCM. Hesabu zilizopigwa ni kwamba posho zilizotengwa zikikatwa nchi hii inaweza kuokoa zaidi ya Sh bilioni 900. Kiasi hiki cha fedha kingeelekezwa katika ununuzi wa mashinde za kufua umeme, kwa wastani wa megawati moja Sh bilioni moja, ndani ya mwaka huu pekee tungezalisha megawati 900.
Ikwia kiasi hiki cha Sh bilioni 900 kingeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu kama barabara, reli, usambazaji wa umeme vijijini au kununua madawati shuleni, kila mwanafunzi angekalia dawati. Lakini uliza. Hawa wabunge wakizipata hizi hela zinafanyiwa nini? Sitaki kusema ila ni aibu. Mwishoni mwa wiki nilikwua Dodoma, nilishuhudia maajabu. Wapo wabunge wanokesha baa wakinywa pombe na kuchoma nyama. Wengine wanafanya matendo ya kumuudhi Mungu, kwani karibu machangudoa wote wa Dar es Salaam na Mwanza sasa wamehamia Dodoma. Unadhani kama kusingekuwa na biashara machangudoa wangethubutu kulipa nauli kwenda Dodoma? Jibu mwenyewe.

Sitanii, napenda kuhitimisha makala hii kwa kutaja baadhi ya magamba yenye kuisumbua CCM na kama chama hiki kinataka kipendwe basi kirekebishe haya, nyoyo za wananchi zitakirudia. Lipo kundi la walimu waliohitimu katika vyuo mbalimbali wakaahidhiwa ajira, lakini hadi leo wanazisoma ajira zao magazeti hawajaziona, hili ni gamba. Mgawo wa umeme umesababisha baadhi ya viwanda vifungwe, hili ni gamba.
Bei ya sukari ilikuwa inauzwa Sh 450 mwaka 2005, leo ni Sh 1,800, hili ni gamba. Nauli ya daladala ilikuwa S 100 kwa wakubwa na Sh 20 kwa wanafunzi mwaka 2005, leo ni Sh 450 kwa wakubwa na Sh 150 kwa watoto, hili nalo ni gamba. Bei ya lita moja na petrol ilikuwa Sh 580 mwaka 2005, leo ni Sh 2100, lakini kwa nchi jirani kama Burundi lita ilikuwa sawa na Sh 450 za hapa mwaka 2005, leo ni Sh 1,200. Ikumbukwe mafuta yao yanapitia Dar es Salaam kabla ya kwenda Bujumbura. Hili nalo ni gamba.

Tuliwapa matumaini watoto wetu kuwa wataingia kwenye sekondari za kata, ni kweli wameingia, lakini sekondari hazina walimu, maabara au vitabu vya kiada na ziada, hili nalo ni gamba. Wakati hayo yakisemwa, kwa njia ya uongo uliokubuhu, matatizo yote yanaelekezwa kwa Rostam, Lowassa na Chenge kuwa ndiyo waliosababisha mazingira magumu hapa nchini.

Tena cha ajabu, hata kama Rostam angekuwa na dili Richmond, ambayo hadi kesho haijawahi kulipwa hata senti tano, ingawa Dk. Harrison Mwakyembe, aliwapotosha Watanzania na kuwambia kuwa ilikwua inalipwa Sh milioni 152 kila siku iendayo kwa Mungu, wakati uhalisia hawajawahi kulipwa hata senti tano, na hata hiyo Dowans inayotajwa kurithi mkataba wa Richmond hizo Sh bilioni 94 tunazosema zitaau uchumi haijalipwa bado kesi inaendelea mahakamani.

Maajabu kuliko yote, hizo Sh bilioni 94 zinazobishaniwa mahakamani sehemu kubwa ni malipo ya umeme tulioutumia wakati Dowans mitambo yake inazalisha umeme pale Ubungo kwa muda wa miezi 18. Kwamba umeme tuliutumia, fedha zinakusanywa kutoka kwa wananchi lakini Tanesco na Serikali haijawahi kuilipa Dowans umeme huo. Hivi nikuulize wewe mpendwa msomaji. IKiwa wewe unatumia umeme nyumbani kwao, hivi ipo siku uliwahi kwenda Tanesco kununua umeme wakakwamba usilipie huo ulikuwa umeme uliotokana na Dowans? Tuliutumia, hatutaki kuulipia.

