Mtaalamu wa uchumi (CCM) apigia chapuo sera ya CHADEMA ya serikali ndogo

Waishi nchi gani au wewe ni Mkenya?
Ufisadi ndo unasababisha mtu asiwe mwajibikaji kwani anajua kuwa atapata kila anachotaka
Au unahatred na CDM?
 
Huwezi kutawala nchi bila mipango ya kiuchumi hata siku mmoja...nakumbuka Slaa alishawahi kusema siku mmoja kwenye sera yake ya uchumi wakati wa kampeni za urais kuwa Chadema wakichukuwa nchi mfuko wa Saruji mmoja utauzwa Sh5000 lakini hakuonyesha njia atafanyaje mpaka hiyo bei ishuke.

Mkuu unajikamua kweli kweli kama Maulid Kitenge redioni.
 
Huyu jamaa naisi katumwa sasa msichangie hoja yake mtampa mailej sana wakati hastaili asiejua maana msimwambie kwanza namshangaa sana hii Nchi si ya Ccm ni ya watanzania wote.
 
Tangu chukua chako mapema .ccm.watawale watu weng wanashindwa kuwa wakwel.ni kwamba hk chama kinaubaguz,manake kama wewe upo kwenye system bas huwez kumbuka wengne,bora chadem ipate nch then ikosee tuone.
 
Ng'ombe ni ng'ombe tu, ukimwekea keki na nyasi mbele yake, ni lazima atakula nyasi tu! Na keki ataiacha kama ilivyo. Utumwa wa kimwili na mawazo ni hatari sana. Pole mleta thread hii.
 
Mkuu Nakei,
Ni kweli nakubaliana na wewe kwenye hii thread yako katika suala la uchumi Chadema siku zote uwa sio sera yao sera yao kuu ni ufisadi na maandamano yasiyokuwa na tija kwa taifa.

Hata ukiwasikiliza viongozi wao wa juu kama Slaa, Mbowe, siku zote uwa wanajikita zaidi kwenye suala mmoja tu Fisadi ndio sera yao kuu huwezi kusikia wanaelezea jinsi watakavyowasaidia wa Tanzania kiuchumi.

Ukimsikiliza Mbowe maneno yake ni yale yale...Mpaka kieleweke, Hakuna kulala,Pipoz pawaa, Maandamano nchi nzima.

Slaa, nae maneno yake yale kila siku...Tutafanya nchi isitawalike, Ufisadi, Naipa serikali siku tatu, Tutandamana nchi nzima.

Kwenye suala uchumi kwa Chadema hakuna kitu.

Akili nzuri UKIWA NAYO.

Wewe na muanzisha mada mlitakaje, CHADEMA ianzishe wizara zake na kuanza kukusanya kodi?

Yale mnayoyasikia bungeni ndio sera za CDM kuhusu jambo husika. Kama huwezi kuona uhusiano wa ufisadi na udidimiaji wa uchumi wa nchi basi wewe ni ZERO kichwani.

Labda niwape mfano ndugu zangu BONGO LALAS: Serikali yenu ya MAGAMBA imekuja na mbwembwe za maana zikija na jina KILIMO KWANZA. Hapa tukashuhudia Ubadhirifu, wizi na rushwa katika utoaji wa pembejeo na suala la vocha likawa kizungumkuti. Kwa sasa kumekuwa na ukimya mkubwa juu ya hii story yenyewe ya KILIMO KWANZA na sijasikia mkiuliza. Sasa kama mpaka hapa huoni uhusiano wa UFISADI na kuanguka kwa harakati za kuinua uchumi basi una screw kwenye kichwa imekatika.

Kaa chini tafakari usiwe kama kuku. Ni kuku wa mayai tu ndie hutaga yai leo, likaondolewa na mfuga kuku na yeye (kuku) akataga lingine bila kujiuliza la jana limekwenda wapi.

Ikiwa pipa limetoboka, jukumu la kwanza ni kuliziba tundu na sio kukazana kama JUHA kujaza maji ilhali unajua yatavuja. Kwa akili kama zenu mnafurahia hotuba zenye kuwahimiza kuwajibika kama watumwa bila kuangalia mustakabali wa majasho yenu.

Suala la wewe na huyo mwenzio kutokuona mipango ni suala la udogo wa ubongo wenu na sio kosa la CHADEMA. Narudia tena, ni UJUHA kuweka mahindi katika ghala lililosheheni panya. Tutaua mapanya buku yote kwanza ndio turudi kuweka mazao ghalani.

