Mtangazaji wa Channel Ten Afariki kwa Ajali!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,551
ramadhs.jpg

RIP Abdallah Ramadhani
Wanabodi,
Mtangazaji nyota wa Channel Ten, Abdallah Ramadhani, amefariki dunia leo kwa ajali ya gari huko Msumbiji akirejea nchini Tanzania kutokea Afrika Kusini, alikofuata Prado yake.

Habari hizi ni kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten ya saa moja usiku.

Huu ni msiba mwingine kwa Mtangazaji wa Channel Ten kupoteza maisha kwa ajali ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili. Herri Makange alimtangulia. Wote wameacha wajane na mtoto mmoja.

Abdalah Ramadhani alikuwa ni mmoja kati ya watangazaji wachache wa Channel Ten ambaye alikuwa ni ever smilling.

Poleni sana wanafamilia, Channel Ten na wanahabari kwa ujumla kumpoteza kijana huyu mahiri aliyekuwa amechipukia vizuri kwenye umahiri akielekea kwenye kubobea.

Update:
Mwili wa Abdalah Ramadhani, umewasili leo mchana ukitokea Deira Msumbiji na kuswaliwa katika msikiti wa Ilala na amezikwa jioni hii kwenye makaburi ya Kisutu.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo wanahabari na watu mbalimbali wakiwemo Iddi Azan na Zungu, pia kamanda Kova alikuwepo.

Mungu aipumzishe roho ya Abdalah Ramadhani, mhala pema peponi, apumzike kwa amani -Amen.
RIP Abdalah Ramadhani.
 
Wanabodi,
Mtangazaji nyota wa Channel Ten, David Ramadhani, amefariki dunia leo kwa ajali ya gari huko Msumbiji akirejea nchini Tanzania kutokea Afrika Kusini, alikofuata Prado yake.

Habari hizi ni kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten ya saa moja usiku.

Huu ni msiba mwingine kwa Mtangazaji wa Channel Ten kupoteza maisha kwa ajali ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili. Herri Makange alimtangulia. Wote wameacha wajane na mtoto mmoja.

David Ramadhani alikuwa ni mmoja kati ya watangazaji wachache wa Channel Ten ambaye alikuwa ni ever smilling.

Poleni sana wanafamilia, Channel Ten na wanahabari kwa ujumla kumpoteza kijana huyu mahiri aliyekuwa amechipukia vizuri kwenye umahiri akielekea kwenye kubobea.

Mungu aiweke roho ya David Ramadhani, mahala pema peponi, apumzike kwa amani..Amen.

RIP David Ramadhani.

Naoma Kusahishisha Si David Ramadhani aliyefariki ni Abdalah Ramadhani

RIP Abdallah Ramadhani
 
Naomba kujua yule si anaitwa abdallah ramadhani au ana majina mawili?nadhani kuna abdallah na david...aliyefariki ni abdallah ramadhani..........he is very young!amezaliwa 1982.............mungu mpumzishe kwa amani handsome dullah.....
mnakumbuka ule wimbo wao magic fm
abdallah ramadhani bombaaa eeh...eeh bomba eeh..
iga utepeteee!
amebeba madafu sijui alafu na t.shirt nyeupe!
 
Ayaa!! Ni mara ya mwisho kumsikia ni pale alipokuwa akihojiana na wanaharakati kuhusu kauli ya shimbo. Rip david

Kingi, kumbe sio David Ramadhani, ni Abdalah Ramadhani, hivyo uliyemuona ni David is still alive and kicking!
 
Naomba kujua yule si anaitwa abdallah ramadhani au ana majina mawili?nadhani kuna abdallah na david...aliyefariki ni abdallah ramadhani..........he is very young!amezaliwa 1982.............mungu mpumzishe kwa amani handsome dullah.....
mnakumbuka ule wimbo wao magic fm
abdallah ramadhani bombaaa eeh...eeh bomba eeh..
iga utepeteee!
amebeba madafu sijui alafu na t.shirt nyeupe!
Faithful, ni Abdalah Ramadhani, huyo David Ramadhani pia ni mtangazaji wa kituo hicho na ni mzima!.
 
mungu ailaze roho yake mahala peme peponi. jamaa alikuwa mtu poa saaana. nshapiga naye naye kazi ofisi moja huyu jamaa. kweli tumepoteza nguvu kazi moja mahili sana.
 
Wanabodi,
Mtangazaji nyota wa Channel Ten, Abdallah Ramadhani, amefariki dunia leo kwa ajali ya gari huko Msumbiji akirejea nchini Tanzania kutokea Afrika Kusini, alikofuata Prado yake.

Habari hizi ni kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten ya saa moja usiku.

Huu ni msiba mwingine kwa Mtangazaji wa Channel Ten kupoteza maisha kwa ajali ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili. Herri Makange alimtangulia. Wote wameacha wajane na mtoto mmoja.

Abdalah Ramadhani alikuwa ni mmoja kati ya watangazaji wachache wa Channel Ten ambaye alikuwa ni ever smilling.

Poleni sana wanafamilia, Channel Ten na wanahabari kwa ujumla kumpoteza kijana huyu mahiri aliyekuwa amechipukia vizuri kwenye umahiri akielekea kwenye kubobea.

Mungu aiweke roho ya Abdalah Ramadhani, mahala pema peponi, apumzike kwa amani..Amen.

RIP Abdalah Ramadhani.

RIP Rama.
 
Back
Top Bottom