Mtanzania anaweza Kutajirika

"Utafiti pia umebaini kuwa tulidanganywa na serikali, Benki ya Dunia na serikali za nchi wafadhili kwamba, iwapo uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini utafunguliwa milango nchini, nchi itafaidika na itapata fedha nyingi, lakini yote hayo yaliyosemwa miaka kumi iliyopita hayajatimia," alisema Lissu. KIKWETE NAKUOMBA NIKO CHINI YA MIGUU YAKO. MPE MTU KAZI KUTOKANA NA TAALUMA YAKE NA USIMPE MTU KAZI KUTOKANA NA URAFIKI. ILI KULIEPUSHA TAIFA NA HILI BALAA LA VIHIYO LA SIVYO KUKUA KWA UCHUMI NI NDOTO
 
Alitoa mfano akisema, kabla ya makampuni makubwa ya uchimbaji madini hayajaruhusiwa kufanya kazi hiyo, wachimbaji wadogo walikuwa wakiingizia dola 37 milioni kwa mwaka tofauti na dola kati ya 13 milioni na 28 milioni zinazoingizwa sasa na makampuni makubwa.
 
Ufisadi nao je? Unachelewesha maendeleo ya Mtanzania mmoja mmoja?
 
Ufisadi nao je? Unachelewesha maendeleo ya Mtanzania mmoja mmoja?
Ndiyo,

Ufisadi wa viongozi unawakosesha watu nafasi ya kujiendeleza kwa namna nyingi sana; baadhi ya mifano yake ni kama ifuatavyo:

(a) Watu wanazuiwa wasitumie raslimali za nchi kwa vile fisadi keshaziuza kwa mzungu. Kwa mfano raia wanazuiwa wasichimbe madini kwa vile fisadi keshauza ardhi hiyo kwa mzungu. Sasa kama eneo liliuzwa ni la kijijini kwangu nilikozaliwa na kukulia, mnataka niende wapi kujitafutia maendeleo?

(b) Watu wanalazimishwa kulipia huduma mbalimbali kwa bei ya juu sana kuliko inavyopashwa ili kujaza pengo lilosababishwa na ufisadi. Hiyo inawafanya washindwe kujiwekea akiba na kujijenga mitaji ya kujiletea maendeleo.

(c) Watu wanakosa miundo mbinu sahihi kutokana na fisadi kuiba fedha za serikali ambazo zilitakiwa zijenge miundo mbinu hiyo. Kwa hali hiyo wanakuwa na ufanisi wa chini sana katika kujiletea maendeleo. Kwa mfano kutoka Sinza kwenda Kariakoo na kurudi inachukua karibu saa nne kwa vile hakuna barabara za kutosha; kama kungekuwa na barabara za kutosha ningetumia dakika 40 tu na kutumia hizo saa 3 na dakika 20 zinazobaki kujitafutia maendeleo binafsi.
 
Back
Top Bottom