Mtaalam wa Microsoft Excel

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Namtafuta, miongoni mwenu, mtaalam wa Microsoft Excel, atakayeweza kunitengenezea document itakayofanya kazi hii:

Sales Invoice

Invoice inatakiwa kuwa na worksheet mbili.

Worksheet ya kwanza ni ile ambayo itajazwa kuonesha ni bidhaa gani zinauzwa, jina na anuani ya mteja, jina na anuani ya mwuzaji, na gharama zote, zikiwa ni pamoja na usafirishaji wa bidhaa na kodi stahiki.

Worksheet ya pili itawekewa orodha ya bidhaa zinazouzwa na bei ya mauzo ya kila bidhaa moja (unit price), na kupewa alama (Code) maalum.

Kinachotokea ni kwamba, kwa mfano, mtu anauza spare za magari, kama ni tie-rod end, basi inakuwa na Code yake. Akiiweka kwenye mahali husika, maelezo ya bidhaa yanatokea mahali husika (mstari mmoja chini yake) na bei inatokea kwenye column mbili zifuatazo upande wa kulia, column ya kwanza anaweka idadi ya bidhaa zinazouzwa, chini kabisa majumlisho yote yanafanyika.

Je, tunaye mtaalam wa kuweza kufanya kazi hii?

Faida ya document hii ni kwamba, mwuzaji anachotakiwa ni kubadilisha bei na bidhaa, na kuacha Codes zikiwa pale pale, au anaweza pia kubadilisha codes. Invoice ya namna hii inaweza kurekebishwa kukidhi mahitaji ya sekta yoyote ile, hata kwenye mambo ya stationeries pie, kwani hakuna tofauti kubwa kwenye mfumo wa kibiashara.

Asanteni.

-> Mwana wa Haki
 
kwanini usitafute ile program ya POS, [oint of sales, inakuwa imekamilika kila kitu mpk deatils unakonunuambei percentage unayouzia,yaani ni mwisho wa tabu yako ya kibiashara.
 
Mbona ni rahisi, ni PM then nikuelekeze kwa kijana wangu mmoja akutolee hiyo kitu in few minutes.
 
Back
Top Bottom