Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Jenga Choo ya kulipia eneo la Kariakoo. Utakuwa na uhakika wa kurejesha gharama zako ndani ya muda mfupi kama ifuatavyo:

Wateja - Akina mama (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
- Akina baba (150 * 100/= * 30days) = 450,000/=
- Watoto/vijana/wanafunzi (200 * 100/= * 30days) = 600,000/=
JUMLA KWA MWEZI 1,650,000/=

Kwa mwaka (19,800,000), kwa miaka kumi (198,800,000/=).

Yaani baada ya miaka kumi utakuwa millionea mkubwa sana, na usisahau kurudi hapa JF na kutushukuru.

NB: Kumbuka, uzuri mmoja kwa biashara hii, haina suala la mvua wala kiangazi. Kila siku biashara inaenda.

...wazo zuri, ukizingatia makontena yapo ya kumwaga (mobility) leo wateja kariakoo, wikiendi uwanja wa saba saba, au uwanja wa taifa.

...modification ndogo ndogo tu. Shukran.
 
...haswaa!... hapo umemnena kila kitu. Shukrana sana Malila, nimepokea michango ya kutosha (mawazo), ilobakia sasa ni utekelezaji! Shukran.

Mbu!
Acha huu mjadala uendelee mana bado michango ya mawazo inazidi kuja,wengine tunaelemika pia kwenye hili. Mada safi kweli
Nimenote down idea zote za biashara nilizoziona kwenye thread hii, huwezi jua bwana one day yes nikifikiria biashara. Imenisadia kwakweli binafsi.

Kwako wewe,nakutakia mchanganuo mzuri katika kujipanga kuanzisha hivyo biashara utakayodhamiria.
 
Kuna huduma ya massage nafikiri ukiianzisha hii na ukachagua vimwana poa dah mzee utatukamata wengi hapo wazee wakujiexpress, we weka waarabu na wahindi na watoto wa A-town wale weupeeeeeee utamake sana mkuu.
 
ha ha haa... sawa mazee, wewe unahamasika zaidi na huduma za kijamii hususan kwenye hii miili yetu iliyojaa stress za mafisadi, umeme, nk...

Massage parlour Bongo ndio zinaitwa Saloon za kiume? haya bana, kidogo kidogo tutafika tu :D
 
Kuna huduma ya massage nafikiri ukiianzisha hii na ukachagua vimwana poa dah mzee utatukamata wengi hapo wazee wakujiexpress, we weka waarabu na wahindi na watoto wa A-town wale weupeeeeeee utamake sana mkuu.

Kuna wajanja wanawa-import kutoka asia ...ni balaa! (Professional masseuses)
Inakuwa bomba zaidi kwenye mahoteli
 
Mbu!
Acha huu mjadala uendelee mana bado michango ya mawazo inazidi kuja,wengine tunaelemika pia kwenye hili. Mada safi kweli
Nimenote down idea zote za biashara nilizoziona kwenye thread hii, huwezi jua bwana one day yes nikifikiria biashara. Imenisadia kwakweli binafsi.

Kwako wewe,nakutakia mchanganuo mzuri katika kujipanga kuanzisha hivyo biashara utakayodhamiria.

...Spot on BJ,

hata mimi nitafurahia wakijitokeza wachangiaje wengine wengi zaidi. Nimefarijika mawazo toka sehemu mbali mbali hasa kuhusiana na biashara zinazowezekana kuanzishwa Bongo kwa mtaji wa 10m/=

kuhusu 'Products' nishapata mawazo, Kasheshe itabakia location, na market, na muda muafaka wa kuanzisha biashara hiyo.

Mjadala na uendelee kwa faida ya wote, bado tunaelimishana nikiamini kuna memba wengine watakuja na michango mizuri zaidi!
 
Mbu Hongera kwa kuamua kuwa MJASIRIAMALI,nakupa ushauri kwenye kilimo
Unaweza ukaenda kwenye mikoa yenye rutuba na mvua za uhakika(Mbeya,Morogoro,Iringa,Ruvuma,Tanga) ukakodi au kununua mashamba na kulima mazao ya chakula (Mahindi,Mpunga,Mihogo,Maharage) ukishavuna unasafirisha kwenda kwenye mikoa ambayo ina upungufu wa chakula kama Mtwara,Lindi,Dar,Kigoma na unaenda kuuza kama mambo yatakwenda sawa mvua zikinyesha na mazao yakapata huduma nzuri biashara inalipa mno
Njia ya pili unaweza kwenda kununua mazao vijijini punde tu wakulima wanapovuna huko vijijini then unakuja kuyauza mjini
 
...wazo zuri Belo, lakini hapo nimepatwa na wazo la kuwa middleman. yaani nakwenda kwa mkulima nanunua, kisha nakwenda kuuza jumla. Au unaonaje? Kununua Shamba, ulimishe, mbolea kisha usubirie mvua duh! kwa mtaji wa 10m/= nikujitolea mhanga mno, au?
 
Belo, mambo ya kilimo kwa sasa yana risk kubwa sana. Mbu anaweza akapoteza 10m zake. Haya mabadiliko ya climatic condition sio mazuri, mara mwaku huu mvua mara mwakani hakuna. Kama unamshauri kuhusu kununua mazao yalikuwa tayari yamevunwa hiyo inaweza kuwa afadhali kwa upande fulani.
 
