Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Habari, mimi ninatatizo na koo langu baada ya kubalehe nimekua na sauti nzito sana ikiambatana na makohozi ambayo kama yana vumbi sasa nashindwa kuelewa ni tatizo japo sijawahi kwenda kwa daktari yeyote juu ya hili pia nahofia isijekua kansa maana baba yangu mdogo alikua nayo ya koo. tafadhari naomba msaada wako
Mkuu ungeenda hospitali kwanza ukapime vipimo ili utapokuja tena uweze kusaidia nini cha kufanya
 
Mkuu ungeenda hospitali kwanza ukapime vipimo ili utapokuja tena uweze kusaidia nini cha kufanya
nilikuwa na tatizo hilo makohozi yanakuwa mengi katika koo pia hata kwenye kuongea unaona yanakuzui kuongea alafu kukohoa sana nilikuja nikaenda hospitali moja ipo magomeni mwembe chai inahusika na ENT nikapewa dawa ila ilichukua muda nikaja kuona nimepona ile hali
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

View attachment 361607

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.










Nakupongeza kwa kujitolea kutuelimisha kuhusu magonjwa mbalimbali. Nina ndugu yangu ambaye anasumbuliwa na kuumwa viganja vya mikono kulikochanganyika na ganzi usiku wakati amelala kabla hajapatwa na usingizi. Ni muda sasa tokea apatwe na tatizo hili. Naomba msaada/ushauri.
 
Habari Daktari. Mimi nina tatizo la kukohoa mara kwa mara hususan koo huwa linakereketa sana. Nimetumia dawa nyingi bila afueni. Naomba msaada wako.
 
Mkuu unakula mlo gani nspenda hili tatizo lingefsmia kwangu
Mkuu nakulanga vyakula vya kwaida kama ndiz nyama, ungali, wali, tambi, almost vyakula vyote ila sanasana nikiwa hapa dar ni ungali, wali, na chips.
 
heshima kwako daktari mimi tatizo langu ni kwamba sikio la upande wa kulia kuna wakati lilikuwa linapiga kelele sana nikaenda kwenye hospital kadha wakani mulika na vifaa vyao wakasema hilo tatizo huwa linatokea kisha linaweza kuisha lenyewe sasa ni mwaka unaisha lile tatizo lipo ila siyo muda wote nikiwa nimechoka huwa linatokea au nikiwa na mawazo sana hiyo hali inanisumbua na nikijaribu kupiga push up hiyo hali hutoweka naomba msaada wako daktari
 
DR POLE ya kazi
nashukuru kwa moyo wako wa kujitolea kutusaidia angalau kujua matatizo yetu na baadae kupata matibabu sahihi.
Mimi nina mfanyakazi wangu ana matatizo mawili
i)anapenda sana kutafuna mifuniko ya chupa za maji,soda kila wakati
2) analalamika sana kuumwa miguu wakati amekaa,hivyo mara nyingi anapenda miguu kukaa imenyooshwa juu ya kiti au kulala.hali hii ameishi nayo zaidi ya miaka 3
huyu ni jinsia ya kike umri wa miaka 29
 
naomba kufahamu dawa nzuri ya kutibu ugonjwa wa Typhoid sugu, asa kwa kutumia dawa lishe?
 
mbona tunakula sawa tu basi una bahati mkuu
naomba unisaidie hili tatizo daktari
heshima kwako daktari mimi tatizo langu ni kwamba sikio la upande wa kulia kuna wakati lilikuwa linapiga kelele sana nikaenda kwenye hospital kadha wakani mulika na vifaa vyao wakasema hilo tatizo huwa linatokea kisha linaweza kuisha lenyewe sasa ni mwaka unaisha lile tatizo lipo ila siyo muda wote nikiwa nimechoka huwa linatokea au nikiwa na mawazo sana hiyo hali inanisumbua na nikijaribu kupiga push up hiyo hali hutoweka naomba msaada wako daktari
 
Dawa ya fangas pembeni ya mapaja au kweny miferej ya mapaja inanitesa San mm kidog ni mnene

Sawa. Ushauri wangu ni yafuatayo:

1. Baada kumaliza haja kubwa na ndogo hakikisha una kausha pembeni ya mapaha na miferej ya mapaja.
2. Usivae nguo za ndani ya kubana.
3. Tumia Dawa Hizi:
- Terbinafine Tablets 250mg; Kidonge kimoja kila siku asubuhi kwa muda wa miezi moja
- Terbinafine Cream; pakaa kutwa mara mbili, asubuhi na usiku kabla ya kulala kwa muda wa miezi moja.

Asante.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom