Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Naomva kujua uzito sahihi wa mtoto wa umri wa miaka 5 kiume na 4 wa kike angalau range ya uzito au hata formula ya kujua weight ya mtoto acording to umri
 
habar nimerudi tena mi ni mvulana umri miaka 24 sasa lakini na tatizo la kujichua sana yani haipiti siku bila kujichua na kwa siku nafanya tendo hili kama dozi vile hata mara 4 kwa siku yani balaa tupu. Naomba msaada kwa hili ata wa kimawazo tu unatosha....
 
Mkuu, niambie unavyoendelea baada ya siku 3. Je uvimbe unaongezeka? Je kichwa inaendelea kuuma? Je una homa?
Uvimbe umepungua kidogo na kichwa hakiumi ,napata maumivu kidogo eneo ya koromeo
nilienda hospitali(kairuki) nikawapima damu (fullblood pict)wakasema ninabacteria infection wakanipa dawa (antbiotics)sizijui jina lakni naona bado hali haijawa nzuri sana


Naomba msaada tafadhali maana hali siyo nzuri kwa sasa
 
Dr ,kwa mara ya kwanza jana nilipitia uzi huu,sikuwa najua kuwa unamafundisho kiasi iki na ni muhimu sana kwetu watanzania tuishio mbali na huduma za afya ,Mungu akubariki kwa msaada huu unaoutoa bure kwa Watanzania ,nina amini wengi wamenufaika na ushauri wako muhimu.
Dr Mimi nina tatizo kubwa la tangu ujana wangu la kutoa harufu mbaya mdomoni,nalijua ilo tatizo na kadri nilivyokua nilijaribu mbinu mbalimbali na tiba tofauti bila mafanikio,nimetumia kila aina ya mouth wash,napiga mswaki kutwa mara nne,nimetumia kila aina ya dawa ya meno iliyoko sokoni sijawahi kupata relief na honestly huu ni aina ya ugonjwa unaomkosesha mtu amani na confidence.
Nimewahi kushauriwa niwaone wataalamu -specialist wa kinywa na koo,nikaenda Bugando nikapimwa lakini Dr akaniambia haoni tatizo na akanipa vidonge vya vitamin.Nimedumu na ili tatizo muda mrefu na siumwi meno wala nini.Niliposoma ushauri wako kwa watu mbalimbali,nkapata faraja na kuona kuwa hatimaye nimepata mtu anayeweza kuelewa tatizo linalonikabili na kutoa ushauri wa tiba.
 
Naomba ushauri wako juu ya ugonjwa wa prostatitis,au maambukizi sugu ya prostate.Yamekua yananisumbua sana kwa miaka mingi bila mafanikio.Maumivu kwa pelvic floor,kwenye testicles etc
 
Nina matatizo mawili doctor ,1 sehemu ya koo inakwaruza sana nikimeza mate nahisi kuna michubuko ila sikohoi kuna kipindi nilikuwa siwezi kuongea sentensi ndefu nakwama,2 nina tatzo la chest nodules painless hili ni la mda mrefu, naomba kujua tiba yake
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

View attachment 361607

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.








Dr tatizo la magoti kutoa sauti kama kuna msuguano husababishwa nanini?na tiba yake ni nini??
 
Nasumbuliwa na miguu ifikapo usiku inauma sana kiasi kwamba sipati usingizi.nikitembea nakua kama vile nakanyaga mawe lakin haija vimba iko kawaida tu...hospital nmeenda nmeambiwa sina tatizo.msaada mkuu
 
Mm Nina Tatzo La Kuumwa Joint Na Mifupa,napata Joto Kali Na Nguvu Zinaisha,pia Napungua Mno Na Huu Ni Mwaka Wa Sita Na Experience Hali Hii.Nmeshatmbea Hosptal Kadhaa But Sijapata Tba Sahihi Zaid Ya Kunipima Uti Maralia Au Typhod Na Huw Cpatwi Sana Na Matatizo Hyo.Nmeshapima Vpimo Vngne Km Vile Kisukar Ukimwi Na Hata Pressure Zaidi Ya Mata Mbil Cna Tatizo Asa Sijajua Ni Kipimo Kipi Nkapime Ili Kugundua Kinachonisibu Msaada Tafadhal Napata Shida Mno Nashindwa Hata Ksoma Vzuri.Nina Miaka Ishrin Na Nne
 
Dr pole na majukumu ya kila siku ya kuitumikia jamii! Naomba msaada wako Dr...
Kuna vinyama au niviite vipele vinaniota kichwani (upande wa kilia wa kichwa karibu na sikio la kulia) taratibu na huwa vinaongezeka taratibu sana, toka nimetambua ni kama miaka mitatu sasa(Hakuna maumizu nayopata wala muwasho na huwa navijali kipindi napoenda sallon kunyoa) nikivikandamiza kwa nguvu naskia maumivu. Sijui ni ninina je vina tiba?
 
Dr pole Na majukumu, Kuna Mtu wangu WA karibu alipata mimba lakini, bahati mbaya imetoka, Dr amemwambia y'a kuwa kizazi chake kimelegea, Je anaweza beba mimba tena ama Ndo itakuwa hivi kila akibeba.
Aliwahi toa mimba akiwa mwanafunzi.
 
Dr Nina kitu kama kohozi kwenye koo linaleta hali ya kukera, kuna wakati linapungua lakini nilipata vumbi kidogo linarudi... Ushauri wako jinsi ya kuiondoa hali hii
Asante
 
Nini Tiba ya Mtoto mwenye mwaka na nusu ana kama kauvimbe kidogo juu ya kitovu , tulichek tukaambiwa kitovu hakijafunga vizuri , muda mwingine tumbo linajaa gas . Majibu dokta
 
Doctor naomba kujua matibabu kamili ya Scabies manake nishatumia dawa naona kila mara ugonjwa unajirudia
 
Dr. Kwanza nikupe pongezi kwa kujitolea kusaidia jamii wachache wenye moyo huo, ila nataka kujua je una ofisi? Iko sehemu gani? Mimi nipo Sumbawanga nataka kuja dar nikutafute unisaidie maradhi yangu. Ubarikiwe
 
ivi kwa mwanaume kukaa muda mrefu bila kushirik tendo kuna madhara yoyote ?? au ngiri inahuusiano na tendo LA ndoa??
 
Back
Top Bottom