BOB OS
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 3,427
- 6,786
Na Markus Mpangala
WIKIiliyopita tuliona jinsi Kirilo Japhet alivyokwenda UN kuhutubia. Naye MwalimuNyerere alikwenda kuhutubia UN mwaka 1955 na baadaye mwaka 1956, ikiwa ni miakamitatu tangu Kirilo Japhet ahutubie.
Katikakipindi hicho TANU ilikuwa imefungiwa kufanya shughuli za kisiasa na utawala wamkoloni wa Kiingereza. Japhet Kirilo alizaliwa mwaka 1921 na kufariki duniamwaka 1997.
Jinalake kamili ni Kirilo Japhet Ayo. Alizaliwa katika kijiji cha Poli, Nkoaranga ambaposasa ni wilaya ya Arumeru. Baba yake aliitwa Nganayo au maarufu Ngura Ayo,ambaye alikuwa kiongozi wa jadi kijijini hapo na wakulima wa zao la kahawa waMeru.
Kiriloalifariki dunia Mei 30, 1997, na kumwachia mkewe, Ndeleto Kirilo watoto sita wakiume na wanne ni wasichana. Bahati mbaya watoto wawili wa kiume walifarikidunia.
Watotowake wawili wa kiume Zakaria Kirilo na Jefferson Kirilo wanaishi Marekani. AnnaKirilo ni mtoto wake wa kike ambaye anafanya kazi katika Hospitali ya MountMeru.
Katikamaisha yake Kirilo alifanikiwa kupata elimu yake kwa miaka nane na alisomea ualimukatika chuo cha Marangu. Baadaye alifanya kazi serikalini akianzia Mpwapwa, mkoaniDodoma na Arusha.
Wakatialipoteuliwa kuwa mwakilishi wa wakulima waliokuwa kwenye mgogoro mjini Meru,Kirilo alikuwa na miaka 31 tu. Pia alikuwa mashuhuri wakati akiongoza tawi lachama cha TAA akiwa Katibu Mkuu.
Kiriloanaelezwa kuwa shupavu katika ujenzi wa hoja katika vikao mbalimbali vya Barazavya wilaya kuanzia mwaka 1950 na kuwa alama bora kwa wananchi wa Meru.
Babayake Ngura Ayo licha ya kuwa kiongozi wa kijadi, pia alikuwa mweka hazina wakanisa huko Meru. Mzee Ngura Ayo anatajwa kuwa mkulima wa kwanza kununua Trektamwaka 1935 na kuwa mkulima wa kisasa.
Dk.Mesaki anamwelezea Kirilo Japhet kama miongoni mwa wapigania uhuru wasiokuwa nawoga kipindi hicho. Alifanya kila njiakuhakikisha waafrika wenzake wanapata haki zao za msingi.
Hatahivyo kama walivyo viongozi wowote, Kirilo Japhet hakukosa tuhuma kutoka kwawakulima wenzake na wananchi wa Meru.
Marabaada ya kuwasili Meru akitokea Marekani Kirilo Japhet alituhumiwa kutafunafedha za misaada za ushirika. Jambo jingine baya lililowahi kumtokea ni kitendocha kumiliki ekari 60 za ardhi, na kumfanya Kirilo kuwa mkulima wa kiwango borawakati huo.
Hatahivyo ardhi hiyo ilimsababishia matatizo makubwa na kungarimu nafasi yake yauongozi ndani ya chama na ubunge kwa madai alikuwa bepari (mnyonyaji).
“Nilikuwambunge kati ya mwaka 1971 na 1974. Nilituhumiwakuwa na fedha nyingi, na nililazimishwa kuuza mashamba yangu ikiwa ni sharti lakuendelea na ubunge.
“Lakininilikataa sharti hilo kutokana na kiasi na faida za kulima kahawa kwa wakulimawa Meru kilikuwa kikubwa. Hivyo alichagua kuwa mwakilishi wa wakulima wa kahawakatika maeneo mbalimbali Afrika,”
Kiriloalikuwa mstari wa mbele kuendesha harambee ili kupata fedha za kuwasomesha njeya nchi vijana wa Meru. Miongoni mwa walionufaika na harambee hizo ni PeterKishuli Pallangyo, Eliawira Ndossi, Moses Ndosi, Mathias Kaaya, Mike Urio, NdewiraKitomari.
HivyoKirilo alichagua kuishi na wakulima wenzake kuliko sharti la kuuza mashambayake (AMHT3, 1988). Kwa utawala wa kikoloni, Kirilo Japhet alikuwa raia mkorofina mwanasiasa hatari.
LakiniKirilo alikuwa akifanya kazi kubwa ya mapambano ya uhuru na wakati wa shughulizake aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali hapa nchini chini ya mwamvuli waTANU.
Kiriloalikuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU katika jimbo la Kaskazini. Kirilo Japhetbaada ya kutoa hotuba yake Umoja wa Mataifa alibaki nchini Marekani kwa mwakanzima akijifunza mambo mbalimbali.
Kiriloalifanikiwa pia kukusanya michango mbalimbali ya kifedha kutoka nje ya nchi nakujenga shule za msingi, sekondari na vyuo vya ufundi kwa wakazi wa Meru. Kirilopia alishiriki kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na Jenerali Mirisho Sarakikya.