Mtanzania afariki Italia

Ladslaus Modest

JF-Expert Member
Jun 27, 2008
635
20
ABDALLAH MJUME aka DULLAH au Jr, amefariki leo jumapili asubuhi katika nyumba aliyokuwa akiishi. Sababu ya kifo chake bado haijajulikana,ila taarifa fupi kutoka kwa watu waliokuwa nae inasema kuwa Dullah alikuwa Disco kabla ya kufariki. Wakati huo huo Katibu wa jumuiya ya watanzania anawatangazia watanzania wote wanaoishi Napoli kuwa kutakuwa na mkutano siku ya jumatatu saa kumi jioni kwa ajili ya taarifa kamili ya msiba na mipango ya mazishi,wote mnatakiwa kufika bila kukosa. (INALILLAH WAINA ILAH-RAJ'UN) RIP.

(Chanzo: MwanaKijiji.COM - Mtanzania afariki Italia)


Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen.
 
Poleni sana wafiwa. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana liimidiwe.

RIP Dullah.
 
R.I.P. Dulla Jnr.,

n1246250343_30237478_4312.jpg

"innaa lillaahi wainnaa ilayhi raaji'un"​
 
Last edited:
Jamani, andikeni kile tu mkijuacho! Acheni kupotosha maneno matakatifu!!! Kwani ni lazima muandike msichokijua???

Si sahihi kusema/kuandika: "INALILLAH WAINA ILAH-RAJ'UN" !! Bali hivi ni karibu sana na usahihi: "INNAA LILLAAHI WAINNAA ILAYHI RAAJI'UN"
 
Kaka nashukuru sana kwa sahihisho lako,hata hivyo ni kazi ya mola(Allah) binafsi ni kiwa kama binadamu sina pingamizi.
 
Poleni sana wafiwa, aliye na taarifa zaidi tunaomba atujulishe, kama marehemu mwenyeji wa wapi Tanzania? Jee ameacha mke/mtoto?, taratibu za mazishi nk.
Tunajumuika pamoja kumuomboleza mwenzetu aliyetutangulia katika haki.
Mungu amlaze pema. Amen.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom