Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Babu njoo huku kusini mwa tanzania ingia vijijini nunua mkaa wa kwenye viroba peleka dar kwenda kuuza inalipa sana ila mwanzo maliasiri watakusumbua ila ukiwazoea hawakunyimi usingizi

Usafiri tu kutoka kusini mpaka Dar ni zaidi ya hiyo milioni
 
Wandugu habari.

Wajuzi wa mambo msaidie huyu Jamaa yangu kanifuata kuniomba ushauri wa biashara ana Tsh.3,000,000/=.nikaona nami Nije kuwashirikisha wadau

Wenye maujzi ni biashara gani anaweza kufanya?
 
Inategemeana na maeneo alipo, lakini hata kama ni mjini au kijijini anaweza kujikita katika ulanguzi wa mazao ya nafaka. Subiri msimu wa uvunaji kisha nunua mazao ya nafaka hasa maharage na mchele kisha weka stoo, kuwa mvumilivu kwakipindi cha miezi michache halafu uza kwabei ya juu. Angalizo nikwamba kama umenunua maharage hakikisha kuwa umeweka dawa yakuzuia wadudu wabunguzi. Au pia waweza nunua mazao hayo yanafaka vijijini yanapolimwa nakuyasafirisha mjini nakuuza kwa bei kubwa kidogo, ila unachotakiwa nikubalansi pesa ya nauli ya mzigo pamoja namengineyo. Ukiwa siriasi kwakipindi cha miaka miwili utakuwa namtaji maranyingi kidogo zaidi ya huo ulionao.
 
Kama anaweza kupata dereva wazuri anunue pikipiki aongezee kama laki nne anunue pikipiki 2. Aingie mkataba na dereva kwa miezi kumi awe anamletea 10,000 kila siku. Ikifika miezi hiyo pikipiki inakuwa ya dereva. hadi itakapofika miezi kumi atakuwa ameingiza pesa ya pikipiki mbili kwa kila pikipiki so anaweza kuendelea na kununua pikipiki nne.

Me nimefanya hiyo na ninaendelea sio biashara mbaya kama unapata madereva makini
 
Me namshauri atafute site nzuri then afungue mabanda ya chips, kwa haraka haraka anaweza kunufungua magoli matatu na kila moja atatumia kama laki tano hiv.

Mlipo ni kukubaliana na wauzaji ,kwa mwanzo inaweza kuwa 15,000.00 kwa siku.Maana yake ni chipsi yai sita na kavu moja.A angalie pesa yake asikabane nao ili apate faida kwa haraka.

Moja na nusu ilyobaki soma upepo kwani katika investment hutakiwi kuweka yoote.likibuma utachanganyikiwa mkuu.ni hayo tuu
 
Hili sio wazo zuri kabisaa.
Jela itamwita,inamaana kila miezi kumi anatafuta madereva wapya.Hii mikataba ya kizamani sana na walioingia kichwa kichwa kwa tamaa,siku hizi mtu anakuletea 50,000 na bado pikipiki inakuwa yako.Ingekuwa hivyo basi hadi watu wa daladala zingekuwa zao.

Rudi giningi we mwali.
 
Inategemeana na maeneo alipo, lakini hata kama ni mjini au kijijini anaweza kujikita katika ulanguzi wa mazao ya nafaka. Subiri msimu wa uvunaji kisha nunua mazao ya nafaka hasa maharage na mchele kisha weka stoo, kuwa mvumilivu kwakipindi cha miezi michache halafu uza kwabei ya juu. Angalizo nikwamba kama umenunua maharage hakikisha kuwa umeweka dawa yakuzuia wadudu wabunguzi. Au pia waweza nunua mazao hayo yanafaka vijijini yanapolimwa nakuyasafirisha mjini nakuuza kwa bei kubwa kidogo, ila unachotakiwa nikubalansi pesa ya nauli ya mzigo pamoja namengineyo. Ukiwa siriasi kwakipindi cha miaka miwili utakuwa namtaji maranyingi kidogo zaidi ya huo ulionao.
Hlili bonge la Plan
 
Me namshauri atafute site nzuri then afungue mabanda ya chips, kwa haraka haraka anaweza kunufungua magoli matatu na kila moja atatumia kama laki tano hiv.

Mlipo ni kukubaliana na wauzaji ,kwa mwanzo inaweza kuwa 15,000.00 kwa siku.Maana yake ni chipsi yai sita na kavu moja.A angalie pesa yake asikabane nao ili apate faida kwa haraka.

Moja na nusu ilyobaki soma upepo kwani katika investment hutakiwi kuweka yoote.likibuma utachanganyikiwa mkuu.ni hayo tuu
Hapa napo patam
 
Fafanua vizuri hapa mkuu kwamba utakusanyaje pesa kwa mchomaji na utamlipaje yaan mnakubaliana hela utakayo mlipa kwa siku? au naje usipouza? nimeipenda hii
 
Ni hiv mkuu,inakua kama mikataba ya mabodaboda au bajaji,kwa gharama ya laki tano ni kama mtaji na vitu vya kuanzia,pia sehemu nyingi za chipsi huwa hawalipi kwa miezi,so ni makubaliano kati yako na mwenye eneo.

Napo sema mahitaji namaanisha,Vit,Meza,sanduku la chipsi,pango lasehemu ,viazi,mishkaki,kuku hata wawili kwa kuanzia,kachumbali na mengineyo.

Kuhusu mkataba badala ya kukubaliana nae kumlipa kwa siku au kwa sahani.wewe unamwambia nitafutie 15,000.00 kwa siku vingine ni juu yako.kama sehemu ipo vizur unaweza ukaona wivu kwani kiepe kina pesa balaaa.NB:WATANZANIA TULIO WENGI HATUPIKI SOO NDO TUNAPOJIDAI HAPO.

Kribu mkuu kwa swali zaidi
 
😊Mkuu hoja yako nimeipenda watanzania tulio wengi hatupiki bali tunashindia chips tu, hivyo kiepe kinalipa sana
 
5 - tafuta mtu muaminifu aliyeko mwanza au ukerewe au unaweza kwenda mwenyewe kuchukuwa aina mbalimbali za samaki wanaopataikana huko kwa bei nzuri na kuja kuuza huko unakoishi. Unaweza kununua bidhaa kama nguo, viatu na urembo katika miji mikubwa kama Dar na kuuza huko (mwanza na ukerewe) wakati unaenda kununua samaki (hivyo utakuwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja).
Idea imesimama sana mkuu.
Heko kwako....
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom