Mtangazaji wa Channel Ten Afariki kwa Ajali!

picha plzeeeeeeeeeeeeeee!!

ramadhs.jpg


RIP Abdallah Ramadhani
 
Innalillah wa-inna ilaihi raji'un

Truly to Allah we belong, and truly to Him shall we return.

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

 
Mwili wa Abdalah Ramadhani, umewasili leo mchana ukitokea Deira Msumbiji na kuswaliwa katika msikiti wa Ilala na amezikwa jioni hii kwenye makaburi ya Kisutu.<br />
<br />
Mazishi hayo yamehudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo wanahabari na watu mbalimbali wakiwemo Iddi Azan na Zungu, pia kamanda Kova alikuwepo.<br />
Mungu aipumzishe roho ya Abdalah Ramadhani, mhala pema peponi, apumzike kwa amani -Amen.<br />
RIP Abdalah Ramadhani.
 
Ni masikitiko makubwa kumpoteza mtangazaji ambaye alikuwa na moyo wa kazi. Kwa niaba ya jamiiforum ninawapa pole Channel Ten kwa kumpoteza mchapakazi mwaminifu Mungu aipokee roho yake Amen
 
ramadhs.jpg


RIP Abdallah Ramadhani
Wanabodi,
Mtangazaji nyota wa Channel Ten, Abdallah Ramadhani, amefariki dunia leo kwa ajali ya gari huko Msumbiji akirejea nchini Tanzania kutokea Afrika Kusini, alikofuata Prado yake.

Habari hizi ni kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten ya saa moja usiku.

Huu ni msiba mwingine kwa Mtangazaji wa Channel Ten kupoteza maisha kwa ajali ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili. Herri Makange alimtangulia. Wote wameacha wajane na mtoto mmoja.

Abdalah Ramadhani alikuwa ni mmoja kati ya watangazaji wachache wa Channel Ten ambaye alikuwa ni ever smilling.

Poleni sana wanafamilia, Channel Ten na wanahabari kwa ujumla kumpoteza kijana huyu mahiri aliyekuwa amechipukia vizuri kwenye umahiri akielekea kwenye kubobea.

Mungu aipumzishe roho ya Abdalah Ramadhani, mhala pema peponi, apumzike kwa amani -Amen.
RIP Abdalah Ramadhani.
Rejea
Mwandishi ni Mtangazaji wa zamani wa External Service ya RTD.
Mabandiko mengine ya mwandishi kuhusu Watangazaji wa iliyokuwa RTD
P
 
Back
Top Bottom