Sitanii, siasa zimetufikisha hapo. Tuliikataa mitambo ya Dowans kisiasa tu, kwa muda wa miaka mitatu. Leo wamekuja Symbion wameinunua mitambo hiyo hiyo, inazalisha umeme na kupunguza makali ya mgawo wa umeme, tunashangilia. Hatuwapingi Symbion kwa sababu ni Wamarekani. Jamani, tutatawaliwa kimawazo hadi lini? Ukoloni mambo leo utaisha lini hapa kwetu? Mbona simsikii Sitta au Mwakyembe wakihoji ujio wa Symbioni? Nasema, nyie CCM endeleeni na harakati za kujivua gamba, wenzenu Chadema wanachanja mbunga.


Tuonane wiki ijayo
deobalile@yahoo.com au 0784 404827
 
Ushuuzi mtupu... Nenda kwa mafisadi ukachukue chako ukalale... watoto hawajaenda chooni siku ya tatu leo nyumbani!
 
Endeleeni kutuelimisha zaidi dhidi ya hawa mafisadi wavua magamba,tatizo nyani haoni ***** lake,zaidi anamcheka mwenzake anayemwona!yatasanuka mengi sana mwaka huu.
 
Alieandika makala hii nilianza kumsifia kwa uchambuzi wake mzuri wa kile anachojaribu kufanya Nape na mapungufu yake. Lakini pale karibu na mwisho alipoanza kuwatetea akina RA na EL ndio nikafumbuka macho na kuelewa nia ya makala yenyewe. Ukweli unabaki pale pale kwamba RA, EL na Chenge ni mafisadi waliokubuhu ingawaje CCM viongozi wote wa juu hakuna aliyemsafi tukianza na mwenyekiti wao!!!!

Tiba
 
The government, which was designed for the people, has got into the hands of the bosses and their employers, the special interests. An invisible empire has been set up above the forms of democracy and leave majority of our people poor...

At the end we must beware of Ministers in this government who can do nothing without money, and those who want to do everything with money.

It’s a sad day in our nation when you have members of members of parliamnet who are literally criminals go undisciplined by their colleagues. No wonder people look at Tanzania and their President and know this Country is totally broken.”
 
Sitta angepata kipindi cha pili cha uspika, nchi hii tungepigana vita

Hapa mwandishi ndiyo kaniacha hoi, du ina maana hao mafisadi wana watetezi wasio hata na aibu!!!!!! Huyu jamaa ameajiriwa na nani????
 
nice article lakini finishing duh! Ni sawa kujenga ghorofa kaaali afu choo cha passport size nje
 
Hapa mwandishi ndiyo kaniacha hoi, du ina maana hao mafisadi wana watetezi wasio hata na aibu!!!!!! Huyu jamaa ameajiriwa na nani????
Sasa nimeelewa kuwa hata uropokaji wa Nape pia ni gamba,Kikwete ndiyo gamba kuu kwa kutufikisha hapa tulipo bei ya vitu juu juu zaidi kila siku!Lakini pia hata mwandishi wa makala hii ni gamba anatetea magamba menzake yaliyoshindikana na yanasaka mtetezi mwenye moyo wa chuma ili kuyasafisha!
 
teh teh teh huu mwaka na unaokuja and the next tutaona na kusikia yasiosikika hahahaha magamba is going dowwwn deep down....
 
Wtz,haina haja kutafuta msimamo wa mwandishi wa makala hii,ni dhahiri ni gamba but ka alivyosema,cdm inasonga mbele na uzuri anatupa cha kuwaambia wananchi wht is wrong kwa magamba.ukitaka kumshinda adui yako,mwashe akuelezee matatizo yake na kupitia hapo,utajijenga na kumbomoa vizuri.
 
teh teh teh huu mwaka na unaokuja and the next tutaona na kusikia yasiosikika hahahaha magamba is going dowwwn deep down....

Kila kitu kina mwanzo na mwisho ninaona upuuzi huu umefikia mwisho kama Misri ya Mubaraka.
 
Mwandishi alvyo aanza article yake nilijisikia raha ya kuisoma nilpoendelea nilihis karaha tupu...! Nyumba nzur ya ghorofa ndan choo cha shimo....
 
Wednesday, June 15, 2011
Na Deodatus Balile


Sitanii, napenda kuhitimisha makala hii kwa kutaja baadhi ya magamba yenye kuisumbua CCM na kama chama hiki kinataka kipendwe basi kirekebishe haya, nyoyo za wananchi zitakirudia. Lipo kundi la walimu waliohitimu katika vyuo mbalimbali wakaahidhiwa ajira, lakini hadi leo wanazisoma ajira zao magazeti hawajaziona, hili ni gamba. Mgawo wa umeme umesababisha baadhi ya viwanda vifungwe, hili ni gamba.
Bei ya sukari ilikuwa inauzwa Sh 450 mwaka 2005, leo ni Sh 1,800, hili ni gamba. Nauli ya daladala ilikuwa S 100 kwa wakubwa na Sh 20 kwa wanafunzi mwaka 2005, leo ni Sh 450 kwa wakubwa na Sh 150 kwa watoto, hili nalo ni gamba. Bei ya lita moja na petrol ilikuwa Sh 580 mwaka 2005, leo ni Sh 2100, lakini kwa nchi jirani kama Burundi lita ilikuwa sawa na Sh 450 za hapa mwaka 2005, leo ni Sh 1,200. Ikumbukwe mafuta yao yanapitia Dar es Salaam kabla ya kwenda Bujumbura. Hili nalo ni gamba.

Tuliwapa matumaini watoto wetu kuwa wataingia kwenye sekondari za kata, ni kweli wameingia, lakini sekondari hazina walimu, maabara au vitabu vya kiada na ziada, hili nalo ni gamba. Wakati hayo yakisemwa, kwa njia ya uongo uliokubuhu, matatizo yote yanaelekezwa kwa Rostam, Lowassa na Chenge kuwa ndiyo waliosababisha mazingira magumu hapa nchini.

Tuonane wiki ijayo
deobalile@yahoo.com au 0784 404827

Je,

Wewe kwa ufahamu wako unadhani hayo yote hapo juu yamesababishwa na kina-nani?

Deo,

Ukiisoma hii makala yako haina hata chembe moja ya shaka kuwa, wewe uko kwenye payroll ya kina-ACHE !

Wewe Deo Balile, siku nyingine jaribu kuwa japo na chembe ya ustaarabu kwa kutowashambulia wale unaoamini hawako upande wako! kwani hii ni sawa na kutumwa ukamtukane mtu, kesi hapa itakuwa yako nasiyo ya yule aliyekutuma.

 
mwandishi amesita kutueleza ukweli kwamba ni mwajiriwa wa kampuni ya Rostam.... Habari corporation...... nina mashaka kama ana ubavu wa ku-balance uandishi wake labda awe tayari kufukuzwa kazi kesho yake.
 
Hii vita inayoendelea baina ya hawa wanamtandao ni kubwa, kama isipotumika busara ya wanaccm wakongwe kutatokea machafuko, ndani na nje ya ccm.
Inavyoonesha mstari umeshachorwa maadui wanajulikana, upande mmoja yupo JK na wapambe wake, upande wa pili wapo RA, EL na AC. hawa pia wana wapambe wao. Ni dhahiri kundi la pili lina nguvu sana, na lenye mtandao mkubwa unaoungwa mkono na wanaccm wa kizazi hiki kisicho cha TANU, kundi la JK linategemea sana wanaccm wazee, na viongozi wastaafu wa serikali. Nidhahiri kila kundi limejidhatiti kutokushindwa, na lile la pili liko tayari hata chama kife lakini wote washindwe, wakati la JK linajitahidi kuokoa chama. Mwisho wa hii vita kwa vyovyote vile si mzuri kwa ccm na taifa hususani tuelekeapo 2015.
Kama makundi yote yaking'ang'ania kubaki ndani ya chama, basi watashindwa uchaguzi mkuu, jambo ambalo hawapo tayari na hivyo hofu ya kuzuka machafuko.
Kama vita hii ikiendelea basi CCM itavunjika na kufa, taharuki itatokea maana serikali itayumba, na machafuko yanaweza tokea. Njia iliyo baki ni kundi moja kuanzisha chama mbadala cha siasa, jambo ambalo ni ngumu kwa kila kundi.
Ni muhimu sasa kwa vyombo vya usalama hususani UWT kuacha ushabiki na kuanza kudhibiti hali hii. Mzaha mzaha........, tutakuja juta mambo yakiharibika.
 
Back
Top Bottom