Mtandao/internet kwenye tafiti na uchunguzi

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Hivi ninavyoandika sasa hivi watumiaji wa Mtandao nchini Tanzania ni 676,000 hiyo ni asilimia 1.6 ya idadi ya Raia wote wa Tanzania wakati huo huo watumiaji wa Mtandao jamii maarufu kuliyo yote duniani kwa sasa nchini Tanzania ni 141,580 hiyo ni asilimia 0.3 kwa watumiaji wa mtandao kwa Tanzania hizo ni takwimu mpaka mwezi juni mwaka 2010 toka ITU , mwaka 2009 idadi ilikuwa 520,000 na ni asilimia 1.3 tu ya watanzania walikuwa wanatumia mtandao .

Idadi inaweza kuongezeka kutokana na matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyomwezesha mtu kuweza kuunganishwa na mtandao kama simu za mikononi , komputa na vifaa vingine vingi vya mawasiliano ambavyo ni vya kubeba ambavyo pia vinawezesha taarifa na habari kusambazwa kwa kasi zaidi na wepesi toka eneo moja kwenda kwingine toka mtu mmoja kwenda kwa mwingine .

Kwa sasa huduma za internet zimekuwa rahisi zaidi na gharama nafuu kutoka kwa wauzaji wa vifaa mpaka wale wanaotoa huduma za aina hiyo kwenye migahawa ya internet maarufu kama internet cafรฉ , kwa wale watumiaji wa majumbani , maofisini na kwenye simu kuna vifurushi wanavyoweza kununua na kutumia huduma za internet kwa kadri ya ukubwa wa kifurushi chake .

Ukuaji huo pamoja na huduma za internet kupunguwa zimechochewa sana na kuingia mkonge wa mawasiliano nchini kati ya mwaka 2009 na 2010 ambao ulileta mapinduzi hayo katika mawasiliano haswa yanayohusu mitandao kuanzia kwenye simu na vifaa vingine kama komputa lakini gharama za mawasiliano ya kimataifa kati ya Tanzania na sehemu nyingine hazijapungua sana kutokana na sababu kadhaa ambazo zinaweza kuzuilika kama baadhi ya mambo yakiwekwa sawa .
Pamoja na kukuwa kwa huduma za mawasiliano Tanzania na upunguzaji wa gharama za mawasiliano hapa nchini kuna upande mmoja ambao nimeona niuongelee kwa kifupi ili kuweza kuleta jumuiya ya watazania na wana afrika mashariki katika njia moja ambayo inaweza kuwakomboa na kusaidia wengine katika shuguli zao za kila siku haswa zinazohusu biashara na mawasiliano mengine kwa njia ya mtandao .

Kama neno lenyewe Internet ย– International Network , Mtandao wa Kimataifa linavyomaanisha , muungano wa mitandao ya komputa duniani unaowezesha watu kwa mamia na maelfu kuungana na wenzao walio sehemu mbalimbali duniani katika shuguli mbalimbali kama biashara , elimu , mawasiliano binafsi , utafiti na mengine mengi .

Utumiaji wa njia za zamani za mawasiliano na huduma karibu zote sasa hivi zinaweza kuwezeshwa kwa kutumia Internet , kama mawasiliano ya Barua ambapo sasa kuna barua pepe , huduma za burudani kama muziki na sinema ,sasa hivi kuna tovuti za kuweza kuangalia video na kushusha kwa ajili ya kuangalia baadaye au kusikiliza , sasa hivi ukitaka kufanya mkutano na watu wa mbali si lazima tena kwenda ulaya au japani mtandao unakuwezesha kufanya yote hayo na zaidi kadri ya siku zinavyozidi kwenda .

Kwa wafanyabiashara na masomi mbalimbali kupata taarifa za kweli , kwa gharama nafuu zinazoenda na wakati kwa njia ya mtandao imekuwa muhimu sana kwa ajili ya shuguli zao za kila siku .

Mfanyabiashara wa kisasa lazima ajue watu anaofanya nao kazi na mashirika anayofanya nao kazi haswa walio upande mwingine wa dunia , masoko yao na aina za biashara wanazofanya na madhara mengine yanayoweza kutokana na muingiliano huo wa kibiashara au kisomi kwenye shuguli .

Mtandao wa kimataifa / Internet inawapa wafanyabiashara na wasomi njia nyepesi zaidi za gharama nafuu na zinazoenda na wakati katika ufanyaji wao wa kazi haswa katika kutafuta taarifa na mawasiliano katika teknologia na tekinologia hizi nyingi hazijulikani kwa wengi au wanajua lakini wanatumia kidogo sana au hawatumii kabisa au wanaotumia hawaelewi kwa kiwango cha kutosha ili kuweza kufanikisha malengo yao ya kikazi .

Ili kuweza kufanikisha malengo ya kazi au shuguli yoyote kwenye mtandao pindi unapojiunga tu kwa ajili ya kazi zako kuna mambo unayotakiwa kujua na kuelewa haswa njia za kutafuta vitu na kuwasiliana , kutangaza na kuuza bidhaa mbalimbali , kuweka mawasiliano yako na jinsi mawasiliano yako yanavyoweza kutafutwa kwa ajili ya shuguli nyingine za biashara au uhalifu .

Kwenye masomo haya utajifunza programu mbalimbali na njia mbalimbali mtu anazoweza kutumia katika kufanikisha malengo yake pindi anapokuwa ameunganishwa kwenye mtandao kama ni mwanafunzi , mtafiti , mfanyabiashara na wengine wengi wanaopenda mtandao na maendeleo yake .


ITAENDELEA

YONA F MARO

0786 806028
 
Back
Top Bottom