Governor of Bettors-GB
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 9,871
- 8,889
Zanzibar Spices
Hao wanaokata tamaa kufanya biashara za kilimo niwazee wa simple gum boots kwao sum na adui
Hahaha,nikweli mkuu.
Yaani unakuta mtu analamikaa,ukiagalia changamoto zenyewe ni zakawaida.Wakati huo huo kuna changamoto watu wanakumbana nazo ukiambiwa unaweza kusema kweli hakuna pesa rahisi na wengine hukimbia kabisaa hata kama walikuwa na pesa kidogo ya kuboost.
Ila ukiona shamba la mwenzio limependeza basi unaona kama vile limeletwa na malaika,unaweza kukuta shamba hilo unaloona limependeza,miaka miwili nyuma mwenye shamba alikula hasara kubwa kabla ya kujipanga upya.Sasa unakuta baadhi yetu tunachukulia mafanikio ya kilimo kwa kukuta shamba la mwenzio limenawiri vizuri na kuona kwamba na wewe ukianza tu inakuwa kama hivyo.
Wakulima wana siri kubwa saana,ndio maana raha ya kilimo ni kwamba ingia ucheze rhythm ya wakulima ndio utajua.Unaweza kuchukua hatua zoote lakini kikakupiga vile vile,maana dizasta nyingine za kilimo zinakuwa hazina namna wala formula.
Tena labda niwaambie kitu kimoja,mkulima wa kweli ambae Kilimo kimo kwenye dam yake na dhamira yake ya kweli,basi ni kama TEJA mla Unga au zaidi ya teja mla unga.Maana akili yake,mwenendo wake,maisha yake,yoote yanakua kikilimo kilimo tuu.Anaweza kupoteza mazao shamba lote either kwa Janga la moto au magonjwa ya mimea,lakini unamkuta amekaza,na tabasam linakujia kama vile hana shida vile au hana tatizo.Ila moyo wa Ujasiri wa dhamira ndio unampa faraja.
Sasa kutana na yule anaelima kwa kuona shamba la mwenzie na kutaka na yeye afanikiwe kaka mwenzie kirahisi.Akipata tatizo tuu,basi huwezi amini anachanganyikiwa kabisa.Na anaweza kukitukana kilimo na wakulima wote.
Na wengine huishia kusema kwamba Kazi ya Kilimo cha mashamba lazima uwe mshirikina ili shamba lako lipate mazao mazuri.Yaani ndio akili ya wakulima waigaji.Na unaweza kukuta anapolima yupo peke yake hakuna mwingine Karibu.
Na kama mkulima wa dhati na umeamua kujiripua,basi amini usiamini,kama tatizo likitokea basi usitafute mtu wakukufariji ambae sio mkulima,atakupoteza.
Mkulima hufarijiwa na mkulima mwenzie.Namkulima akipatwa na Tatizo basi wa kwanza kumfikishia ni Mkulima mwenzie.
Sasa unakuta mtu amelima then ikitokea tatizo au hasara anamtafuta mtu ambae mambo hayo sio yake ilimradi tu yeye anaona ndio wa karibu yake,we unategemea nini zaidi ya kwamba atakuambia oyaa we umeona nani kalima hapa Tanzania amefanikiwa,weee vipi acha ujinga wako,we huoni watu wanalima na hawana pa kuuzia,we mjinga sana,nilikuambia mie,na nilikuwa nakuangaliaa unavyohangaika na kulima,watu wanalima kijijini hukoo na sio mjini weee vipi,mjini biashara kijijini kulima,we nimekuambia fungua duka la sim tupige hela,umekalia kilimo.Na upuuzi mwingine teleeee.Sasa na wewe ukiambiwa hivyo,basi ukimkuta mkulima mwenzio amakumbana janga kama lako basi unamwambie the same story za kejeli,mwisho wa siku inakuwa kama vile chain fulani,ya kwamba mie nililima lakini kilimo hakina tija,ni hasara,unapoteza muda na mambo meengi,wakati ukweli ni kwamba Umekimbia kilimo na changamoto zake.
Sasa lazima pia uangalia na watu gani wanaokuzunguuka.
Huwezi kuwa na dhamira ya kulima au kufanya kilimo then ukataka ushauri kwa mtu asie mkulima.Au mtu ambae anasikia tu watu wanalima.Lazima utapata ushauri sio.
Na pindi linapotokea tatizo au hasara yoyote kwenye Kilimo,basi kuwa mbali sana na familia na ndugu na jamaa katika taarifa au tathmini ya kilimo chako.Nalisema hilo kwa kuwa nimewahi kuliona kwa Mwenzangu.Yaani alilima kwa kukodi sehem,basi alipopata tatizo ndugu zake ndio walikuwa wakwanza kumlaumu na kumkatisha tamaa kwa maneno ya kejeli,maana wakati analima na alipokuwa amefanya maamuzi hayo,walitokea ndugu zake waliotaka walipiwe ada za vyuo vya ufundi,wengine walitaka mitaji,na wengine kesi za ajabu ilimradi walijua ndugu yao alipata hela ya Udalali wa kiwanja.
Basi alipopatwa na tatizo la ng`ombe kukata njia na kufamia shamba,basi huwezi amini walishangilia ile mbaya.Yaani jamaa unamuonea huruma,maana mie nililima Pilipili na yeye alilima Nyanya.
Maana mbaya zaidi hakujua ni mifugo ya nani,maana hakukuwa mtu shambani muda ule.Sasa kumbe jamaa mmmili wa ng`omber wale alikuwa mstaarabu,kama wiki mbili hivi wakulima wenzie tukajiunga na kufanya tathmini kujua nani alifanya hivyo.Na tukaweza kumjua,na alikuwa mzee wa Kiarabu na alilipa pesa ya mazao kamili.Na wakati huo tulikuwa tumechangishana pesa kama ujirani mwema kama majirani ili alime tena.
Baada ya kumpata mmiliki wa mifugo hiyo,Basi jamaa hajaamini kama anaweza kulipwa Nyanya za mwezi na nusu kwa pesa kamili.Tumekuwa nae kama ndugu.Na anasema kwamba haamini kama ndugu zake walikuwa na kinyongo namna ile ila baada ya tukio ndio alijua.
Na alipotata hizo pesa alikaa kimyaa,wao wakaona amefulia,kumbe shamba tulimchagia upya na pesa za kuliwa mazao alilipwa pesa nzuri kweli.Na alichofanya ni kwamba alikodi shamba sehem nyingine na ni mkulima wa level nzuri sana kwa ukanda wetu ule,na shamba hili la ziada alilokodi hakuna ndugu hata mmoja analolijua zaidi ya sie,jamaa yeye ameenda mbali zaidi maana hata mkewe hajui,aisee ana hasira kweli kwa yaliyomkuta.
Sasa rafiki wa Mkulima ni mkulima mwenzie,ni bora rafiki mkulima mwenye roho mbaya kuliko ndugu ambae sio mkulima mwenye roho nzuri,maana hawa ni rahisi sana kubadilika muda wowote na kukatishana tamaa pale unapopatwa na tatizo.Lakini mkulima wa kweli atakuwa na roho mbaya lakini atakupa njia tu,then mbele utajiongoza mwenye.
Ujumbe kwa Vijana wa Kiume,Inasikitisha sana wanawake ndio wanoongoza kuwa na roho ngumu,na masugu balaa kwenye kilimo hasa ufugaji.Idadi yao inakuwa kwa kasi saana na katika kila kina mama wastan 10 ambao ni wakulima ni wawili tu ndio utakuta wamekimbia changamoto za kilimo au ufugaji,ila kwa wavulana kati 10 unaweza kukuta 7 au sita wamekimbia kilimo au ufugaji hicho.
Na hii inaonekana kwamba kina mama wanaamini kwamba kesho nayo ni siku,mie nikiona sehem la Shamba au mifugo yupo mwanamama,basi huwa hata siulizi najua hapo huyo ni milionea mtarajiwa.Yaani masugu sana aisee.Na pia wepesi sana kufuata ushauri na wengi wa kinamama sio watu wa kubahatisha ndio maana wengi wanafanikiwa.
MUNGU ULIEHAI,UTUPE NA UTUJAALIE NA SIE TUNAOTAKA KULIMA ZAIDI NA TUNAOTAKA KUANZA KILIMO, MOYO WA UVUMILIVU WA CHANGAMOTO ZA KILIMO,NA PIA MUNGU UTUPE MAAMUZI SAHIHI YA AINA YA KILIMO KULINGANA NA DHAMIRA HUSIKA.UTUONGOZE KATIKA UAMINIFU KWAKO NA KUAMINI KWAMBA WEWE NDIO MSIMAMIZI WA KILA JAMBO TUNALOAMUA NA NDIO MUONGOZAJI WAKILA JAMBO LINALOKUWA.NA PIA NDIO MTATUZI WA KILA TATIZO AU CHANGAMOTO INAYOTOKEA KWA KUTOA NJIA SAHIHI YA UTATUZI NA FARAJA,TUNAKUOMBA UTUKINGE NA KUKUKOSEA KWA KULAUMU MATOKEO HASI KATIKA MAISHA,ILA TUELEKEZE KATIKA IMANI KWAMBA TUTAMBUE HUO WOTE NI UFALME WAKO KATIKA MAJARIBU,UTUJAALIE TUSHINDE MAJARIBU BILA KUKUKOSEA KWA JINA LAKO NA UTUKUFU WAKO WA MILELE."AMEEN"