Mbu ndio maana nimetoa njia mbili Kulima au Kununua na kuuza nai kweli hilo la kulima linategemea sana na hali ya hewa but ndio maana nimesema chagua maeneo ambayo ni mazuri
 
ningepata mimi hizo milion kumi,
ningewekeza ktk ardhi hasa ktk mitiki maana kama nitaweka uangalizi mzuri basi nitakuwa na uwezo wa kukopa benki pesa nyingi baada ya hapo in two years time.
analisisi yake ningeipata baada ya kuwatafuta wataalam wa michanganuo na kuwamegea laki tano waniandikie mchanganuo wa hii kitu.
ah nawaza kwa sauti hapa ops!
 
...wazo zuri Belo, lakini hapo nimepatwa na wazo la kuwa middleman. yaani nakwenda kwa mkulima nanunua, kisha nakwenda kuuza jumla. Au unaonaje? Kununua Shamba, ulimishe, mbolea kisha usubirie mvua duh! kwa mtaji wa 10m/= nikujitolea mhanga mno, au?

Kilimo cha umwagiliaji.
Shamba lisiwe mbali sana na mlaji (to minimize transport cost).

Je ukipata mnunuzi hata kabla hujaweka mbegu chini?
Muhogo mfano. Kuna viwanda vya nguo vinahitaji watu kuingia nao mkataba kuzalisha muhogo tani kadhaa. Kuna challenge zake. (You're not planning to avoid challenges, are you?)
 
Mzee tafuta eneo zuri nunua viwanja tu 2 kila kimoja 5m. Then subiri tu baada ya mwaka utauza zaidi ya mara 2!

Ardhi/viwanja Dar hupanda bei kila sikU!
 
ningepata mimi hizo milion kumi,
ningewekeza ktk ardhi hasa ktk mitiki maana kama nitaweka uangalizi mzuri basi nitakuwa na uwezo wa kukopa benki pesa nyingi baada ya hapo in two years time.
analisisi yake ningeipata baada ya kuwatafuta wataalam wa michanganuo na kuwamegea laki tano waniandikie mchanganuo wa hii kitu.
ah nawaza kwa sauti hapa ops!

Thanks msanii,

Wazo la kuwekeza ktk ardhi hasa miti (mitiki,milingoti,pines) ambayo growth rate yake ni kubwa na ina good future ni bomba sana. Hizo hela ni nyingi sana kwa shughuli za kuwekeza ktk miti ie mitiki kwa kuanzia. Siku ukipata hela kidogo kama milioni moja hivi nitafute,nitakupa mchanganuo kwa vitendo bure ushindwe mwenyewe.

Kwa sasa,tujitahidi kukamata ardhi ndugu zangu,tuendako kubovu sana.
 
Mkuu
Nimeahidiwa na mwana JF mmoja hapa hiyo milioni moja.
je nitakupataje nipate huo mchanganuo mkuu? nitumie nitumie kwenye PM kama unaweza pls.
nipo siriaz
 
Mzee tafuta eneo zuri nunua viwanja tu 2 kila kimoja 5m. Then subiri tu baada ya mwaka utauza zaidi ya mara 2!

Ardhi/viwanja Dar hupanda bei kila sikU!

...dah, usinitie uchungu ndugu yangu, kuna kiwanja pale kibada (kigamboni) nilikionea ubahili mwaka 2005 kulipia milioni tatu na kidogo, leo hii kinauzwa 8m/=
 
ningepata mimi hizo milion kumi,
ningewekeza ktk ardhi hasa ktk mitiki maana kama nitaweka uangalizi mzuri basi nitakuwa na uwezo wa kukopa benki pesa nyingi baada ya hapo in two years time.
analisisi yake ningeipata baada ya kuwatafuta wataalam wa michanganuo na kuwamegea laki tano waniandikie mchanganuo wa hii kitu.
ah nawaza kwa sauti hapa ops!

...on a serious note, faida ipo kwenye ardhi na miti. Wazo zuri sana! kuna shamba moja maeneo ya kimanzichana linashangaa shangaa tu,...inabidi niipande hiyo mitike kwa wingi (kama ikikubali), inaonekana deal la nguvu hilo.

Mitike, na ufugaji ng'ombe wa maziwa na kuku wa kienyeji ndio mawazo yaliyonivutia kwa sasa. Nitaanzaisha kama 'kijiji' hapo, nikishaweka jamaa zangu wa Kinyamwezi wawili watatu na wake zao maisha yanaendelea.
 
...dah, usinitie uchungu ndugu yangu, kuna kiwanja pale kibada (kigamboni) nilikionea ubahili mwaka 2005 kulipia milioni tatu na kidogo, leo hii kinauzwa 8m/=
ukome na ubahili wako
ila ulifanya uamuzi sahihi kwani hivi sasa ungekuwa miongoni mwa watakaolia kwani ule mradi wa mji mpya wa kigamboni upo hadi kule kwa hiyo ingekula kwako mkuu.
 
...we acha tu. Ndio kusema wale waliopewa hati za viwanja pale kibada hawana lao tena? nimeshaiona mpaka master plan ya eneo hilo, sidhani kama watavunjiwa!

Ardhi mali acheni tu,...ngoja niangalie usawa wa Mkuranga na kimanzichana huko!...
 
Msanii/mbu

Kama mnamaanisha ktk biashara hii ya miti,nipe e mail address zenu halafu tuone tutafanya nini.Sitaki hela ya mtu.Mimi nilishituliwa na mshikaji bure na mimi nitakusaidia bure. Michanganuo yenu mtafanya baadae mkipenda. Mimi sikufanya hiyo michanganuo.
 
Back
Top Bottom