Chokochoko
JF-Expert Member
- Oct 15, 2011
- 438
- 183
hili neno kwa hela hiyo inatosha kuweka na kinywaji cha kushushia na itakulipa tuu.Samahani kama ntakukwaza coz sijui imani yako.Biashara ya kibanda cha kiti moto inalipa vizuri sana hata ukiwa na mtaji wa milioni 2 tu.Hakikisha unapata vijana wawili sharp na eneo lisilo rasmi saana na iwe ni kwenye viunga vya mji kama uko Dar namaanisha maeneo kama Tabata,Ukonga ambayo mahitaji ni makubwa ila outlets bado ni chache na hayana imani kali wengi.Ukipata eneo la kibanda hata kama utalipa elfu 50 kwa mwezi ukapata na friza ya mtumba ya laki 2 kwa ajili ya kutinzia then jiko la gezi linaweza kukugharimu laki moja na structura ya kuuzia mathalani lako 2 au 3 hivi coz haipaswi kuwa rasmi sana though hygiene iwe ni driving factor.
Hii una uhakika wa kuwa unaiona hela yako kila siku na kuamua ipi irudi na ipi usevu au utanue biashara zaidi.