Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mi mchango wangu ni huu ufuatao:
Kwanza nawashukuru wote mliochangia na pia mtoa mada.
Kwa hiyo million 10 unaweza kufanya biashara ya bajaji kwa miji kama mbeya, Iringa na Bukoba ni biashara inayolipa pia competition yake ipo chini...Mimi nimewahi kufanya kama dereva wa bajaji by mwaka 2012 niliona jinsi hiyo kitu ilivyo ila inahitaji usimamizi na kwa mtaji wako inabidi uchanganye wakati wa kununua hizo bajaji yaan nununua baadhi used na baadhi mpya hata ukianza na bajaji tatu si mbaya pesa itarudi
Pia kuna idea ya kufungua hizi college za masomo ya biashara na social studies pia kibongobongo naona it is a high rate growing business na watu wanazipenda coz we mwenyewe ni shaid jins wazazi wanavyosumbuka na watoto baada ya kumaliza form 4 na 6 na kukosa sifa au nafasi vyuoni...angalizo usifanye Hii kitu Dar competition ni kubwa mno coz kuna utitili wa colleges ila mikoani huku mambo safi kabisa
Mwisho kama utaipenda hiyo idea ya pili na kutaka kuifanya mi sina mtaji ila niko tayari kuisimamia na kukupa mwongozo na eneo na returns zake na jinsi ya kuiendesha najua una shaka na walimu hao very cheap tunawapata na mi ni mmoja wa walimu wazuri kwenye issue za business admin..
Mawazo yangu ni hayo

asante sana bk@ ntakutafuta
 
Fanya biashara ya mazao masasi mtwara unanunua kwa tsh 500 unauza kwa tsh 770 unatoa gharama za yshuru chama cha msingi 50/kg halnashauri 25/kg usafiri 40/kg onayobaki zidisha kwa mzigo utakaonunua ndio faida yako unaweza kukusanya tani 20 kwa wiki kama mzunguko umesimama vixuri je haujatoka hapo.
 
quote_icon.png
By Mgombezi

Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
 
Safi, ng'ombe ni uzalishaji mzuri sana!

Fuga usiache kwa kuwa hata samadi inauzwa au kama una shamba sehemu hii itaongeza mavuno ambayo yatasaidia kutunza familia yako na chakula cha mifugo yenyewe.
 
Fanya biashara ya mazao masasi mtwara unanunua kwa tsh 500 unauza kwa tsh 770 unatoa gharama za yshuru chama cha msingi 50/kg halnashauri 25/kg usafiri 40/kg onayobaki zidisha kwa mzigo utakaonunua ndio faida yako unaweza kukusanya tani 20 kwa wiki kama mzunguko umesimama vixuri je haujatoka hapo.
oh yes ....hapo ni mazao gani yanapatikana masasi mtwara?
 
quote_icon.png
By Mgombezi

Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:

Ujenzi wa banda = Ths 500,000/=
Manunuzi ya Ngombe 5 x Tsh 900,000 = Tsh 4,500,000/=
(Ngombe utawanunua wakiwa na mimba ya miezi 6)
Kuwahudumia ng'ombe kwa miezi mitatu kabla ya production = Tsh 1,500,000/=
(inahusisha mshahara kwa wafanyakazi wawil + chakula + madawa)

Jumla = Tsh 6,500,000/=

Baada ya Miezi 3;

UZALISHAJI:

Ngombe hawa watakuwa wakitoa maziwa si pungufu ya lita 5 kwa asubuhi na jioni kwa kila ng'ombe. Hivyo uzalishaji kwa siku utakuwa lita 10 kwa siku kwa ng'ombe.

MAPATO

Lita 10 x Ng'ombe 5 = lita 50 kwa siku x Tsh 1000 (bei ninayouza mimi hapa) = Tsh 50,000 kwa siku
Mapato kwa mwezi = Tsh 50,000 x 30 = 1,500,000/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi = Tsh 600,000/=

Faida = Tsh 900,000/= kwa mwezi

BAADA YA MIAKA 5:

Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.

safi sana nmependa ulivyoelezea
 
Mie naona Mbu uwekeze kwenye mfumo wa maji safi kule bongo, nenda sehemu ambazo hawana maji ya bomba na ukachimbe visima vya kutumia mota ya umeme ili wapate maji safi badala ya kuchota maji kwenye madimbwi. Hiyo pesa unaweza kuchimba visima 5, hapo utasaidia wananchi wenzako. Unaweza kurudisha pesa yako, iwapo utafanya kila ndoo ya maji ni shs 100.

inategemea na sehem vipande vingi vya dsm vina maji yw chumvi
 
Nunua Bajaji 3 uzisimamie na upasuke kichw kidogo zitakulipa soon baada ya mwaka unaweza ukawa nazo 7...ila kama unapenda hayo mambo ya biashara za usafiri

hahaha this is something impossible kaka bei ya bajaj moja kwa sasa ni tsh 6.5m mpaka 7m na hioo 10m kivip umiliki bajaj 3 ahah na hata ivyoo bajaj per week inapeleka hesabu kwa bosi ya 105,000/= kwa mwaka piga 54 weeks x 105,000= 5,670,000/=
hapo mwaka umeisha hata pesa uloinunulia bajaj moja haijarud kivip sasa baada ya mwaka uwe na bajaj 7???????????
na bajaj maintenance costs pia unatakiwa uzipigie hapo sioo kumpa mtu ushauriii ambao utamcost baaadae.
 
Ooooh kumbe bajaji kwa wiki ni 15,000/=
 
Habari za asubuhi,

Mimi ni kijana wa miaka 24,ni mwenyeji wa Dar es salaam. Katika kuhangaika nimejitahidi nimekusanya fedha kidogo kiasi cha milion 7,Naombeni ushauri ni biashara gani ya kufanya katika sekta yoyote.

Naombeni michango yenu ya kimawazo
.
 
Kuwa speculator nunua dollar au paundi au pesa yeyote unayoona inalipa after sime days ikipanda utauza na faida utapata
 
Kijana kuna uzi nimeuweka unahusu biashara ya viatu vya mtumba vya kike na kiume kutoka jamhuri ya korea

viatu tunauza kwa bero na vinakuwa mchangayiko kama vile open shoes simple viatu vya mpira boot vya ofisi raba n.k

bei zetu ni kama ifuatavyo.

vya wanaume sh. 220000 kwa bero moja na inapungua kutegemeana na idadi ya bero za mteja

vya kike 130,000 na inapungua kulingana na idadi ya bero anazochukua mteja

NB. bero moja la viatu vya kiume lina wastani wa viatu pair 55 hadi 60 Kwa kawaida 60
vya kike pair 80 hadi 90

PIGA SIMU NAMBA 0758176058 kwa maelezo zaidi na jinsi ya kuweka oda ya mzigo. Pia inapatikana kwa watsap

Viatu ni vya ubora wa hali ya juu na vinaenda na wakati na vingi vinakuja vikiwa kama vipya kwa maana havijatumika sana

TUNAPATIKANA CHANG'OMBE DAR.

KARIBU SANA NA HUWEZI JUTA......
 
je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?

Malila plz nitafute pm
 
Back
Top Bottom