Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.
Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!
Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.
Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?
========================

========================Samahani wanaJF, hivi Mswahili ni nani?
Kwa nijuavyo, mswahili ni mtu anaejua kiswahili na anayeongea sana maneno mazuri mazuri yenye ahadi nzuri nzuri ambazo hazitekelezi, yaani ana uongo mwingi kuliko ukweli.
Baadhi ya wabara wakifika pwani hujaribu kuiga uswahili na wengine wanafanikiwa kuwa waswahili wazuri!!
Kwa jumla, waTZ wengi wana uswahili kuliko waKenya na waGanda. Ndiyo maana sisi waTZ tuna maneno mengi kuliko vitendo!! Siasa siasa tu zisizo tafsirika katika vitendo!! Matokeo yake tuko nyuma kimaendeleo licha ya juwa na raslimai nyingi majirani zetu!!
Tuache uswahili ili tuendelee!! Tuache kuongozwa na waswahili!!
SAMAHANI KWA NILIOWAKWAZA!!
Asubuhi njema!!
=============================Wanajf naomba tu share changamoto niliokutana nayo. Leo asubuhi nikiwa kwenye daladala naelekea mjini kati. Baada ya kuwaza na kuwazua, karibu yangu alisimama mtoto wa kike I think she is at 7 or 8 aliyekuwa amevaa sare za shule.
Kwa kuhisi kuwa yuko embarased kutokana na foleni, nikaamua kum keep bize kwa kumpa recognition kwa kumuuliza maswali ya kitoto ya hapa na pale ali mradi tu tufike bila ya uchovu. Unaishi wapi, Unaitwa nani, unasoma shule gani na darasa la ngapi. Nikamuuliza huku nikiwa sina uhakika kama nitajibiwa vizuri swali langu. Nilishtushwa na uwezo mkubwa wa kujieleza baada ya kujibu kwa ufasaha maswali yangu ya mpigo. Du!! Nikajiona Chief mzima napigwa TKO kutokana na jibu la mtoto kwani wahenga walisema kuwa jibu likisadifu swali, ni kama kiu iliyokatwa kwa maji safi ya kisima cha chemchem.
Mtu mzima sikutaka kushindwa kirahisi.nikamuuliza swali lingine ambalo niliamini kuwa litamsumbua kutokana na umri wake. " Umesema unaishi Kimara, Wewe ni kabila gani?" Huku nikitegemea jibu la "Mimi ni Mchaga" kutokana na maeneo mengi ya Kimara kugeuzwa kuwa mashamba ya Migomba kutokana na kukaliwa na Wachaga wengi, nilishangaa kusikia jibu alilolitoa yule mtoto. Kwa kujiamini alijibu "Mimi ni Mswahili" Huku nikiwa siamini masikio yalichosikia, nikamuuliza tena. "Umesema wewe ni kabila gani?" Akijibu kwa msisitizo na kujiamini, alisema "Mimi ni Mswahili" Nikajiona Chief mzima leo ninalo.
Nikajitutumua na kuuliza tena. "Kwa nini unasema wewe ni Mswahili. Kwani baba yako ni kabila gani." Kwa kujiamini akajibu. "Baba yangu ni Mhehe na Mama yangu ni Msukuma. Na kwa kuwa wazazi wangu ni makabila tofauti, mimi ni Mswahili kwa kuwa sifuati mila yoyote wala situmii lugha yoyote ya wazazi wangu zaidi ya Kiswahili".
Ghafla nikasikia sauti ya Konda, "Akiba wa kushuka". Nikajibu "tupo" bila ya kujali kuwa sikutumwa na mtu yeyote kumjibia. Nikashuka zangu huku nikijiuliza MSWAHILI NI NANI?
=========================Habarini wadau,
Kwa kawaida neno mswahili limekuwa likitumiwa kumaanisha haya
-Mtu wa hali ya chini (kiuchumi) na anayeishi uswahilini
-Pia mara nyingine humaanisha mtu ambaye ana sound nyingi au muongomuongo,utaskia "Acha uswahili wewe"
-Pia watu wengi wa mikoani (especcially wakristo) wanawachukulia waswahili ni waislam wa pwani,Dsm na hata zanzibar
-Lakini pia watoto wa mjini wanawachukulia mswahili ni mjanja mfano utaskia "Mimi ndio mtoto wa kiswahili/kiswazi huwezi niingiza kingi"
SWALI: Mswahili haswa ni nani? Au ni yeyote anayezungumza kiswahili? Kuna kabila la Waswahili?