Au kama mmetumwa na Mkulo kutuhimiza kujaza zaidi ili muibe, mwambieni tumeshtuka. Period!
 
hongera kwa swali zuri, na kwa hakika majibu umeyapata! hebu fikiria kwanza na kuwa mchunguzi kabla hujaweka post yako humu. unajua nini, watu tunakuona kama mtoto wa fisadi fulani au shushu, ukiwa na maswali na mawazo ya kishamba kama hayo. o.k? kesho usirudie wapo watakaokosa uvumilivu watakutukana.
 
Nakei, mimi kila siku namshukuru Mungu kwani uligombea ubunge Iramba mashariki na tukakupiga chini ndani ya kura za maoni, kipigo cha mbwa mwizi! Wewe ni mbumbumbu kwa kila kitu. Go to hell...

Poleni sana wana Iramba. Ni dhalili kwa jimbo lenu kuwa na mgebea wa namna hii. Kile kitendo tu cha yeye kufikiria kugombea jimbo lenu ni kuwadharau. Atawezaje kufikiri nyinyi ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama yeye kuwa muwakilishi wenu.

Kwa kweli mngemchagua mngestahili voboko wote. Hongereni na asanteni kwa kumburuzia nje mbali. Chaf chaf, NJE!
 
Mkuu Nakei,
Ni kweli nakubaliana na wewe kwenye hii thread yako katika suala la uchumi Chadema siku zote uwa sio sera yao sera yao kuu ni ufisadi na maandamano yasiyokuwa na tija kwa taifa.

Hata ukiwasikiliza viongozi wao wa juu kama Slaa, Mbowe, siku zote uwa wanajikita zaidi kwenye suala mmoja tu Fisadi ndio sera yao kuu huwezi kusikia wanaelezea jinsi watakavyowasaidia wa Tanzania kiuchumi.

Ukimsikiliza Mbowe maneno yake ni yale yale...Mpaka kieleweke, Hakuna kulala,Pipoz pawaa, Maandamano nchi nzima.

Slaa, nae maneno yake yale kila siku...Tutafanya nchi isitawalike, Ufisadi, Naipa serikali siku tatu, Tutandamana nchi nzima.

Kwenye suala uchumi kwa Chadema hakuna kitu.
Tija ni "productivity" i.e production per person yaani uzalishaji mali kwa mtu mmoja.
Hakuna maandamano yenye tija hata siku moja ndugu yangu! Maandamano sio tendo la uzalishaji mali! Maandamano ni moja ya namna watu wanaweza kuonesha hisia zao na lengo lake ni kupinga au kuunga mkono jambo fulani kwa wakati huo. Hiki Kiswahili tunakipeleka wapi?
 
Huwezi kutawala nchi bila mipango ya kiuchumi hata siku mmoja...nakumbuka Slaa alishawahi kusema siku mmoja kwenye sera yake ya uchumi wakati wa kampeni za urais kuwa Chadema wakichukuwa nchi mfuko wa Saruji mmoja utauzwa Sh5000 lakini hakuonyesha njia atafanyaje mpaka hiyo bei ishuke.

mnataka kuiga?
 
Poleni sana wana Iramba. Ni dhalili kwa jimbo lenu kuwa na mgebea wa namna hii. Kile kitendo tu cha yeye kufikiria kugombea jimbo lenu ni kuwadharau. Atawezaje kufikiri nyinyi ni wajinga kiasi cha kumchagua mtu kama yeye kuwa muwakilishi wenu.

Kwa kweli mngemchagua mngestahili voboko wote. Hongereni na asanteni kwa kumburuzia nje mbali. Chaf chaf, NJE!
Tulimchinjilia baharini mapema kabisa kwa sababu huyu jamaa ni kiwavi.
 
Mkuu uwanja wa kwako sisi wengine tunajifunza matusi na kejeli kutoka kwako...
Hapa hakuna matusi wala kejeli bali ni ukweli mtupu. Tatizo lako wewe unafikiri kama kuku aliyekatwa kichwa [ headless chicken ]
 
Inaonekana wewe hujawahi kuhudhuria mikutano ya chadema wala kusikiliza bunge Zitto anavyomwaga sera
 
Sasa kanda ya Ziwa mfuko wa saruji unauzwa zaidi ya shs. 20,000 je uliambiwa ulielezwa jinsi utakavyopanda! Na bado?
Ili kupunguza bei hujui Serikali yaweza kutoa ruzuku kwa wazalishaji na kuondoa kodi. Pia kusimamia mfumo wa usambazaji kwa hayo machache tu wanaweza kupunguza bei. Kingine ni serikali kuanzisha viwanda vyake au kuwa na hisa za nyingi kwenye viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za mlaji ili kuwafanya wananchi wawe na maisha bora.
 
Back
Top Bottom