Mtaala watinga Star TV: Kamishna wa Elimu Ndani ya Star TV Live

ngongeki

Member
Dec 17, 2012
81
36
Wadau ule mzimu wa Mtaala leo unaongelewa ndani ya Star TV. Kamishna wa Elimu yuko Star TV
anaongea kuhusu maana ya mtaala, wenye muda fuatilieni, je atakidhi kiu ya Mbatia?

Stay tuned
 
Anajikanyaga anasema mtaala upo lakini siyo kitu kinachoweza kutumika kwa mtu wa kawaida,
Ina maana walimu na siye siyo watu wa kawaida mbona hatuoneshwi huo mtaala?
 
Inanikera hapa Tanzania huwezi kujua ni nani mtaalamu ma nk yupi mwana siasa yaani nchi imekuwa ya ajabu bla blaa tu. Mradi kuche jua lizame. Ifike mahali wataalam wssimamie ukweli na wana siasa wasimamie uongo. Mimi nasema hakuna mitaala ya elimu Tanzania. Ukweli utaniweka huru.
 
Ndiyo maana nchi haiendelei yaani anasema eti kuna Taasisi ya Elimu lakini Wizara ndiyo mama kila kitu lazima iamue. Tatizo la Wizara kuingilia kazi za utaalamu zimazoganywa na taasisi zake ndizo zilimpa Mungai kiburi cha kuanzisha vitu vya ajabu kama vile Physics with Chemistry, akafuta Michepuo n.k. Kwa mtaji hio tutafika?
 
Bado hajaweza kueleza kama kweli mtaala upo. Kama ni kitu ambacho hakina manufaa kwa mtu sasa kwa nini waliahidi kuutoa kwa Wabunge? Yaani kuna mkanganyiko mtangazaji amemuumbua anasema kuna syllabus inayoonesha majukumu ya Idara ya Sekondari na mojawapo ya jukumu limeandikwa kuratibu ukuzaji mtaala, mkanganyiko ni mkubwa kwa sababu mara Kamishna anaidhinisha, TIE wanaandaa, Sekondari wanaratibu. Kwa maana hiyo wa msingi unaratibiwa na Idara ya Msingi. Kweli kuna kazi Taasisi ya elimu inaingiliwa mo na wizara
 
Mtaala unatakiwa kubeba mtazamo wa nchi juu ya elimu kwa muda wa miaka zaidi ya kumi, kwa sasa mtaala wa elimu umebebwa na waziri wa elimu+ wanasiasa, wana nguvu ya kutegua na kubadili chochote.kwa sasa hakuna mitaala iliyowazi. Cha ajabu professional people are toothless to talk about this issue, they only elaborate what politicians have said.they become stepping stone to politicians
 
Jana kwenye Clouds Fm Mh. Mbatia alizungumza nengi kuhusu ufeki wa mitaala iliyowasilishwa bungeni. Akaendelea kusisiiza kuwa nchi haina mtaala rasmi na kuwa ana barua ambayo iliandikwa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa Mtafiti mmoja aliyekuwa anaomba mitaala ikimjulisha kuwa hawana ntaala rasmi ila wana rasimi. Amedai kuwa mtaala uliowasilishwa Bungeni haujatiwa saini na mtu yeyote na hata cover page haina nembo yoyote kitu ambacho kinaufanya usiwe rasmi.. Sasa ni vema huyo Kamishna naye ajitokeze atoe ufafanuzi kuhusu madai hayo kwani hili suala linatuchanganya na huku shuleni hatujawahi kabisa kuuona mtaala na pia nimejaribu kwenda kwenye ofisi za Elimu hawana hizo docs.

Tunaomba ufafanuzi wa serikali vinginevyo inaonekana madai ya Mbatia yalikuwa sahihi
 
Anajikanyaga anasema mtaala upo lakini siyo kitu kinachoweza kutumika kwa mtu wa kawaida,
Ina maana walimu na siye siyo watu wa kawaida mbona hatuoneshwi huo mtaala?
Hata REO wa Dododma alikuwa hana mtaala, kichekesho kweli. Serikali dhaifu.
 
Back
Top Bottom